Na Chalila
Kibuda,Globu ya Jamii
VIONGOZI wa nchi
wametakiwa kushiriki katika mkutano wa umoja wa Mataifa wa kujadili malengo 17
ya maendeleo endelevu utaofanyika Septemba 25 mwaka huu nchini Marekani.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa
Mtandao wa Mabadilliko ya Tabia nchi (CAN), Sixberty Mwanga ,amesema kuwa
mkutano huo ni muhimu katika kuweza kutekeleza eneo la mabadiliko ya tabia nchi
kutokana na kadri ya siku zinavyoongezeka hali ya ukame inazidi kuongezeka.
Amesema kutokana na
kuongezeka kwa kasi kwa mabadiliko ya tabia ya nchi
nchi inatakiwa kutumia dola za Kimarekai bilioni 1000 kwa mwaka
na hiyo inatokana na mabadiliko katika ukame na utowekaji wa maji pamoja na uharibifu wa miundombinu inayotokana mafuriko.
Aidha amesema mkutano
wa maendeleo endelevu unahitaji utashi wa kisiasa wa kuweza kufanikisha malengo
ya hayo ikiwemo suala la mabadiliko ya tabianchi ambalo linahitaji rasilimali za kutosha.
Mwanga amesema mabadiliko ya tabianchi yanasababishwa na
vitu vingi ambavyo vinatkiwa kuepukwa kwa kuweza kutumia vitu asili kama
matumizi ya nishati mbadala.
“Malengo 17 ya
Maenndeleo Endelevu utekelezwaji wake itawezekana kama dhana ya mabadiliko ya
tabianchi yatazingatiwa kwa vitendo”amesema Mwanga.
Aliongeza kuwa
kuongezeka kwa njaa ikwa ni lengo la maendeleo endelevu ambayo inatokana ukame
ambao umebasababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko hali ya hewa ,Sixbart Mwanga akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusiana na mkutano wa maendeleo endelevu ya mabadiliko ya tabia ya nchi utakaofanyika nchini Marekani Septemba 25 mwaka huu.
Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko hali ya hewa ,Sixbart Mwanga akizungumza na waandishi wa habari npamoja na wadau wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa jijini Dar es Salaam leo, kulia ni Mhasibu wa Mradi wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa, Erick Makere
Kulia ni Afisa Mradi wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa, Onditi Msololo na Mhasibu wa Mradi wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa, Erick Makere wakimsikiliza Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko hali ya hewa ,Sixbart Mwanga leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa leo jijini Dar es Salaam.





No comments:
Post a Comment