Benki M yaadhimisha miaka 8 toka ilipoanzishwa,
pichani ni naibu mkurugenzi mkuu wa Benki M Bi. Jaqueline Woiso katika mkutano
na waandishi wa habari wikiendi hii katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Regency,
kuelezea mafanikio waliyopata katika kipindi hicho cha miaka 8 , kulia ni
mkurugenzi wa mawasiliano wa benki hiyo Bw. Allan Msalilwa.
BANK M Tanzania plc leo inatimiza miaka 8
toka ilipoanzishwa July 27, 2007. Akiongea na waandishi wa habari, Naibu
mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso alisema wanaadhimisha miaka
minane yenye mafanikio makubwa, “mwaka 2007 tulifunga mwaka tukiwa na
rasilimali zenye thamani ya TZS 32 billioni tu, na sasa tumefikia kiasi cha TZS
800 billioni. Tumekuwa tukifanya vizuri katika masoko kwa muda mrefu na
tulifanikiwa kuanza kupata faida ndani ya miaka miwili (2) tu toka kuanzishwa
kwa benki yetu. Kwa mwaka huu hadi kufikia June 2015 tumepata faida ya TZS 11.5
Billioni”.
Alisema kuwa Benki hiyo ilianza na kiasi kidogo sana cha TZS 16
billioni hadi kufikia TZS 630 billioni, huku mtaji ukiwa pia umeongezeka kutoka
TZS 6.5billioni hadi kufikia TZS 84 billioni kwa sasa huku idadi ya wafanyakazi
pia imeongezeka kutoka 40 hadi 236, kwa uwiano wa asilimia 50% kati ya wanaume
na wanawake.
Kwa upande wa huduma kwa wateja, Bi woiso
alisema kuwa Benki M imekuwa ni benki ya kwanza kutoa huduma masaa 12 kila siku
kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku, siku 7 za wiki yaani Jumapili
hadi Jumapili. “Pia tunatoa Garantii endapo tutazidisha muda tuliokubaliana
kufanikisha miamala ya wateja, huduma hii inajulikana kama SSG (Service
Standard Guarantee)” aliongeza.
Benki hiyo pia
imekuwa ikishiriki kwa kiasi kikubwa katika kusaidia jamii ikiwa ni moja ya
sera kubwa za benki hiyo ambayo huiita Money@heart, alisema Woiso.
“tunashirikiana na taasisi mbalimbali katika kufanikisha miradi mingi kwenye
jamii katika sekta ya Afya, Elimu, Maji Utunzaji wa mazingirana pia kuwainua
wajasiriamali na wasanii wa michoro ya asili nchini”.
Pia alisema kuwa wamefanikiwa kupata tuzo mbalimbali za
kimataifa ikiwemo tuzo ya benki bora ya biashara kwa mwaka 2015 iliyotolewa
katika soko la hisa la London, Benki bora katika sekta ya biashara za makampuni
Afrika Mashariki na Benki bora inayoshiriki katika maendeleo ya jamii Afrika
Mashariki zilitolewa na Banker Africa.
“Hatimaye
tumefanikiwa kuwa chaguo bora katika benki zinazotoa huduma kwa makampuni
nchini (Preffered Bank)”, alimalizia Bi Woiso.
No comments:
Post a Comment