JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


VIJANA WALIOTIMIZA MIAKA 18 WAASWA KUPIGA KURA ILI KUCHAGUA VIONGOZI WANAO WATAKA.

Share This
Na Avila Kakingo,Globu ya jamii.
VIJANA waliotimiza miaka 18 kwa mwaka huu waaswa kupiga kura ili kumchagua kiongozi wanaemtaka na watambue mchango wao katika jamii kwa kupiga kura  kwaajili ya maendeleo ya taifa letu.

Nae Mwenyekiti wa  asasi isiyo ya kiserikali Tanzania People  with Disabilities Organization (TAPWAO), Michael  Mwanzalima ameomba tume ya uchaguzi  kutoa vipaumbele kwa  walemavu wa viungo mbalimbali siku ya kupiga kura ili isiwe kikwazo kwao katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ili waweze kuwachagua viongozi wanao wafaa.

 Hayo yamesemwa na  vijana mbalimbali waliohudhuria katika mdahalo wa “ELEKEA UCHAGUZI 2015 NA VIJANA ”ulioandaliwa na  kampuni ya Tanzania Bora Initiative (TBI) ikiwa na nia ya kuadhimisha siku ya vijana dunia katika mdahalo uliofanyika katika hoteli ya New Afrika Dar es Salaam leo.

Pia katika mdahalo uliohusisha vijana mbalimbali hapa nchini ikiwa na wacheza muvi,waimba mziki wa kizazi kipya (Bongo freva) na vijana kutoka makampuni mbalimbali wakijadiliana kuhusiana na UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25 MWAKA HUU, vijana watashiriki vipi ili kuchagua kiongozi wanae mtaka.

Pia katika mdahalo huo uliambatana na  uzinduzi rasmi wa kampeni ya njia ya mtandao ya habari ujulikanao kama  UCHAGUZI 2015# KURA YETU.

 Mbunge wa viti maalumu (CCM) Maria Salungi akichangia maada kuhusiana na kijana anajitambuaje katika kuhamasika kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu ili waweze kumchagua kiongozi wanae mtaka, kwa kuwa baadhi ya vijana ni mara yao ya kwanza upiga kura.
Le Mutus akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Tanzania Bora Initiative uliofanyika katika hoteli ya New Afrika jijini Darr es salaam jana.
 Mwigizaji wa Bongo Muvi Rose Ndauka akichangia maada kuhusiana na waandishi wa habari vijana wanaweza kusaidia zaidi katika kufikisha ujumbe kwa vijana wengine ili waweze kwenda kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakao fanyika Oktoba 25 aliyazungumza hayo katika mdahalo uliofanyika katika hoteli ya New Afrika jijini Darr es salaam jana.
Mwenyekiti wa  asasi isiyo ya kiserikali hapa nchini ya Tanzania People  with Disabilities Organization (TAPWAO), Michael  Mwanzalima akizungumza katika mdahalo uliofanyika katika hoteli ya New Afrika jijini Darr es salaam jana, yeye akiwakilisha walemavu akiomba rai kwa  Tume ya uchaguzi kuwawekea mazingira rafiki katikauchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 waweze kupiga kura bila  kikwazo chochote.
 Baadhi ya vijana waliohudhulia katika mdaholo uliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam.
 wageni waalikwa wakiwa katika mdahalouliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam.
Manzilishi wa kampuni ya Ekihya na mwenyekiti wa mdaholo uliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam.akizungumza na vijana waliohudhulia mdahalo huo.


 Hamfrey Pole pole akizungumza katika mdahalo uliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam. akiwaasa vijana wajitokeze katika upigaji kura wa mwaka huu utakaofanyika Oktoba 25 ili kuwachagua viongozi bora na sio bora viongozi.
Bandi ya muziki ambayo jina lake halikuweza kupatikana ikitumuiza katika  mdaholo uliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad