Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasalimia watoto Othman na Zainab waliokaa kwenye kisiwa kinachosadikiwa kuwa na mafuta katika eneo la Tundauwa.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipandisha bendera katika tawi la CUF Tandani shehiya ya Kilindi lililokuwa chini ya Chama cha ADC, kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi hilo.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wanachama wa wanachama wa Jumuiya ya maendeleo ya wanawake Tundauwa. (Hawapo pichani).
Picha na Salmin Said, OMKR.
Tawi
jengine la ADC la eneo la meli tisa Wingwi, pia lilibadilishwa kuwa
tawi la CUF baada ya wanachama wake kukihama chama hicho.
Na: Hassan Hamad, OMKR
Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad, ametembelea kisima kinachosadikiwa kuwa na mafuta katika
eneo la Tundauwa, na kusema kuwa mafuta ya Zanzibar yatachimbwa katika
kipindi kifupi kijacho.
Amesema
kwa miaka mingi Zanzibar imeshindwa kuchimba mafuta yake kutokana na
kutokuwepo mikakati imara, na kuahidi kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais
wa Zanzibar atahakikisha kuwa suala hilo linawekewa mikakati imara ya
uchimbaji, ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali hiyo muhimu kwa
maendeleo ya taifa.
Kwa
mujibu wa kumbukumbu zilizopatikana katika eneo hilo, kisima hicho
chenye urefu wa zaidi ya futi 12 elfu na mia saba, kilijengwa miaka 53
iliyopita na kuonesha dalili za kuwepo mafuta.
Wakati
huo huo Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
ametembelea Jumuiya ya maendeleo ya wanawake Tundauwa, na kutoa wito
kwa wananchi wa kijiji hicho kujiunga na jumuiya hiyo ili kupata
mafanikio zaidi.
Amesema
jumuiya hiyo inayojihusisha na masuala mbali mbali yakiwemo uhifadhi wa
mazingira na kilimo, imekuwa mfano mzuri wa kuigwa kutokana na
mafanikio inayoyapata tokea kuanzishwa kwake.
“Jumuiya
hii inafanya kazi nzuri ya kupigiwa mfano, hivyo natoa wito kwa
wananchi wa vijiji hivi kujiunga kwa wingi ili kuleta mafanikio zaidi”
amesema Maalim Seif.
Mapema
akisoma risala ya Jumuiya hiyo, bibi Raya Abdallah Rashid amesema lengo
la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kupambana na umaskini, maradhi pamoja
na uhifadhi wa mazingira.
Amesema Jumuiya hiyo pia imekuwa ikiielimisha jamii juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi na dawa za kulevya.
Amesema
Jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 imepata mafanikio makubwa
yakiwemo kutambuliwa kama jumuiya rasmi, kupanda mikoko ekari mbili kwa
ajili ya uhifadhi wa mazingira, ufugaji wa nyuki na kilimo cha mboga
mboga.
Hata
hivyo bi Raya amesema bado wanakabiliwa na changamoto ikiwa ni pamoja
na ukosefu wa jengo la ofisi, na kulazimika kuanzisha ujenzi ambapo
zaidi ya shilingi milioni saba na nusu tayari zimetumika kwa ajili ya
ujenzi huo, na kuomba kupatiwa misaada zaidi ili wamewe ukamilisha
ujenzi wao.
Katika
hatua nyengine Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, amefungua tawi
jipya la CUF Tandani shehiya ya Kilindi lililokuwa chini ya Chama cha
ADC.
Amesema
Tawi hilo limebadilishwa kutoka ADC na kuwa tawi la CUF baada ya
wanachama 25 wa ADC kuamua kujiunga na CUF na kuongeza idadi ya
wanachama wa tawi hilo kufikia 103.


No comments:
Post a Comment