UNAJUA
watu wengi hawajawahi kujiuliza maswali kama haya hapa... Kwa nini
Mungu aliumba mito? Kwa nini Mungu aliumba Miti? Kwa nini Mungu aliumba
chuma? Mungu hakukupa vitu vilivyotimia kwa sababu anajua una asili ya
uumbaji ndani yako maana umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, hivyo basi
hakukupa vitu vilivyokamilika ila alikupa vitu ambavyo vitakupelekea
kutengeneza vitu vingine ili uendeleze ule uumbaji ambao yeye
aliuanzisha ,tunajua kabisa kwamba Mungu ni asili ya uumbaji.
Nataka
nikwambie hivi binadamu kawekewa uwezo wa ajabu sana ndani yake na
Mwenyezi Mungu wa kutenda mambo makubwa na ya ajabu ndio maana Mungu
hakukupa vitu vilivyokamilika kama magari,nyumba, ndege,umeme,meza, n.k
ili aliweka ndani yako uwezo wa kutumia mito ukatengeneza madaraja juu
yake na magari yakapiti lakini pia alijua kabisa unao uwezo wa kutumia
mito ukatengeneza mitumbwi ikapita, lakini pia alijua unao uwezo wa
kutumia maji ukatengeneza umeme na ukautumia huo umeme kwa matumizi
mbalimbali kama kwenye viwandani,manyumbani,maofisini na kadhalika.
Pia
Mungu aliumba miti hakuumba meza, wala vitanda ,wala viti,wala mkaa kwa
sababu anajua unao uwezo wa kubadili hivi vitu kuwa vitu vingine kwa
ajili ya matumizi yako na pia ukaendeleza uumbaji wake.
Hebu
angalia tena fikiri kwa kina Mungu kaumba chuma lakini hakuumba gari
ila ndani yako wewe kama mwanadamu aliweka uwezo wa kutengeneza magari
kwa kupitia zile chuma. Sasa swali nakuuliza katika vitu vyoote Mungu
alivyotupa bure kabisa kuna ardhi,kuna maji, kuna anga,kuna hewa, kuna
bahari, kuna maziwa na vingine vingi wewe umetumia kipi kuendeleza
uumbaji wa Mungu hii ni changamoto kwangu na kwako.
Hebu
tazama Wright Brothers waliweza kutumia anga kutengeneza ndege, Hivi
unajua kwamba katika kikao cha mwisho kilichojumuisha wanasayansi 64
wote walisema kwamba haiwezekani kutengeneza ndege ikapaa hewani? Na je
unajua kwamba hao wenyewe tuu ndio walibakia katika kikao kile wakisema
kwamba inawezekana? Na je unajua Baba yao aliwaambia wakifa watachomwa
moto kwa kuwa na wazo kwamba inawezekana kutengeneza ndege na kuirusha
angani? Leo ndege zipo au hazipo?
Nafurahi
hawakumsikiliza yeyote walisimamia wazo lao waliamini inawezekana na
kweli mwisho wa siku waliweza Leo hii tunasafiri kwenda sehemu
mbalimbali duniani pasipo shida ya aina yoyote kwa sababu ya Wright
Brothers, ushawahi kujiuliza kama kungekuwa hakuna ndege watu wakasafiri
kwa mabasi au meli ingekuchukua mda gani kutoka hapa Tanzania kufika
Marekani au Brazil au Canada au Wingereza? Bila shaka ungesafiri hata
miezi miwili mitatu na bado usingefika. Mungu awapumzishe pepa peponi
asante Mungu kwa kuwaumba.
Nakuja
kwako wewe je una mipango mingapi umeiacha kisa watu wamekuambia
haiwezekani? usiwasikilize nakwambia maana watu wengi wameshindwa
kutimiza ndoto zao kwa kusikiliza watu hata kama ni mzazi wako, hata
kama ni rafiki,hata kama ni ndugu ivi kweli jaribu kutafakari haya
maneno kwa kina kama tungefanya kama wazazi wetu walivyofanya mabadiliko
yangekaa yatokee?
Wright
Brothers wangemsikiliza baba yao leo tungekuwa na ndege?anza
kushughulikia mpango wako maadamu unauona katika fikra zako ina maana
unaweza kuutimiliza mimi nakuhakikishia hakuna kitu kitakachoweza
kukuzuia kupata kile unachokitaka labda tuu uamue kujizuia mwenyewe ila
kama kweli umenuia kukitafuta kwa moyo wako wote na ukafuata taratibu
zote za kukitafuta utakipata tuu na sina wasiwasi katika kusema hivi.
Naomba
nimalizie kwa kusema hivi kitu pekee kitakachokuzuia kupata kile
unachokitaka ni wewe mwenyewe na kingine ni kuruhusu maoni ya watu
wengine kutawala mawazo yako kwamba huwezi ukafanikiwa katika hilo
unalotaka kufanya.
IMEANDALIWA NA HUMPHREY MAKUNDI NA ALLARD MINJA.



No comments:
Post a Comment