Baadhi ya wateja wa benki ya CBA wakipata futari iliondaliwa na benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania, DK. Gift Shoko akiongea na wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) wahudhuria futari maalumu iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
4/5/12:Baadhi ya wateja wa benki ya CBA wakipata futari iliondaliwa na benki hiyo katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Imam Mkuu wa Masjid Ma, Amour Sheikh Issa Othuman Issa akitoa mawaidha wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya CBA katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wateja wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CBA, Dk.Gift Shoko (wa nne kushoto) na Imam Mkuu wa Masjid Ma, Amour Sheikh Issa Othuman Issa (wa tano) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa waandamizi wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake.
Yafuturisha wateja wake Dar es Salaam. Benki ya CBA Tanzania imewafuturisha baadhi ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuboresha uhusiano na wateja ambapo pia itawaandalia wateja wake futari kwenye maeneo mbalimbali yalipo matawi nchini. Akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na CBA Tanzania kwa wateja katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Dk.Gift Shoko alisema “ Tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote kwa kuendelea kuiamini benki yetu katika kupata bidhaa na huduma za kibenki na ndio maana tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili pia tuweze kujadiliana na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo kwenye futari hii”.
Alisema Benki ya CBA Tanzania huwa inakutana na kushirikiana na wateja wake katika masuala mbali mbali ya jamii ikiwemo michezo burudani na hata katika matukio ya kuchangia kuinua sekta mbali mbali mfano afya na elimu. “Lakini leo ni siku muhimu kwetu hapa Dar es Salaam kwa kuwa tunafuturu pamoja na kutakiana mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani ambao unaendelea”.
Dk.Shoko aliahidi kuwa Benki itaendelea kuboresha bidhaa na huduma zake ili ziendelee kuwa na ubora wa hali ya juu kabisa ikiwa ni pamoja na kubuni huduma mbalimbali za kuwarahishia maisha wateja wanapohitaji kupata huduma za kibenki na kuboresha shughuli zao.“Benki ya CBA Tanzania tunawatakia mfungo mwema wa Ramadhani lakini pia maandalizi mema ya sikukuu!, endeleeeni kufurahia huduma zetu mbalimbali na msiache kutembelea matawi yetu au kutembelea mtandao wetu kwa njia ya kisasa ya kuona huduma zetu mbalimbali kama vile huduma ya mkopo wa bima ambayo inaonekana kuwa mkombozi kwa watu wengi,mikopo ya kununua nyumba yenye masharti nafuu pia tunatoa huduma ya M-Pawa kwa kushirikiana na Vodacom inayowezesha wateja wa M-Pesa kuweka akiba na kupata mikopo kwa haraka na bila masharti magumu.”
Alisema Benki ya CBA Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.Bado CBA ina mpango wa kutoa misaada katika mikoa mbalimbali kwa dhumuni la kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu. CBA Tanzania ni sehemu ya CBA Group iliyopo katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, CBA Tanzania ina matawi kumi na moja yaliyosambaa sehemu mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment