JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


STAMICO KUANZISHA MTANDAO WA KUWASAIDIA WACHIMBAJI WADOGO

Share This
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico), Zena Kangoi akizungumza na waandishi wahabari juu mafanikio ya stamico yaliyofanywa katika katika Ofisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuuwa Stamigold, Mhandisi Dennis Sibugwao akizungumza na waandishi wahabari juu Stamico inavyosimamia mgodiwa STAMIGOLD, katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Stamico,jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Stamico, Rehema MwakajubeBeatrice akizungumza na waandishi wahabari juu ya mipango mikakati ya uwekezaji wa Stamico iliyofanyika Makao Makuu ya Stamico jijini  Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Deusdedith Magala, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchongaji ,Alex Rutagwelela.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico, Zena Kangoi akiwa na baadhi ya wakurugenzi wakati akieleza mafanikio ya shirika hilo kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika makao Makuu jijini Dar es Salaam.

 Na ChalilaKibuda,GlobuyaJamii 
 SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico) limesema linatarajia kuzindua mtandao utaosaidia kupata taarifa mbalimbali za kuweza kuchimba kisasa. 

Akizungumza na waandishiwa habari jijini Dar esSalaam, Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji, Zena Kongoi amesema kuwa kuanzishwa kwa mtandao kwawachimbaji wadogo kutawafanya kuweza kukua kiuchumi kuliko ilivyo sasa kwa uchimbaji duni. 

Amesema kuwa mtandao utasaidia jinsi ya kuweza kupata vifaa vya kuchimbia madini kutokana na taarifa zitazowekwa katika mtandao. 

“Lengo letu ni kuwa saidia watanzania wenzetu katika uchimbaji wamadini kuweza kwenda kisasa zaidi nasio uchimbaji duni ambao unarudisha maendeleo yao”amesema Zena. 

Amesema Stamico imeongeza mapato yake kutokana na uwekezaji wakupitia kampuni tanzu za utoaji wa huduma za kibiashara kutoka Sh.Milioni 281 kwa mwaka fedha 2014 /2015 hadi kufikia Sh.Bilioni 3.17 kwa fedha 2014 /2015. 

Zena amesema wanatarajia kuzalisha umeme wamakaa yamawe ya Kiwira ambapo watazalisha megawati 400 za umeme hali ambayo itapunguza tatizo la umeme kwashirika  licha yakuweka miradi yakusaidia wachimbaji wadogo lakini wameweza kuwekeza uchimbaji wamadini kwakushirikiana na makampuni mengine kutokana sharia ziliwekwa baada ya mabaoresho ya shirika hilo. 

Amesema baadhi yamiradi ya uzalishaji wa  madini imeanza kuzalisha na kuwezasha shirika kutoka hatua moja kwenda nyingine katika utoaji huduma pamoja ili kukuza uchumi wa nchi pamoja kuongeza ajira nchini kutokana na miradi ya uzalishaji wa dhahabu. 

Zena amesema kuwa shirika limeanzisha miradi kuendeleza wachimbaji wadogo kitaalamu na ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu (SMMRP) katika kuwaondoa katika uduni. 

Amesema katika mradi wa Stamigold umesafirisha na kuuza dhahabu katika nchi ya Switzerland kwa kiasi cha Wakia 12,923.35 na kuingizia shirika la Taifa la Madini (Stamico) na taifa kwa ujumla Dola za marekani Milioni 15.6. na kuaza kurejesha mrabaha wa asilimia 4.0 ya mauzo sawa na sh.1.3 milioni za serikali na Wizara ya Nishati na Madini na kulipa ushuru sh.milioni 40.

Aidha amesema shirika limeweza kuanzisha mradi wa ununuzi wa madini ghafi ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo wa maeneo ya vijiji vya Kabingo,Murongo ,Syndicate na Rugasha katika Wilaya Kyerw,mkoani Kagera na kuyauza madini hayo kwenye soko la nje ya nchi ikiwa na lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo . 

Zena amesema wako katika mazungumzo na Benkiya TIB kuweza kukopa Dola za Marekani700,00090000 kwaajili ya kununua mitambo hali ambayo shirika litaweza kukua katika kuendesha miradi mbalimbali. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad