TIMU
ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja la
kwanza imeshindwa kuonyesha makali yake mbele ya wadogo zao timu
ya AFC Arusha inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kutoka suluhu
ya bao 1-1 katika ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.
Mchezo
huo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, uliwashuhudia
maafande hao wa Oljoro wakianza kucheka na nyavu za AFC baada ya
kujipatitia bao lake kupitia kwa mchezaji Swalehe Idd alilofunga kwa
njia ya Penalti mnamo dakika ya 58, iliyosababishwa na mabeki wa timu
pinzani kunawa mpira katika eneo la hatari.
Vijana
wa AFC walionyesha juhudi zao kwa kulishambulia lango la Oljoro ambapo
walifanikiwa kusawazisha bao mnamo dakika ya 88 kupitia kwa mshambuliaji
wao Wandima Malechela baada ya kuachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja vyavuni.
Ufunguzi
huo ni utangulizi tu wa Mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 13
yaliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media yenye kauli mbiu "Uchaguzi wa
Amani 2015,
ndio taifa moja kwa maendeleo ya utalii nchini" na yatafikia kilele siku
ya kilele tarehe 19 mwezi huu katika viwanja vya Makumbusho Arusha.
Akifungua
mashindano hayo kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji la Arusha Idd Juma,
Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat Ntabindi
alieleza kuwa mashindano hayo ni humimu hasa kwa watoto hao wenye vipaji
kuonyesha uwezo wo huku wakikuza uelewa kwa vijana wadogo na kumuenzi
hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa
mbele katika kuhamasisha michezo hadi kugharamia kambi za timu ya Taifa
kitendo ambacho kwa sasa hakipo.
Naye mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya Bimo Media Bertha Ismail alisema maadhimisho hayo yataambatana na mashindano ya kila mwaka ya ki- elimu ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji picha juu ya masuala ya utalii kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha.
“ Lengo ni kuhamasisha uchaguzi wa mwaka huu kufanyika kwa amani vile vile kuhamasiha watu kuhudhuria hifadhi za utalii zilizoasisiwa na Mwl Nyerere na tunategemea Zaidi ya wanafunzi 700 watashiriki katika shindano hilo la isha.”ismail alifafanua.
Timu
za nyota academy,Future Stars,Kijenge Youth,Rolling Stone,Young Life na
palloti zitachuana na washindi watakabidiwa zawadi mbalimbali ikiwemo
vikombe na fedha.



No comments:
Post a Comment