Suala la matunzo ya watoto/mtoto lim ekuwa ni suala ambalo wasomaji
wengi wamekuwa wakiniuliza sana. Wengi wao wanaouliza ni wale ambao
wamezaa nje ya ndoa na hivyo kuna utata wa matunzo ya watoto na wale
ambao wamekuwa wana ndoa lakini sasa tayari wametengana aidha kwa
talaka au bila talaka. Niseme tu kwa ufupi kuwa suala la matunzo ya watoto
linajumuisha mambo mengi nami nitaeleza baadhi tu.
1.HUWEZI KUMLAZIMISHA MTOA MATUNZO KUTOA AMBACHO HANA.
Kumekuwepo na tabia ya wazazi hasa upande wa wazazi wa kike kuwalazimisha wanaume ambao wamezaa nao na kutengana nao kutoa matunzo ya watoto kwa kiwango cha juu kabisa ambacho pengine kinazidi hata kipato cha mtoaji. Hili si sawa. Ni kweli sheria inamlazimisha mwanaume kutoa matunzo ya mtoto lakini haimlazimishi kutoa kuliko anachopata. Sheria haiseme kwakuwa mwanamke anaishi na mtoto wa mtu basi mwanaume ndio sasa afanywe kitega uchumi. Inafikia hatua mwanamke hafanyi kazi yoyote isipokuwa anategemea ile pesa ya matunzo ya mtoto ndio iwe kila kitu katika maisha yake.
Hii ndio sababu hata akipewa kiasi kinachotosha haoni kama kinatosha kwakuwa kinakuwa na njia nyingi kama saluni, nguo za kuvaa, pesa ya upatu, michango ya harusi na kitchen party na kila kitu kinachohusu maisha yake binafsi. Ieleweke wazi kuwa kwa mujibu wa sheria pesa ya matunzo ya mtoto haihusiki na haya. Pesa ya matunzo ya mtoto ni pesa ya matunzo ya mtoto kama neno lenyewe lilivyo na linavyojieleza si vinginevyo.
2.INARUHUSIWA KUKATAA IKIWA UNALAZIMISHWA KUTOA MATUNZO YANAYOZIDI UWEZO WAKO.
Ikiwa mwanaume analazimishwa kutoa kuliko kipato chake basi anaruhusiwa kukataa hata kama amri hiyo imetolewa na mahakama. Wengine huandikishana polisi lakini bado haibadili maana kwakuwa mtu anatakiwa kutoa kulingana na uwezo wake au kipato chake. Wapo wazazi hasa wa kike ambao huwalazimisha wanaume kutoa matunzo ya kuwasomesha watoto international schools wakati kipato cha mwanume ni shule ya kata. Sheria inachokataza ni kukataa kabisa kutoa matunzo ya mtoto lakini haimlazimishi mtu kutoa kilichomzidi. Au wengine hulazimisha kuwekewa mpaka wafanykazi wa ndani( house girl) wakati kipato cha mwanaume hakiruhusu jambo hilo.
Huu nao ni unayanyasaji kwa upande wa wanaume na haukubaliwi na sheria. La msingi ni kuwa iwapo utalazimishwa kutoa kuliko uwezo wako we kataa. Na kama uamuzi huo umetolewa na mahakama basi kataa kwa kukata rufaa kupinga kabisa jambo hilo. Sheria inaposema matunzo ya watoto haisemi kuwa watu watoe kuliko uwezo wao hapana. Sheria ni haki na haki huzingatia ukweli na hali halisi ya jambo.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

No comments:
Post a Comment