Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuondoka nchini kesho usiku kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye michuano ya Michezo ya Afrika (All Africa Games) inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 3, mwaka huu.
Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa TFF, Twiga Stars haikuondoka leo kuelekea nchini Congo – Brazzavile, Shirikisho bado linasubiri mwongozo wa Wizara ya Habari,Viajana, Utamaduni na Michezo.
Imani ya TFF ni kuwa timu itasafiri na kuwahi mechi ili kuepuka hatari ya kuadhibiwa na CAF ikiwa ni pamoja nan a kulipishwa fainai au kuondolewa kwenye michuano hiyo.
Mchezo wa kwanza wa Twiga Stars katika michuano hiyo utakua dhidi ya Ivory Coast tarehe 6, Septemba, mchezo wa pili dhidi ya Nigeria Septemba 9 na mchezo wa mwisho katika kundi hilo utakua dhidi ya Congo-Brazzavile Septemba 12, 2015.
Timu mbili kutoka kundi A zitaungana na timu mbili nyingine kutoka kundi B kucheza hatua ya nusu fainali.
No comments:
Post a Comment