Meneja
Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo (kushoto),
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu kuendelea kufanyika kwa Tamasha la Muziki Bar kwa Bar
baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza. Kulia ni
Mtangazaji, Dina Marios.
Mtangazaji, Dina Marios akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu kuendelea kufanyika kwa Tamasha la Muziki Bar kwa Bar
baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza. Kushoto ni Meneja
Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja
Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo katika mkutano uliofanyika makao makuu ya EFM-Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
BAADA ya kumalizika kwa Tamasha la musiku mnene Bar kwa bar awamu ya
kwanza, na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena, Uongozi Efm umekubali
ombi hilo na sasa Tamasha hilo linarudi tena kwa kishindo likiwa limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia
watu wengi zaidi.
Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na
mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu wake
na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa utapelekwa pia
katika mkoa wa Pwani.
Maeneo
ambayo wanatakiwa kukaa tayari kwa
Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa na Madjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha,
Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe,
Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo
za mashabiki wetu.
Muziki
Mnene bar kwa bar mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 5/09/2015 . Lakini
katika kuelekea huko efm imeanza na Muziki mnene bango katika sehemu yako ya
biashara ambako bwana E anapita na ukiwa umeweka bango la EFM na unasikiliza
matangazo yetu basi utapata kifurushi chenye zawadi kibao.
Na
kama ilivyokawaida yetu, mwishoni tutakuwa na Tamasha kubwa la hitimisho ambalo
litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa
vionjo vingi sana.
“Ninawaomba
wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana tutawafikia na kuwamiminia Burudani
ambayo pia itarushwa live kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM.
Njoo tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu Muziki
unaongea”.
LAKINI jambo la pili ambalo ndugu zangu wanahabari tungependa
kuwajulisha ni kwamba katika kuhakikisha tunaendelea kukupa kilicho bora zaidi
kupitia vipindi vyetu mbalimbali,sanjari na kuwa na watangazaji wenye ushawishi
na uwezo mkubwa. leo hii tunamtambulisha kwenu mtangazaji Dina Marios ambaye
wengi uwezo wake mnaujua na sasa ameungana na wenzake wenye uwezo mkubwa katika familia ya Efm.
Mwisho
niwashukuru sana kwa mwitikio wetu na kwakuwa tumeendelea kushirikiana mara
nyingi hivyo naomba tuendelee kushirikiana hivi hivi. Asanteni sana kwakunisikiliza.
No comments:
Post a Comment