SERIKALI
imetwaa jumla ya Ekari 7000 baada ya ubatilishwaji wa Mashamba ya
Tanzania plantatition limited yaliyokua yakimilikiwa na
mwekezaji kutoka nje ,mashamba hayo yanatajiwa kugawanywa kwa wananchi
2000 wenye uhitaji wa ardhi ya makazi na mashamba .
Aidha
baada ya ubatilishwaji wa mashamba hayo Arusha imepata ekari 6176.5 na
Halmashauri ya Meru ekari 925 hivyo kufikia ekari 7101 ambazo
zitagawanywa kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi
Nyumba na Makazi,Wiliam Lukuvi wakati akitoa taarifa ya usuluhishi wa
migogoro ya ardhi katika mikoa ya Arusha na Manyara katika mkutano wake
na Waandishi wa Habari,Lukuvi amesema kuwa mashamba hayo yalikua na
migogoro kwa kipindi kirefu kati ya mwekezaji na Wananchi hivyo kutokana
na uhitaji mkubwa wa ardhi serikali imeamua kubatilisha mashamba hayo.
“Nimekuja
Arusha na timu yangu ambayo itafanya uhakikiki wa watu 2000 wenye
uhitaji na baada ya kujiridhisha watafanya zoezi la ugawaji na pia
wananchi watapatiwa hati ya kumiliki ardhi zao safari hii hatutagawa
ardhi kienyegi” Alisema Lukuvi
Lukuvi
amesema kuwa mbali na shamba hilo pia wamepata ekari 100 katika shamba
la Imani Estate na pia Shamba la Noors lenye Ekari 2296 lililokua na
mgogoro kati ya Mwekezaji na wananchi wa Kijiji cha Laroi na Kisima cha
Mungu litagaiwa kwa wananchi baada ya mazungumzo kati ya Mwekezaji
kukubali kuachia shamba hilo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC ,Fidelis Lumato amesema kuwa ugawanywaji wa mashamba hayo utasaidia kupunguza migogoro mikubwa ya ardhi iliyokua inakabili wilaya hiyo kutokana na uhaba mkubwa wa ardhi.
Jumla
ya migogoro 80 iliyowasilishwa kwa Waziri Lukuvi kutoka katika
Halmashauri ya Jiji la Arusha ,Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na
Halmashauri ya Meru imepatiwa ufumbuzi hivyo kupunguza migogoro ya ardhi
ilikua ikilisakama jiji la Arusha.


No comments:
Post a Comment