Mwenyekiti wa QAML Mwenyekiti,Yusuf Manji wa
kwanza kulia, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
ya magari ya General Motors East Africa (GMEA) Limited, Mario Spangenberg wakikata utepe kuashiria
uzinduzi wa jengo la Isuzu uzinduzi huo uliofanyika jiji Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya General motors (GMEA) Bi.
Rita Kavashe akisaini makubaliano ya
kibiashara na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Quality automotive Vinay
Upadhyay.
Mkurugenzi mtendaji wa GMEA Rita Kavashe alisema Kampuni
ya General motors kuingia katika soko la Tanzania ilikuwa ni sehemu ya mkakati
wa muda mrefu katika kampuni hiyo ili kuimarisha uwepo wake Afrika
Mashariki. Kulia ni Rais na Mkurungenzi Mtendaji wa (GM) Africa Mario Spangenberg.
Wakifurahia jambo mara baada ya kukamilisha makubaliano.
PICHA NA
EMMANUEL MASSAKA
General Motors Imerudi tena katika soko
la Tanzania ikiwa imeongeza ufanisi zaidi,
Wenya magari Tanzania leo wana sababu ya kutabasamu maana Kampuni
ya magari ya General Motors East Africa (GMEA) Limited leo wamesaini
makubaliano ya kibiashara na Quality automotive mechanization limited (QAML)
ambayo itashuhudia kampuni ya magari ikiingia
kwenye soko la Tanzania.
Kupitia uuzaji mpya, wateja wa General Motors wataweza kununua
bidhaa mpya aina ya Isuzu na Chevrolet kutoka katika sehemu za mauzo huku
wakipata huduma za kimataifa kutoka katika eneo maalumu la magari hayo.
Akizungumza hi leo wakati wa sherehe ya kutia saini
makubaliano ya biashara, Mwenyekiti Mheshimiwa wa QAML Mwenyekiti Mheshimiwa
Yusuf Manji aliahidi wateja ngazi bora ya urahisi na faraja.
“Tumeweka uwekezaji
mkubwa/muhimu kuhakikisha mafanikio ya kituo hiki na kuwezesha kupenya kwa
haraka kwa bidhaa za Isuzu na Chevrolet katika soko hili lenye ushindani mkubwa”.
Alisema
Eneo la mauzo ya magari limetengenezwa ili kutoa/ kuwapatia
wateja uzoefu na uimara kwa ujumla na bidhaa za General Motors, pamoja na kutoa
huduma za mauzo na vifaa vya magari.
Mkurugenzi mtendaji wa GMEA Bi. Rita Kavashe alisema Kampuni
ya General motors kuingia katika soko la Tanzania ilikuwa ni sehemu ya mkakati
wa muda mrefu katika kampuni hiyo ili kuimarisha uwepo wake katika Afrika
Mashariki.
“Tanzania imejitokeza katika soko na kama General Motors tulitaka
kuwa sehemu ya ukuaji huu. Sehemu hii ya mauzo itakuwa ni hatua ya kuingia kwa
bidhaa zetu zenye ubora na zimetumia utaalamu mkubwa katika utengenezwaji
wake ambapo tunatanua wigo wetu katika
ukanda huu. Kupitia uuzaji huu, wateja wetu watanunua aina mpya za Chevrolet na
Isuzu huku wakipata huduma bora”.
Alisema Bi. Kavashe alisema kuingia ndani ya soko la Tanzania
imetokana na kukua kwa kasi kwa biashara ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki
hasa katika kuendeleza ushirikiano wa masoko ya umoja. Soko la jumuia ya Afrika
Mashariki lina takribani watu milioni 140 .
“Tanzania ni soko linalokua kwa kiwango kikubwa na imekua ni
soko muhimu tunalolitazamia tunapotafuta kujikita katika soko lenye watu wengi
na idadi inayokua kila kukicha. Ukuaji wa viwanda na
kuongezeka kwa kipato ili kutengeneza ongezeko la watu wa
tabaka la kati katika nchi hii ina maana kuwa kuna soko changa la bidhaa zetu,
“aliongezea Kavashe.
No comments:
Post a Comment