JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Mapunda ataka Wadau kuunga mkono Mbio za TIA

Share This

 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda wa (tatu kutoa kushoto) akishangiliwa kwa makofi baada ya kukata utepe kwa ajili Uzinduzi wa maandalizi ya Mbio za TIA

*Fedha zitazopatikana zitatunisha Mfuko WA kusaidia wanafunzi wenye uhitaji na wakiwemo wenye Ulemavu.

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV
MKUU wa Wilaya Temeke, Sixtus Mapunda amesema kuwa Taasisi ya Uhasibu (TIA) imefanya bora katika kutafuta fedha kwa wanafunzi wenye mahitaji ikiwemo wenye ulemavu.

"Kama Serikali tuona ni faraja kwani fedha hizo zitakwenda kuchochea vijana wetu na kuamini hakuna kijana atakosa elimu kutokana na hali ya uchumi"amesema Mapunda.

Mapunda amesema hayo wakati akizindua maandalizi za Mbio 'Marathon' katika Viwanja vya TIA jijini Dar es Salaam zitakazofanyika Oktoba 26.

Amesema serikali inaungana na taasisi hiyo, kuhakikisha lengo la mbio hizo linatimia kwa kuungana na wadau mbalimbali ili malengo yaliyokusudiwa yatimie kwa kundi lililolengwa.

Amesema malengo ya zakutunisha mfuko kwa ajili ya ada wanafunzi walio na mahitaji maalumu kama vile watu wenye ulemavu wakiwemo Wasichana wenye watoto.

“Niwapongeze TIA kwa kubuni mradi huu mkiwambuka hasa wenye mahitaji maalumu, ambao watatimiza ndoto zao, kwa kuwa na uhakika wa kusoma,” alisema Mapunda.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo amesema Taasisi hiyo ilifanya utafiti na kubaini kwamba wapo wanafunzi ambao wanafanya vizuri katika masomo, huku baadhi yao walishindwa kumudu gharama za masomo na kurudi nyumbani.

“Mara nyingi baadhi ya wanafunzi huja ofisini kangu wakiomba msaada wa kulipiwa ada, kama Taaisi tukafikiria kuja na wazo hili ambalo linaweza kuwa suluhisho kwa wanafunzi wenye mahitaji ya kusaidiwa.

“Kuna wanafunzi ambao ni mama vijana ‘young mother's’ ambao wana familia na ni wadogo, ana mtoto anakaa nae hosteli, ana msaidizi, ana ndoto ya kusoma” amesema Prof. Pallangyo.

Alisema kauli mbiu ya mbio hizo ni ‘Run, Inspire and Support’ na kwamba pia lengo ni kuimarisha afya kwa wanafunzi na walimu, pia kukabiliana na Magonjwa Yasiyoambukiza (NCDs).

“Tunaandaa ‘TIA Marathon’ zitafanyika Oktoba 26, mwaka huu, tunalenga kuunga mkono serikali kwa namna anavyosaidia vijana kupata elimu, kuwasaiadia ambao hawana uwezo na zitakuwa za kilomita tano, 10 na 21.”

Amesema kuwa wataoshiriki watakuwa makundi matatu ambapo kundi la Kwanza sh.150,000 na kundi la pili 100,000 huku kundi la Tatu sh.30,000.

prof.Pallangyo ametaka wadau kuunga mkono Mbio za TIA ili fedha ziweze kutunisha mfuko kwa wanafunzi hao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA Profesa William Pallangyo akizungumza kuhusiana na Mbio walizoziandaa kwa ajili ya kutunisha mfuko kwa wanafunzi wenye mahitaji wakiwe wenye Ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda akizungumza mara baada ya Uzinduzi wa maandalizi ya Mbio za  TIA zitazofanyika Oktoba mwaka huu.




Picha za pamoja za makundi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa maandalizi ya Mbio za TIA zitazofanyika Oktoba mwaka huu 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad