JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MAKALA YA SHERIA: NAMNA YA KUMDAI FIDIA ALIYEVUNJA MKATABA AU KUKIUKA MAKUBALIANO YENU

Share This

Kawaida unapokuwa umeingia katika mkataba au makubaliano katika jambo lolote lile kunakuwa na masharti ambayo unapaswa kuyatimiza au kutimiziwa. Na hapa nazungumzia mikataba yote uwe wa kuuza mbuzi au ule wa kujenga ghorofa mia, yote ni mikataba. Masharti hayo huwa ndio makubaliano yenyewe au twaweza kusema kuwa ndio mkataba wenyewe. Kila upande unawajibika  juu ya utekelezaji wa masharti hayo. Yeyote anayefikia hatua ya kukiuka masharti hayo au hata kukiuka sharti moja tu, hana namna ila kukubaliana na  hatua na utaratibu wa kisheria kuhusu  uvunjwaji au ukiukwaji wa mikataba.

1.KUKIUKA MKATABA AU MAKUBALIANO.

Uvunjaji wa mkataba unaweza kutokea katika njia nyingi. Moja ni ile ya kawaida ambapo mtu huamua kujitoa kwa kusema,kutamka au kuandika kuwa sasa sitafanya hili na lile hata kama lipo katika makubaliano yetu.  Pili njia nyingine  ya kuvunja mkataba ni pale ambapo mtu hasemi kwa kutamka kwamba sasa sitafanya hili wala lile isipokuwa hatimiza wala hatekelezi kile mlichokubaliana. Ifahamike kuwa mtu anapoingia mkataba na mtu mwingine  au kampuni na kampuni  au kampuni na mtu sheria inalazimisha kutekeleza kwa usahihi yale yote yaliyokubaliwa  katika mkataba huo. Utekelezaji wa baadhi ya masharti na kuacha mengine au kutotekeleza yote kabisa ni uvunjaji au ni kujitoa katilka mkataba kwa mujibu wa sheria. Aidha nasisitiza kuwa ili mtu ajitoe katika mkataba sio lazima aseme kuwa nimejitoa katika mkataba. Kitendo cha kutofuata makubaliano  kama yalivyokubaliwa  ni kujitoa katika mkataba moja kwa moja.

2.KUMDAI FIDIA ALIYEKIUKA MKATABA AU MAKUBALIANO.

Si vyema mtu akafanya makubaliano na mtu mwingine halafu akapotea bila kutekeleza kile kilichokubaliwa. Ni sababu hii inayonifanya kuwaambia watu kuwadai fidia wale wanaokiuka masharti. Kudai kulipwa fidia baada ya kuvunjwa mkataba ni takwa la kisheria na hivyo si ukorofi kama ambavyo mtu anaweza kufikiri.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad