CHAMA
cha Wananchi (CUF) wilaya ya Kondoa kimewataka wananchi wa Wilaya hiyo
kufanya mageuzi ya uongozi kwa kuchagua wagombea wa vyama vya upinzani
ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kuleta maendeleo.
Hayo
yalisemwa na Katibu wa CUF wilaya ya Kondoa, Jafari Ganga alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CUF Dar es Salaam
jana.
Alisema
kwa miaka mingi wilaya ya Kondoa imekuwa ikitawaliwa na Chama cha
Mapinduzi (CCM)katikangazi mbalimbaliza viongozi wa juu wakiwemo wabunge
ambao kila mara wanatoka chama tawala.
Ganga
alisema kuendelea kudidimia kwa uchumi wa wilaya hiyo kutokana na
uongozi ambao hausimamii ipasavyo maendeleo ya uchumi, hivyo baada ya
kuona hivyo CUF ilianza kuonesha njia kwa kusimamia mambo mbalimbali ya
kiuchumi yaliyofanya chama kukubalika.
Alisema
mpaka sasa katika kata zote 29 za wilaya ya Kondoa zimesimika matawi ya
chama hicho na wanatarajia kutwaa viti vya madiwani na Ubunge katika
majimbo mawili ya Kondoa Vijijini na Kondoa.
"CUF
imeamka inayo matawi 160 katika katika Kata zote 29 za wilaya ya
Kondoa, tumejiandaa kutwaa viti vya madiwani na wabunge" alisema Bw.
Ganga.
Alizitaja
Kata hizo kuwa ni Kondoa mjini, Chemchem, Kilimani, Kingale, Kolo,
Bolisa, Serya, Suruke, Hondomairo, Changaa, Thawi, Sowera,
Kikilo,Salanka, Bereko, Kisese,Kikore, Itololo,Masange, Mnenia, Itaswi,
Bumbuta, Pahi, Kinyasi,Keikei, Busi, Haubi, Kwa Delo, na Kalamba.
Wilaya
ya Kondoa umegawanywa na kuwa majimbo mawili ya Kondoa na Kondoa
Vijijini pia kuna Jimbo la Chemba ambalo Mbunge wake aliyemaliza muda
wake ni Juma Nkamia.
No comments:
Post a Comment