Meneja Uhusiano wa DSTV Barbara kambogi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya moto wa la Liga utawashwa ndani ya Super Sport 3(SS3)katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya New Afrika leo jijini Dar es Salaam.Kulia Meneja Uhusiano wa DSTV Barbara kambogi na Afisa masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samaly.
Meneja uendeshaji wa DST,Ronald Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari juu chanmeli mpya ya michezo katika kingamuzi cha Multchoice,katika hafla iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa DSTV Barbara kambogi.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia taarifa katika uzinduzi wa channel katika hafla iliyofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam. Picha Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WATAZAMAJI wa Supersport watakuwa nafasi pekee kushuhudia mechi kwenye ubora wa HD pamoja na michuano ya Ligi kuu ya Uingereza (EPL),Ligi ya Hispania (La liga),Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (UEFA),Ligi ndogo za Ulaya (Europa),Mechi za FIFA za kirafiki za kimataifa na Klabu bingwa ya Dunia ,Kombe la Ujerumani ,Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey) na Kombe la FA.
Akizungumza na waandsihi wa habari leo Meneja Uhusiano wa Multchoice,Babra Kambogi amesema wateja wa DStv wateja wa DStv wakae tayari kwenye msimu wa mabingwa ulimwenguni ambapo Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara nyingine huku Manchester United wakihitaji kurudisha kiti chao cha ubingwa Uingereza.
Amesema katika msimu huu zaidi ya mechi 900 za kimataifa zitaonyeshwa kimataifa na wateja wa DSTV Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi 450 live huku wateja wa Dstv premium watazawadiwa mechi zote.
Babra amesema wateja wa Dstv vituko vya michuano yote ya ligi kuu Uingereza vitaletwa kupitia Suparspot (SS5) kinochopaatikana katika kifurushi cha Premium na SS5 itakuwa ndio nyumba ya soka la Afrika kwa Ligi kuu ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment