Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akizungumza juu ya Upungufu wa vitamini na Baadhi ya Madini muhimu kama Vitamini A, folate, Madini chuma Zinki na madini joto ni chazo cha vifo kwa Watoto chini ya miaka Mitano na chanzo kikubwa cha maradhi mbalimbali kote Duniani, kulia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Alliance for Iproved Nutrition (GAIN) ,Marc van Amerngen katika mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Alliance for Iproved Nutrition (GAIN), Marc van Amerngen akizungumza na waaandishi wa habari hawapo pichani juu ya Kongamano la kimataifa litakalofanyika jiji Arusha Septemba 9-10 mwaka huu katika mkutano uliofanyika leo Jiji Dar es Salaam kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Michael John.
Mkurungenzi Msaidizi huduma za lishe Dr.Vincent Asey kuliani Dr. Generose Mulokozi akizungumza juu ya Matatizo ya lishe yanamgusa kila mmoja wetu kote Duniani katika mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandish wa habari walio hudhulia mkutano huo jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanue Massaka.
TAKWIMU zinaonyesha zaidi ya watoto milioni 3.1 wenye umri chini ya miaka mitano hufariki Dunia kila Mwaka huku wengine Milioni 161 kupata matatizo ya kudumaa mwili kutokana na kukosekana kwa virutubisho vya chakula.
Madhara hayo yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza virutubisho kwenye vyakula ikiwemo Unga,Mafuta ya kula pamoja na Chumvi.
Hayo yalisemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Michael Jonh wakati wa mkutano na waandishi wa habari ikiwa lengo ni kutoa tamko kuhusu Kongamano la kimataifa la Urutubishaji Chakula litakalo septemba 9 hadi 11 mwaka huu jijini Arusha.
Aidha amesema kuwa Chanzo cha Vifo hivyo ni upungufu wa vitamini pamoja na dbaadhi ya madini muhimu kama vile vitamin A,Folate,Madini Chuma,Zinki na Madini Joto hali inayosababisha maradhi mbalimbali katika maeneo mengi duniani.
Kwa upande wake Mkurugezi Msaidizi wa huduma za lishe kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Vicent Assey alisesema kuwa utafiti wa mwaka 2010 umebainisha asilimia 42 ya watoto ni walemavu kutokana na Lishe Duni.
Alisema kuwa nchi ambazo zimeathirika na tatizo la vifo kwa watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano kutokana na ukosefu wa virutubisho kwenye chakula ni zile ambazo zipo kusini mwa jangwa la sahara Barani Afrika.
Alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na Tanzania ambayo ipo nafasi ya tatu kulingana na takwimu za vifo kwa watoto ,huku DRC Kongo ikishika nafasi ya pili, na Ethiopia ikiwa ni ya kwanza kutokana na sababu kubwa ya kukumbwa na migogoro ya kivita katika nchi hizo.
Kutokana na changamoto hizo Serikali ya Tanzania kwa Kushirikiana na Shirika la masuala ya urutubishi wa chakula duniani la Global Alliance For Improved Nutrition (GAIN) inatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo la kwanza la kimataifa ambalo shabaha yake kubwa ni kuzungumzia masuala ya urutubishaji chakula.
No comments:
Post a Comment