KATIBU wa CCM wa wilaya ya Mufindi Bw. Jimson Mhagama amesema
kuwa chama cha mapinduzi (CCM ) kitaendelea kuongoza kwa kuzingatia uadilifu, , amani,
upendo, utulivu na kuleta maendeleo kwa wananchi wake hivyo kuwataka wananchi
kuchagua cheni nyenye msimamo wa kuwa na diwani, mbunge na rais wa CCM ili
kuendelea kuwaletea maendeleo .
Bw. Mhagama aliitoa
kauli hiyo jana
alipokuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni za
udiwani wa kata ya Bomani kwa kumnadi mgombea wa kata hiyo Bw. John
Chota ,kuwa wananchi waanze kumuunga mkono diwani, na mbunge
anayegombea wa CCM Bw. Cosato Chumi kumchagua kuwa mbunge wa jimbo la
Mafinga
Mjini pamoja na kuelekeza kura zote kwa
Mgombea wa Urais dkt. John Magufuli.
“Uongozi wowote wenye cheni moja ya kutoka chama kimoja ndiyo
unaoweza kuleta maendeleo na hivyo ninawaomba kura zenu mzielekeze kwa diwani
wetu John Chota, Mbunge wetu Bw. Cosato
Chumi pamoja na Rais wetu dkt. John Pombe Magufuli ili kuunda cheni moja ya
mshikamano na kutokana na uwepo wa cheni hiyo kutakuwa na mfumuko sahihi wa
maendeleo kwa wananchi katika sekta zote zikiwemo za elimu, kilimo, afya,
barabara, ujasiliamali, kutunza mazingira, ajira kwa vijana na uwezeshaji wa
akina mama”, alisema Bw. Jimson Mhagama.
Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa cheni moja ya kimaendeleo
uongozi wa awamu ya Tano utakapoingia madarakani utahakikisha kuwa shule zote
za sekondari zinapatiwa umeme, kuendeleza ujenzi wa maabara, kuhakikisha
zinapatiwa walimu wa kutosha na kuongeza
kuwa elimu itatolewa bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari kwa ajili ya
kuhakikisha kuwa watanzania walio wengi
ambao ni vijana wanaelimika na kunufaika na matunda ya nchi yao.
Aidha, alisema kuwa mara baada ya uchaguzi Jimbo la Mafinga
litahakikisha kuwa linajenga stendi kubwa ya kisasa ya mabasi yaendayo mikoani
ambayo yanapita katika Mji wa Mafinga
ambapo alisema kuwa ujenzi wa stendi hyo utagharimiwa na Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii wa LAPF ambapo stendi hiyo inatarajia kugharimu zaidi ya
shilingi Bilioni 3.5 na kuongeza kuwa utendaji huo utakwenda sambamba na
wananchi kuchagua cheni moja ya CCM na siyo kuleta mchanganyo wa wagombea.
No comments:
Post a Comment