JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


LAFARGE TANZANIA YASAIDIA SARUJI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MPUGUSO WILAYANI RUNGWE

Share This
Mkurugenzi mawasiliano na Masoko wa kampuni ya saruji la Lafarge Tanzania Allan Chonjo akiwaeleza wananchi wa kijiji cha Mpuguso kata ya Mpuguso wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwamba kampuni hiyo imetoa mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Cha Afya cha kata hiyo, kushoto ni mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla.
Wakazi wa kijiji cha Mpuguso wilayani Rungwe mkoani Mbeya wakishangilia baada ya kupata taarifa za msaada wa saruji kutoka kampuni ya Lafarge Tanzania.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipokea mifuko ya saruji kutoka kwa Maofisa wa kampuni ya Lafarge Tanzania kwa ajili wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha kata ya Mpuguso kilichopo wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya,(kushoto ni Fundi Mshauri wa ujenzi wa gharama nafuu wa Lafarge Evarist Mnyema,Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Allan Chonjo na Meneja wa Habari na Mahusiano Straton Bahati.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akishirikiana na viongozi wa Kijiji cha Mpuguso kubeba mfuko wa saruji kati ya mifuko 150 iliyotolewa na kampuni ya Lafarge Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akitoa neno la shukurani mara baada ya kukabidhi mifuko 150 ya saruji iliyotolewa na kampuni ya Lafarge Tanzania, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Masoko wa Lafarge Allan Chonjo, kulia ni Diwani wa kata ya Mpuguso.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akishiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mpuguso wilayani Rungwe mkoani Mbeya mara baada ya kukabidhi mifuko 150 ya saruji iliyotolewa na kampuni ya Lafarge Tanzania.
---
Lafarge Tanzania (Mbeya Cement Company), imetoa msaada wa mifuko mia moja hamsini (150) ya saruji ya Tembo ikiwa ni msaada wake kuchangia ujenzi wa kituo cha afya cha kijiji cha Mpuguso kilichopo wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.

Akiongea wakati wa makabidhiano ya msaada huo, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo amesema “Lafarge Tanzania inaelewa kwamba afya ndio kitu cha thamani zaidi katika maisha ya binadamu na kwa sababu hiyo tumeona ni wajibu wetu kuchangia maendeleo ya jamii hii ambayo tunayoishi. Tunasaidia ujenzi wa kituo cha afya Mpuguso kwakuwa tunaelewa kwamba afya njema ndio msingi muhimu wa jamii kuweza kupata maendeleo.”

Chonjo alisema kwamba kampuni hiyo ya saruji inaamini kuwa biashara ni kipaumbele chake lakini inaamini kwamba kusaidia jamii ni jukumu lake la msingi. Msaada huo uliopokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kijijini Mpuguso leo ni sehemu programu ya Lafarge Tanzania kusaidia jamii na umelenga kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa na wananchi unakamilika mapema ili kuboresha utoaji huduma za afya katika eneo hilo.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alielezea kufurahishwa kwake na Lafarge katika kuitikia wito wa wananchi haraka na kutoa msaada huo. Mkuu huyo wa mkoa aliwahakikishia Lafarge kwamba msaada huo utatumika ipasavyo kukamilisha mradi huo ili kuboresha maisha ya watu na kuongeza kwamba kituo hicho kitahudumia maelfu ya wakazi wa Mpuguso na maeneo ya jirani ambapo kituo cha karibu zaidi cha afya kipo umbali wa takribani kilomita 60 kutoka eneo hilo.

Makalla alisema kwamba baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho, wakazi wa Mpuguso na maeneo ya jirani watapata huduma za msingi za afya ambazo ni pamoja na ushauri wa kitabibu, msaada wa madawa, utoaji chanjo kuzuia magonjwa mbalimbali pamoja na kutoa ushauri nasaha kuhusu afya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad