Mpenzi wa bia ya
Tusker aliyefahamika kwa jina la Kikya Mathias akizungumza na
mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash kabla ya kupokea zawadi yake ya mfuko na fulana wakati wa hafla
ya kuipongeza baa ya Coast Pub iliyopo Tangi Bovu-Mbezi Beach jijini
Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya
Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Akijiandaa kutoa
zawadi hiyo (nyuma yake) ni Balozi
wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi. Lengo kuu la kampeni hii ikiwa ni
kuzifikia baa mbalimbali jijini Dar na mikoani na kuzihamasisha kufanya
kweli linapokuja suala la utoaji huduma kwa wateja lakini pia kuzisaidia
baa hizo kuongeza mauzo ya siku wakati wa promosheni.
Mkazi wa Kibaha-Pwani Bi Emelda Joseph akipokea zawadi ya fulana toka kwa Msimamizi wa Mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ubungo Victor Mhindi katika
hafla ya kuipongeza baa ya Miti Mitatu ya Kimara-Korogwe jijini Dar es
salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya
Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker
Mshereheshaji wa
kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash (aliyesimama) kwenye picha
ya pamoja na Bw. Cheni Omary ambaye alijishindia bia za bure na fulana
wakati promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani ilipokua ikiendelea katika
kiwanja cha Miti Mitatu kilichopo Korogwe jijini Dar es salaam.
Mteja wa bia ya Tusker Ezra Mlawa (katikati) akizungumza na mshereheshaji wa kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash (kulia) mara baada ya meza yake kufikiwa na zawadi ya bia za bure na fulanakatika
hafla ya kuipongeza baa ya Miti Mitatu iliyopo Kimara-Korogwe jijini
Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya
Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. (Kushoto) nibalozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi. Tofauti na jiji la Dar, kampeni hiyo pia inaendelea mikoa mbalimbali nchini kama Arusha, Moshi, Mwanza, Morogoro na Mbeya.
Mteja wa bia ya Tusker Bi. Elizabeth Ulomi (katikati) akipokea zawadi yake ya mfuko wenye fulana toka kwa Msimamizi wa Mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Mbezi Beach Obedi Salema (kulia) wakati wa hafla ya kuipongeza
baa ya Coast Pub iliyopo Tangi Bovu-Mbezi beach jijini Dar es salaam
ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani
inayoendeshwa na bia ya Tusker.(kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo Gadner Habash.






No comments:
Post a Comment