Kaimu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Jasper Mero akizungumza mkutano wa kupanga mikakati ya Fedha katika ofisi ya mdhibiti wa fedha za serikali CAG, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa wadau wa kuandaa mikakati ya Ofisi ya CAG wakimsikiliza Kaimu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Jasper Mero mkutano wa kupanga mikakati ya Fedha katika ofisi ya mdhibiti wa fedha za serikali CAG, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Jasper Mero akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mkutano wa wadau wa kuandaa mikakati ya Ofisi ya CAG leo jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MALENGO ya ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) inategemea na mchango wa wadau katika kupanga mikakati ya kuwezesha ofisi hiyo iweze kusimamia katika kuhakikisha
fedha za umma zinaleta maendeleo ya kiuchumi.
Hayo ameyasema leo,Kaimu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG),Jasper Mero wakati akifungua mkutano wa wadau wa
kuandaa mikakati ya Ofisi ya CAG ya 2016 -2021 katika kuweza ofisi hiyo
iweze kusimamia mikakati hiyo.
Mero amesema wananchi wanahitaji usimamizi wa fedha
zao ili waweze kupata maendeleo ya kiuchumi na hiyo inatokana na ofisi ya CAG
kuweka mikakati ya kuhakikisha fedha ya umma haipotei.
Amesema wadau wametakiwa kutoa maoni kwa uhuru
katika ofisi hiyo iweze kupata mikakati ya kuweza kusimamia katika udhibiti wa
fedha ya Umma.
Mero amesema mikakati ya 2011hadi 2016
imetekekelezwa kwa asilimia 100 hiyo ikiwa imetokana na mahusiano ya ofisi ya
CAG pamoja na wadau ambao walitoa maoni chanya katika ofisi hiyo.
Aidha amesema wadau wana nafasi ya kuweka mawazo yao
katika kutengeneza mikakati ya miaka mitano ambayo itafanya mabadiliko ofisi ya CAG katika kudhibiti fedha ya umma.
Amesema katika ofisi ya CAG imepata mafanikio ikiwa
ni pamoja kutoa ripoti za mara kwa mara pamoja na kutoa ushauri wa
kiutekelezaji kutokana na ukaguzi walioufanya katika mashirika ya Umma ,pamoja
na Taasisi za Serikali.


No comments:
Post a Comment