jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

SASA WATANZANIA KUONGEA KWA SAA MOJA BURE KILA SIKU.

Share This
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) Balozi wa Vodacom Tanzania, Nasibu Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia(kulia) na Zarina Hassan(kushoto)wakionesha mabango yenye ujumbe wa jinsi ya kujiunga na Promosheni ya “Ongea Deilee”, wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.
002.ONGEA
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao( kushoto) na Zarina Hassan(Kulia) wakionyeshwa tangazo la promosheni ya”Ongea Deilee” kwenye simu lililofanywa na msaanii wa muziki wakizazi kipya Abdul Nasibu”Diamond Platinum”( katikati) wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Promosheni hiyo itawawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.
003.ONGEA
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya”Ongea Deilee” Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom leo jijini Dar es Salaam,anayeshuhudia kulia ni Balozi wa Vodacom Tanzania,Nasibu Abdul (Diamond Platinum)
004.ONGEA
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya”Ongea Deilee” Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi waongeapo jumla ya dakika 10 Vodaocom kwenda Vodacom, leo jijini Dar es Salaam,wengine katika picha kutoka kushoto,Zarina Hassan, Balozi wa Vodacom,Nasibu Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.


SASA ni wakati wa watanzania kuongea, ambapo kuanzia leo wateja wa Vodacom, mtandao unaongoza nchini wataweza kuongea bure kwa saa nzima!


Kupitia ofa yake maalum kwa wateja ya Ongea Bure Deilee, itakayokuwa ya miezi mitatu mfululizo, wateja wa Vodacom wataweza kuongea kwa muda wa saa moja bure kila siku.

Ili kujiunga na ofa hii ambayo haijawahi kutokea nchini, mteja anachotakiwa kufanya ni kuongea kwa dakika 10 kila siku kwa viwango ya malipo vya kawaida na hapo hapo atapata ofa ya kuongea kwa muda wa saa moja bure.

Ofa hii ya Ongea Bure Deilee pia imemuhusisha mwanamuziki nguli wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz, ambaye moja ya kibao chake kinachotamba ni ‘Number One’, ambao pia ni mwito wa simu maarufu kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Bw. Ian Ferrao amesema “Ongea Bure Deilee ni ofa ya aina yake kutolewa kwa wateja wa Vodacom popote walipo nchini. Ofa hii imebuniwa kubadilisha maisha ya wateja wetu walio wengi na kuendelea kuyafanya kuwa murua!”

Aliendelea kusema kuwa Vodacom Tanzania imedhamiria kuendelea kuvuka kile ambacho wateja wake wanakitarajia, kwa kuwaunganisha kwa viwango nafuu ambavyo wanazoweza kuvimudu, lengo kubwa likiwa ni kuweza kuwainua kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Ofa hii itatolewa kwa wateja milioni moja wa kwanza watakaojiunga kila siku kupitia ujumbe mfupi wa maneno ambapo watakuwa huru kuongea wakati wowote watakao, iwe usiku au mchana, ili mradi watakaowasiliana nao ni watumiaji wa mtandao wa Vodacom.

“Huu ni mwendelezo wa kampeni yetu ya Maisha ni Murua ambayo jitihada zetu katika kuwaletea wateja ofa za kipekee na ambapo kupitia ubunifu wa kutumia mtandao, tunawezesha maisha ya wateja wetu wote nchini kuwa murua. Kama ambavyo tunasema siku zote, tutaendelea toa huduma zinazowawezesha wateja wetu kuwasiliana kwa urahisi na wapendwa wao na hata katika shughuli zao za uzalishaji mfululizo,” aliongeza Ferrao.

Kwa upande wake, Diamond Platinumz, ambaye sasa ni balozi wa Vodacom alisema “Ninayo furaha kuwa sehemu ya kampeni hii kabambe kutoka Vodacom. Nilipopata taarifa kwa mara ya kwanza kuhusu ofa hii nilipata mshtuko na kusema dah, Vodacom imeleta tena bonge la ofa, kwa hakika ofa hii itaniunganisha na washabiki wangu, marafiki, familia na wafanyabiashara wengine”.

Aliongeza “Nitawaelezea washabiki wangu, familia na marafiki jinsi wanavyoweza kufanya maisha yao kuwa murua kupitia kampeni hii mpya kutoka Vodacom. Wanachotakiwa kufanya ili kujiunga na kufurahia ofa ya Ongea Bure Deilee ni rahisi tu, yaani ni kupiga simu *149*01#.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad