JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MGOGORO WA MAENEO YA KILIMO YA VIJIJI VYA ZANZABAR WAISHA

Share This
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Hati  ya umiliki wa eneo la Kilimo kwa Bwana Yuweni Kibwana Nzukwi  Mmoja miongoni mwa wakulima wa Vijiji vya Dole, Ndunduke na Kijichi  baada ya upatikanaji wa ufumbuzi wa mgogoro wa maeneo hayo.
  Mkulima Ana Nyaka Buluju wa Dole    akikabidhiwa hati ya umiliki wa eneo la kilimo kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  hapo Skuli ya Wazazi Dole Wilaya ya Magharibi  “A “.
Baadhi ya wakulima wa  Vijiji vya Dole, Ndunduke na Kijichi wakifuatilia zoezi la kukabidhiwa hati zao za umiliki wa maeneo ya kilimo kwenye Vijiji vyao lililafanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.



HATMA ya Mgogoro wa maeneo ya Kilimo unaowahusisha Wakulima wa Vijiji vya Dole, Ndunduke, Kijichi na Nguruweni dhidi ya baadhi ya watu wanaovamia  maeneo hayo hivi sasa umeshafikia ukingoni baada ya kurindima kwa takriban miaka 12.

Mgogoro huo ulizuka kufuatia baadhi ya watu wenye uwezo wa kifedha pamoja na marafiki na familia za maafisa wa taasisi za Kilimo kuvamia maeneo hayo wakati wakielewa kwamba wakulima wa asili wa maeneo hayo walikuwa wakiyatumia kuendeleza shughuli zao za kilimo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitekeleza Ahadi ya Serikali aliyoitoa Tarehe 14 Disemba mwaka 2012 ya kuwamilikisha Wakulima hao alikabidhi Hati za umiliki huo kwa Wakulima 145 wa Dole, Ndunduke na Kijichi hapo katika maeneo ya skuli ya Wazazi Dole.

Wakulima hao 145 ni miongoni mwa wote Mia 222 wa Vijiji hivyo ambao walipata hati hizo baada ya kuyatumia maeneo hayo ya Serikali  yaliyokuwa chini ya Wizara ya Kilimo wanayolimwa kwa kipindi kirefu cha maisha yao.

Akizungumza na Wakulima na Wananchi wa Vijiji hivyo vya Dole, Ndunduke na Kijichi Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamuwa kufanya hivyo ili kuwapa fursa ya umiliki wakulima hao waendeleze shughuli zao za Kilimo kwa utulivu zaidi akiwatanabahisha kwamba maeneo waliyopewa ni kwa ajili ya kilimo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashukuru na kuwapongeza Wananchi na Wakulima wa Dole, Ndunduke, Nguruweni na Kijichi kwa ustahamilivu wao mkubwa waliouonyesha ambao umeipa faraja Serikali na kufikia hatua njema na ya mafanikio.

Akitoa Taarifa fupi katika mkutano  huo wa makabidhiano ya hati ya umiliki wa maeneo ya kilimo, Mwenyekkiti wa Wakulima wa Dole, na Ndunduke Dr. Daudi Silas Mukaka alisema Serikali Kuu imeonyesha nia thabiti ya kuwajali Wananchi wake.

Dr. Mukaka alisema Wananchi pamoja na Wakulima wa Dole na Ndunduke wamefarajika sana kutokana na kazi kubwa iliyochukuliwa na Serikali  Kuu chini ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa kushirikiana na baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Kilimo na Ardhi katika kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala hilo la mgogoro wa maeneo ya kilimo.

Mapema Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi  alisema licha ya Wananchi wa Vijiji hivyo kuonyesha ishara ya hasira lakini alifarajika kuona kwamba busara ilitawala katika kulishughulikia tatizo hilo.

Mheshimiwa Abdullah alisema Wananchi hao wanapaswa kuendelea kumpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kutokana na Uongozi wake wa busara wa kuweka ahadi na akawa makini kuitekeleza.

Migogoro ya ardhi katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Zanzibar hivi sasa inaonekana kuchukuwa sura mpya ya kuanza kuchukuliwa hatua za ufumbuzi kutokana na uamuzi wake wa kusajili ardhi yote ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad