JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WASHINDI WA BAHATI NASIBU DKT. TANZANIA “FIESTA KONDOM” WAREJEA WAKITOKEA DUBAI.

Share This
 Washindi wa shindano la bahati Nasibu la Fiesta condoms Bw & Bi. Justin Tinieshimo wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea mapumzikoni Dubai mwishoni mwa juma. Washindi hao waliweza kufurahia siku saba za mapumziko mjini Dubai katika safari iliyodhaminiwa na Shirika la DKT Tanzania katika kutekeleza ahadi ya ushindi wao wa droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa Chapa mpya ya “Fiesta condoms” miezi miwili iliyopita Ledger Plaza hotel jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa shirika la DKT Tanzania Bi. Hellen Kimati akitoa zawadi ya shada la maua kwa washindi wa shindano la bahati nasibu la Fiesta condoms Bw & Bi. Justin Tinieshimo mara baada ya wageni hao kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea mapumzikoni Dubai mwishoni mwa juma.
 Mshindi wa shindano la bahati nasibu Bi. Gloria Tinieshimo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili akitokea mapumzikoni Dubai mwishoni mwa juma. (Kulia) ni mume wake Bw. Justin Tinieshimo ambaye aliongozana naye katika safari hiyo ya wiki nzima iliyodhaminiwa na shirika la DKT Tanzania mara baada ya wawili hao kuibuka washindi wa droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa chapa ya Fiesta condoms miezi miwili iliyopita Ledger Plaza hotel jijini Dar es salaam.

KATIKA jitihada za kutangaza matumizi ya njia za uzazi wa mpango na kuzuia mimba zisizotarajiwa na magonjwa yanayo ambukizwa kwa kujamiiana (STDs) nchini, miezi miwili iliyopita katika siku ya wapendanao (valentine day), DKT International Tanzania shirika lisilo la kiserikali ambalo ni moja kati ya watoaji wakubwa wa bidhaa za uzazi wa mpango na afya ya uzazi nchini ilifanya uzinduzi wa aina mbalimbali za kondom zenye ubora zilizopewa jina la “Fiesta kondom” huko Bahari Beach Ledger Plaza hotel, Dar es salaam.

Wakati wa uzinduzi, shindano la bahati nasibu lilifanyika ambapo wanandoa watatu walishinda safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda na kurudi Zanzibar, Afrika ya kusini na Dubai.


Wakielezea msisimko wao wakati wa kurudi kutoka katika safari yao mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), washindi wa safari ya kwenda Dubai ambao walitembelea Dubai kwa mara ya kwanza walifurahia wiki nzima ya kukaa na kutalii Dubai na Abu dhabi, waliishukuru DKT International Tanzania kwa kutimiza ahadi yao na kwa kuifanya safari yao kuwa ya kukumbukwa.
Katika mahojiano wakiwa uwanja wa ndege, washindi walisema kuwa safari imewapa fursa ya kutembelea sehemu za kusisimua huko Dubai kama Burj Khalifa, ambalo ni jengo refu kuliko yote Dubai, maduka makubwa ya kufanyia manunuzi pamoja na mashindano ya mbio za magari ya Formula one huko Dubai.

“Nimefurahia sana kupata safari hii ya kusisimua kwenda Dubai na mke wangu. Tuliweza kujionea wenyewe na kushuhudua mengi yanayoongelewa kuhusu jiji la maajabu. Ninapenda kuishukuru DKT International Tanzania kwa fursa hii nzuri na tunaahidi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Fiesta kondom kila wakati ambapo tutahitajika kufanya hivyo. Alihitimisha bwana Justin Tinieshimo.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Fiesta Kondom bwana Davis Kambi amesema “Tunafuraha kuhitimisha safari ya washindi wetu wa safari ya Dubai na wanashukuru kuwa na fursa hiyo ya kukumbukwa wakiwa Dubai.” Nyakati kama hizo ndizo ambazo zinahusu bidhaa ya Fiesta Kondom, kuleta wanandoa karibu katika nyakati za upendo; DKT International Tanzania imejidhatiti kulete wanandoa pamoja chini ya kampeni za Intimacy by Fiesta ambazo zitahakikisha wanandoa wengine wanapata safari ya kwenda katika sehemu za mbalimbali mwaka huu.
Bwana Kambi alitumia fursa hiyo kuhakikisha kuwa washindi wa zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar tayari walisha kwenda na walisha rejea.
Aliwashukuru wote walioshiriki katika kuhakikisha kuwa shindano la bahati nasibu la uzinduzi wa Fiesta Kondom Valentine limefanikiwa. Fiesta Kondom itafanya tena tamasha la kukutana la wanandoa mwaka ujao ambapo wanandoa wataweza kushinda zawadi nzuri.
Bidhaa ya Fiesta Kondom ya DKT International Tanzania ilizinduliwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na inapatikana katika nchi zaidi ya 40 duniani kote na sasa katika mikoa yote mikubwa ya Tanzania. Fiesta ina zaidi ya ladha 55 tofauti za kondom na zaidi ya aina 60 tofauti. Lakini kwa kuanzia DKT International Tanzania imetambulisha aina 5 tofauti; Fiesta Heat, Fiesta Ultra-thin, Fiesta Strawberry, Fiesta Max dotted and Fiesta Neon! DKT International Tanzania inapanga kuzindua aina zingine 3 za kondom zinazokamilishwa kwa utofauti wa aina mbalimbali kabla ya mwisho wa mwaka 2016.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad