JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MKURUGENZI MPYA NIGERIA ATEULIWA NA SHIRIKA LA NDEGE ETIHAD.

Share This
SHIRIKA la Ndege la Etihad ambalo ni shirika la ndege la taifa katika falme za kiarabu limemteua George Mawadri (Pichani)kuwa Mkurugenzi mpya wa shirika hilo nchini Nigeria, ambapo atahusika na kusimamia shughuli za usafiri wa ndege za Etihad na biashara ya usafari wa anga na kuimarisha biashara hiyo nchini Nigeria

Mkurugenzi huyo mpya amekuwa na uzoefu katika sekta hiyo ya usafirishaji. Amefanya kazi katika Shirika laNdege la British Airways kwa miaka 19 akiwa nchini Uganda, Kenya na Zambia  pamoja na kutoa huduma katika nchi za Zimbabwe, Malawi, Ethiopia, Rwanda, Sudan na Sudan Kusini.

Nimefurahia uteuzi kwenye nafasi hiyo muhimu katika Shirika Ndege la Etihad katika sehemu ya sekta ya anga inayokuwa kwa kasi” Alisema Mawadri. Nitafanya kazi kwa ushirikiano na kuwa mbunifu ili kuongeza ufanisi katika shirika letu, kupanua masoko na kuwapa wateja wetu huduma bora.

Makamu wa Rais wa Shirika la Ndege la Etihad, Danny Barranger alisema “Nina furaha na imani kwamba George ataongoza vyema timu yetu iliyopo Nigeria ili kuongeza soko la biashara yetu nchini humo. Uzoefu wake kwenye biashara hii na rekodi yake ya mafanikio katika sekta ya anga Afrika na maeneo aliyofanya kazi ni jambo ambalo litamwezesha kuendeleza kuongeza ufanisi katika shirika la Etihad ambalo liliona umuhimu wa kumuweka katika nafasi hiyo.

Shirika la Ndege la Etihad lilizindua safari zake kati ya Lagos na Abu Dhabi 1 Julai 2012 na hivi sasa kuna safari nne kwa wiki kwa kutumia ndege ya Airbus A330-200 yenye uwezo wa kubeba abiria 254 ambapo daraja la kati abiria 18 na daraja la uchumi abiria 236.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad