JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAZIRI SILAA AMPA RUNGU LA ARDHI KAMISHNA WA ARDHI PWANI

Share This

 








Na Khadija Kalili, Michuzi TV

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleleo ya makazi Jerry Silaaa amesema kuwa siku tatu za Kliniki ya Ardhi iliyoendeshwa ndani ya Halmashauri ya Chalinze Mlandizi na Bagamoyo na Kibaha Vijijini amebaini kuna migogoro sugu ndani ya Halmashauri hizo.

Waziri Silaa amesema hayo leo Julai 4 alipokua katika Kliniki ya Ardhi inayoendelea Halmashauri ya Bagamoyo ambapo amesema kuwa Kibaha Mjini na Vijijini huku akiyataja mashamba ya Mohammed Enterprises yaliyopo katika vijiji vya Soga , Kipangege yaliyopo Kihaha Vijijini kuwa yanahitaji kuchunguzwa kwa utaalamu zaidi hivyo ameacha maagizo kwa wataalamu wake ambao watayafanyia uchunguzi kwani vijiji hivyo vinahistoria yake wakati vilipoanzishwa katika oparesheni anzisha vijiji kati ya 1950 na 1972

Maeneo mengine yenye migogoro ya muda mrefu ni pamoja na Chamakweza iliyopo ndani ya Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo ambapo wakulima na wafugaji kila mmoja akidai kuwa ndiye mmiliki halali wa eneo hilo.

"Kama jinsi mtaona katika Kliniki ya Mkoa wa Pwani sijafukuza ama kumsimamisha mtendaji wangu yeyote hii ni kwa sababu hawajatajwa kuingiza miguu na wananchi kuhusika katika kashfa yoyote ya uuzaji ardhi.

Waziri Silaa ametoa maelekezo kwa Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Pwani kufuatilia kiutaalamu na kwa kina malalamiko yote yaliyotolewa na wananchi huku ameahidi kuwa atarudi tena Mkoani hapa ambapo ndipo atakuja kutoa maamuzi.

Akifafanua kuhusu maeneo yaliyovunjwa mwezi Juni katika eneo la Mitamba lililopo Kata ya Pangani Wilayani Kibaha Mjini amesema kuwa maelezo ya eneo la Mitamba amelichukua jana Julai 3 ambapo tayari amempa maelekezo Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Pwani pia

wataalamu wake watafuatilia kwa undani zaidi huku akisisitiza kuwa baada ya uvunjaji Wizara imepokea maelekezo kutoka kwa Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutatua migogoro yote ya ardhi kwa amani na weledi wa hali ya juu ilikukwepa kuleta taharuki kwa jamii ndiyo sababu iliyopelekea kusitisha uvunjaji wa nyumba katika eneo la Mapinga.

Aidha Waziri Slaa amewapa pole watu wote ambao walikua na shauku ya kuona akitoa maamuzi na kuwataka wawe na mioyo ya subira.

Wakati huohuo Waziri Silaa amempongeza Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua migogoro ya ardhi.

Akizungumza kuhusu tuhuma za Viongozi wa Halmashauri hasa katika Idara ya Ardhi Kibaha ambao wamekuwa wakitajwa kuhusiana na shutuma mbalimbali za kutumia madaraka yao kinyume na maadili ya kazi zao , amesema apelekewe majina yao watachunguzwa na pindi watakapo bainika watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria.

Ametoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge kutokana na jitihada zake za kutatua migogoro ya ardhi ndani ya Mkoa wa Pwani wakati huohuo amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash kwa kukutana na wananchi kuwasiliza na kuyamaliza kwa suluhu yenye tija matatizo ya ardhi ndani ya Wilaya yake ambapo ameweza kuwakutanisha mlalamikaji na mlalamikiwa na kutatua migogoro mingi kwa njia ya suluhu ikiwamo kukubaliana kupeana fidia kwa njia mbadala.

Naye Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mharami Mkenge aliyekuwa katika eneo la Kliniki hiyo amepongeza sana jitihada zinazofanywa na Waziri Silaa amesema kwa upande wa Wilaya ya Bagamoyo wanatarajia baada ya kupata ufumbuzi wa migogoro ndani ya Jimbo hiyo Halmashauri itakaa na kuipanga vyema Mji huo wenye vivutio lukuki vya asili.

Aidha Waziri Silaa ameunda Mikoa Mikoa miwili lengo kumaliza migogoro ya ardhi Mkoa wa Pwani.

Mhe. Silaa amesema Wizara yake imefikia maamuzi ya kuanzisha Mikoa miwili ya Ardhi katika Mkoa wa Pwani ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan katika falsafa yake ya maridhiano, kujenga upya nchi, uvumilivu na mageuzi yaaani 4R

Waziri Silaa amesema hayo katika Kliniki ya Ardhi Bagamoyo kwa ajili ya kusikiliza na mitatu kero za migogoro ya ardhi kwa wananchi iliyofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Majengo.


Aidha, Waziri Silaa amesema kuwa ofisi za Ardhi zinapaswa kutoa huduma kwa uwazi ili wananchi waweze kusikilizwa pasipo kifucho.

Mikoa mipya iliyoanzishwa ni Pwani Kaskazini itakayohusisha Wiilaya ya Kibaha na Halmashauri ya Chalinze huku Kanda ya Kusini ni Mkuranga,Kibiti,Kisarawe na Mafia .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad