jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

AIRTEL YANG’ARA KATIKA MAONYESHO YA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI

Share This
Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi Abbas Musa (
Kushoto) akimkabithi kikombe Afisa masoko na biashara wa Airtel ,
Emmanuel Raphael mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel
kuibuka mshindi wa pili  katika maonyesho ya Biashara ya Afrika
Mashariki ya mwaka huu.  Katika maonyesho hayo Airtel ilipata makombe
manne katika vipengele mbalimbali ikiwemo, Mtoa huduma bora , Mtoa
huduma bora katika sekta ya mawasiliano,  ubora katika mawasiliano ya
habari na tecknologia  pamoja na mshindi wa pili wa maonyesho kwa
mwaka huu. Akishuhudia (katikati) ni mwenyekiti wa Tanzania Chamber of
Commerce , Industrial and Agriculture Elibariki Mmari

Pic+2+Mwanza
Afisa masoko na biashara wa Airtel, Emmanuel Raphael katika picha na
makombe mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka
washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya
Afrika Mashariki ya mwaka huu

IMG_0357Wafanyakazi wa Airtel kwa pamoja wakiwa na makombe yao mara baada ya
kukabithiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi
Abbas Musa mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka
washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya
Afrika Mashariki ya mwaka huu


·         Yazawadiwa vikombe vinne vya ubora wa huduma na bidhaa.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imepokea
vikombe vinne katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kufatia
ubora wake katika kutoa huduma na bidhaa za kibunifu kwa wateja wake.

Maonyesho haya ya Biashara ya Afrika Mashariki ni maarufu kwa
kuonyesha aina mbalimbali za bidhaa ikiwemo bidhaa za matumizi ya
kawaida na ya viwanda, huduma, mashine na teknologia.  Na maonyesho
haya yametoa fulsa ya kukutanisha wadau pamoja na kubadilishana uzoefu
wa kibiashara na kuwawezesha ushirikiano wa biashara  katika nchini za
ukanda wa mashariki.

Akiongea wakati wa halfa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara, Uledi Abbas Musa alisema” Maonyesho haya yana lengo la
kuwapatia makampuni yaliyoko katika ukanda wa Afrika ya Mashariki
fulsa ya kujitangaza na kukuza biashara zao lakini pia kuwapatia
nafasi ya kuboresha mahusiano ya kudumu na wateja wao. Leo najisikia
furaha kuwazawadia kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  kwa kuonyesha
ubora wake katika huduma, bidhaa, tecknologia za kibunifu na kwa kuwa
washindi wapili katika maonyesho  ya mwaka huu”
Aliongeza kwa kusema” Airtel imedhihirisha dhamira yake ya kutoa
huduma za kibunifu na za uhakika za mawasiliano ya simu za mkononi na
kutokana na hilo tumeona ni muhimu kuwapongeza na kuwazawadia kwa
jitihada zao”

Kwa upande wake Afisa Masoko na bidhaa wa Airtel , Bwana Emmanuel
Raphael alisema” huu ni mwaka watano mfululizo sasa kwa Airtel
kushiriki katika maonyesho haya tukuwa na lengo la kufikia wateja wetu
, kutoa elimu ya huduma na bidhaa tunazotoa pamoja na kuboresha
mahusiano nao. Maonyesho haya pia yamekuwa ni fulsa muhimu kwetu
kuonyesha bidhaa na huduma zetu za kibunifu na za kisasa na pia ni
nafasi pekee ya kushikiana na makampuni mengine yanayoshiriki kila
mwaka”.

“Napenda kuwashukuru waandaaji wa maonyesho haya kwa kutambua na kuona mchango wetu na tunahaidi kuendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma bora na za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu.” 

Aliongeza Raphael Katika halfa hiyo, Airtel ilipokea makombe manne ya ubora katika vipengele vya  namba moja kwenye kutoa huduma, namba moja katika sekta ya mawasiliano, namba moja katika teknologia ya mawasiliano ya habari na namba mbili katika maonyesho ya mwaka huu. 

Nchi zilizo shiriki katika maonyesho ya mwaka huu ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda and Burundi
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad