JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAJI AMOS MAKALLA MJINI GEITA

Share This
NAIBU waziri wa maji Amos Makalla leo ametembelea mradi  unaotekelezwa kwa ushirikiano wa serikali na mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) wa uboreshaji huduma ya maji kwa mji wa Geita, Mradi huu unagharimu fedha sh 10 bilioni ambao kukamilika kwake kutaongeza huduma ya upatikanaji maji kutoka asilimia 13 iliopo sasa hadi  kufikia asilimia 57.

Kwa mujibu wa tathmini ya kazi iliyofanyika mradi huu unatarajiwa kukamilika  mwishoni mwa mwezi august mwaka huu na naibu waziri wa maji ameagiza wahakikishe wananchi wanapata maji wiki ya kwanza mwezi ya mwezi septemba na si vinginevyo.
NAIBU waziri wa maji,Amos Makalla akikagua kazi za uchimbaji mitaro, ulazaji wa mabomba na ukaguzi wa tanki leo katika mji wa Geita
 NAIBU waziri wa maji Amos Makalla akitembele maeneo mbalimbali yaliyo na mabomba ya maji.

Mkuu wa mkoa wa Geita Fatma Mwasa akimpokea naibu waziri maji Amos Makalla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad