JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Benki ya Exim yatoa msaada wa vitabu sekondari Mbeya.

Share This
Meneja wa benki ya Exim Tanzania tawi la Mbeya, Bw Iddy Mwacha(kushoto) akikabidhi msaada wa vitabu vya masomo kwa mmoja wa wanafunzi aliewawakilisha wanafunzi wenzie na uongozi wa shule ya sekondari Sinde iliyopo eneo la Mwanjelwa mkoani Mbeya katika kupokea msaada huo ikiwa ni mwendelezo wa harakati za benki hiyo katika kuisadia serikali kuboresha hali elimu na ufaulu wa wanafunzi hapa nchini. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, uongozi wa shule pamoja na wanafunzi.
BENKI ya Exim Tanzania imetoa msaada wa vitabu vya masomo vyenye thamani ya sh mil. 8/- kwa shule ya sekondari Sinde iliyopo eneo la Mwanjelwa mkoani Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa harakati za benki hiyo katika kuisadia serikali kuboresha hali elimu na ufaulu wa wanafunzi hapa nchini.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu hivyo iliyofanyika kwenye viunga vya shule hiyo mwishoni mwa juma lililopita, Meneja wa benki hiyo tawi la Mbeya Bw Iddy Mwacha alisema msaada huo ni sehemu ya uthibitisho wa namna benki hiyo imekuwa ikipambana kuhakikisha uwepo wake hapa nchini unaleta tija zaidi kwa jamii.
Alisema kipaumbele kwenye elimu ni muhimu kutokana na ukweli kwamba sekta mbalimbali ikemo ile benki ili zifanye vizuri zaidi zinategemea uwepo wa wasomi kuziendesha na jamii iliyoelimika kwa ujumla.
“Ni kutoka na kufahamu ukweli huo ndio maana siku zote tumekuwa tukihakikisha kwamba kile tunachokipata tunagawana na jamii ikiwemo kuboresha ubora wa elimu ili mwisho wa siku tupate matokeo mazuri kielimu,’’ alibainisha.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkuu wa shule hiyo Mwl Shadrack Mwakasyama licha ya kuishukuru benki ya Exim kwa msaada ilioutoa, pia aliwahikikishia viongozi wa benki hiyo kuwa yeye na walimu wote wa shule hiyo watakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha vitabu hivyo vinatumiwa ipasavyo na umakini mkubwa.
“Shule yetu kiukweli bado inakabiliwa na changamoto kadhaa na ndio sababu tunawahikikishieni kwamba tutajitahidi kuhakikisha kwamba kila msaada unaolenga kupunguza changamoto hizi tunauenzi kwa nguvu zetu zote…asanteni sana!,’’ alipongeza.
Aliongeza kuwa ongezeko la vitabu shuleni hapo litakuwa kama chachu ya kutimia kwa malengo ya serikali katika kuhakikisha kwamba ubora wa elimu hapa nchini unakuwa kwa kuridhisha.
Aidha Mwl Mwakasyama alitoa wito kwa mashirika na taasisi nyingine kuiga mfano huo huku akiongeza kuwa kwa sasa serikali peke yake haiwezi kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya elimu hivyo nguvu ya wadau mbalimbali ni muhimu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad