Na Mwandishi wetu-MAELEZO-Dar es salaam
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi wa michezo ya Wizara, Idara zinazojitegemea ,Wakala wa
Serikali na Ofisi za wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) itakayoanza Jumamosi
ijayo(15.8.2015) mjini Morogoro.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es
salaam na Kaimu Katibu Mkuu SHIMIWI Moshi Makuka, mashindano ya mwaka
huu yatafanyika kwa wiki mbili.
Amesema
kuwa siku ya ufunguzi kutakuwa na michezo ya mpira wa miguu kati ya
Elimu na Hazina kwa wanaume , mpira wa pete utazikutanisha timu ya Afya
na Mambo ya Ndani.
Makuka
ameongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwepo mchezo wa kuvuta kamba kati ya
Wakala wa Jiolojia Tanzania na Mambo ya Nje kwa wanaume na kamba kwa
wananwake kati ya Ikulu na Bunge.
Amezitaja
timu zilizothibitisha kushiriki kuwa ni Ikulu, Utumishi, Waziri Mkuu,
Afya, Ardhi, Elimu, Hazina, Kilimo,TAMISEMI, Mifugo, Maji, Afika
mashariki, Maliasili, Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Ulinzi, Nishati,
Maendeleo ya Jamii, Viwanda, Uchukuzi, Ujenzi na Tume ya Mipango.
Timu
nyingine ni Mahakama, Tume ya Utumishi wa Umma, Bunge, Tume ya
Kurekebisha Sheria, Tume ya Mahakama, Ukaguzi, tume ya ushirika , Wakala
wa Jiolojia Tanzania, Wakala wa Ukaguzi wa Madini, Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula, Mkoa wa Lindi, Katavi, Mwanza, Kagera, Rukwa, Dar es
salaam, Mtwara, Iringa, Geita, Kigoma, Manyara , Arusha, Mara, na Tanga
No comments:
Post a Comment