Mwanafunzi wa Zamani wa Forodhan,Mariam Zialor akizungumza wakati wa uzinduzi wa umoja wa wanafunzi waliosoma shule ambayo kwa sasa ni St.Joseph Cathedral leo jijini Dar es Saalaam.
Mwananfunzi wa zamani wa shule ya Sekondari ya St.Joseph hivi sasa, Ashymaa Kwegyry akizungumza katika uzinduzi wa umoja wa wanafunzi waliosoma katika shule hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Wanafuzi walohitimu mwaka 2014 wakisoma lisala ya shule hiyo, Damian Mapalala na Nancy Kimario.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
WANAFUNZI
waliosoma Shule ya Forodhani na Sasa St.Joseph
Cathedral wameanzisha umoja wa shule hiyo kwa ajili ya kusaidia elimu
pamoja na masuala ya kijamii.
Wakizungumza
nyakati tofauti wanafunzi waliosoma hapo wamewataka wanafunzi kufuata
nyayo zao kutokana na shule hiyo kuwa na historia nzuri ambayo hadi sasa
haijaweza kufutika.
Wamesema
kuwa umoja huo utakuwa imara katika kusaidia shule hiyo katika masuala
mbalimbali ikiwemo na kusaidia jamii kutokana na malezi walioyapata
katika shule hiyo tangu Ukoloni.
Akizungumza katika uzinduzi huo mwanafunzi aliosoma shule hiyo,Mariam Zialor,
amesema umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St Joseph convent
school iliodumu kuanzia mwaka 1932 hadi 1969, na Forodhani
Sekondari ilokuwapo 1970 hadi 2008 ( ilitaifishwa na serikali) na baada
ya hapo St Joseph Cathedral High school 2009 (baada ya kurushwa kwa
kanisa la katoliki) hadi leo inatambulika St. Joseph &
Forodhani ALUMNI .
Zialor
amesema katika shule hiyo kuna wanafunzi waliosoma shule hiyo,
wanaoishi nje ya nchi, wanaotoka Canada, Australia, New Zealand
Uingereza na Seychelles wameungana kuhudhuria mkutano huu wa kishitoria
wa kuanzisha umoja wa ALUMNI.
Amesema baadhi ya wanaWengine hawajafika Tanzania kwa miaka zaidi ya 30. Wanarudi kuona shule iliowalea.
Aidha
amesema katika watu maarufu wanaotoka nchi za nje atakuwapo Jaji Mkuu
wa mahakama ya Rufaa Seychelles ambaye alisoma hapo na kumaliza kidato
cha nne mwaka 1968, na baada ya hapo, kuhamia Seychelles na wazazi wake
alipo kuendelea na masomo ya juu.
Kwa
upende wa Mbunge wa Viti Maalumu ,mwanafunzi wa shule hiyo zamani
Ashymaa Kwegyry ametaka wanafunzi kuwa wadhubutu na kuweza kufanikisha
ndoto zao.
Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari ya St.Joseph zamani wakiwa wameshuriki katika uzinduzi wa wanafunzi waliosoma shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Wapigangoma wakipiga ngoma leo jijini Dar es Salaam leo katika nuzinduzi huo.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo wakiwa wamevalia mavazi ya kimasai mara baada ya kucheza ngoma inayowakilisha kabila la wamasai katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule hiyo zamani.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi waliosoma shule ya St.Joseph
Picha ya pamoja ya wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa Umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St.Joseph mara baada ya kumalizika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule hiyo.
No comments:
Post a Comment