
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatarajia kuzindua mashindano ya michezo mbalimbali kwa lengo la kuwashirikisha wananchi wa rika zote na itikadi mbalimbali
yatakayojulikana“KAMISHNA KOVA CUP”.
Madhumini ya mashindano haya ni ni Kuwaunganisha wananchi wenye itikadi mbalimbali ili kupitia mashindano haya watakaoshiriki watajifunza masuala ya usalama, uzalendo na kuzingatia utaifa kwa madhumuni ya kuwashirikisha kikamilifu katika ulinzi wa nchi na kudumisha amani na utulivu katika jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine.
Lengo lingine ni Kuishirikisha jamii kuondokana na dhana ya kutenda uhalifu wa aina mbalimbali kama vile ujambazi, matumizi ya aina mbalimbali ya madawa ya kulevya, wizi katika mitandao,uzururaji, na kukaa katika vijiwe bila kazi.
Pia Kupitia michezo mbalimbali, jamii itafaidika kupata elimu juu ya umuhimu wa jukumu la msingi la kushiriki katika ulinzi na usalama wa nchi hii, itakuwa ni fursa nzuri kujua madhara ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Katika michezo watajifunza kujenga au kuimarisha mahusiano mema baina ya Jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla kupitia dhana ya Polisi Jamii itatekelezwa kwa vitendo.


No comments:
Post a Comment