JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ALIKIBA NA WILDAID WATOA WIMBO KUPINGA UJANGILI WA TEMBO.

Share This
Hatimaye Alikiba ametoa wimbo wake “Lupela” uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wake Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa sasa. Wimbo huo ni sehemu ya kampeni ya “Ujangili Unatuumiza Sote” iliyozinduliwa mwaka jana na WildAid na African Wildlife Foundation mashirikia yanayofanya kazi pamoja barani Afrika na Asia kupunguza mahitaji ya bidhaa zitokanazo na wanyamapori na kuongeza uelewa wa janga la ujangili linaloikabili Afrika. Video ya wimbo huo imerekodiwa jijini Los Angeles Marekani ambapo Alikiba alikuwa mgeni rasmi kweye hafla maalum iliyoandaliwa na shirika la uhifadhi wanyamapori la kimataifa la WildAid. Chini ya kauli mbiu “Ujangili Unatuumiza Sote”, Alikiba amefanya kazi na WildAid kuongeza uelewa wa Watanzania kuhusu tatizo la ujangili wa tembo ambao wamechinjwa kwa maelfu miaka ya hivi karibuni kwa ajili ya meno yao.
Katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es salaam, wageni mbalimbali na waandishi wa habari walipata fursa ya kuusikiliza wimbo na kuangalia video yake kwa mara ya kwanza. "Tunaona fahari sana kuwa na Alikiba kama Balozi wa WildaAid”, alisema Salome Gasabile Meneja wa WildAid Tanzania. “Katika mwaka mmoja uliopita, yeye na meneja wake Seven wamefanya kazi bila kuchoka kupinga ujangili wa tembo na tunaamini wimbo huu utakuwa na faida kubwa katika vita dhidi ya ujangili”. “Nina furaha kubwa kuwa sehemu ya mradi huu. Naamini kila mara watu wakisikiliza wimbo huu watakumbuka faida ya tembo kwa urithi na uchumi wa bara la Afrika. Wanaingiza pesa nyingi kupitia utalii na fedha hizo zinaweza kusaidia kuleta ajira, kujenga shule na hospitali kwenye jamii zinazozunguka hifadhi za taifa,” alisema Aleya Aleya Janell ambaye ameshiriki kwenye video ya wimbo huo kama Lupela.
Asha Franklin, aliyeshiriki kama tembo wanaocheza muziki amefanya kazi na Rihanna na Ciara katika video mbalimbali amesema “Hii video ni nzuri kwani imechanganya burudani ya muziki na jambo zuri kwa jamii” Ushiriki wetu kama tembo wananocheza muziki ilikuwa ni ubunifu wa hali ya juu lakini pamoja na kwamba ni burudani bado unaweza kuona faida ya kubwa ya wimbo huu.” Video hiyo iliongozwa na Kevin Donovan, huku ikirekodiwa na kutengenezwa na muandaaji filamu maarufu wa Hollywood Brian Rumsey ikiwa ni mchango wake kwa kampeni hiyo. Oththan Burnside, ambaye ameishafanya kazi na wanamuziki wengi maarufu kama Rihanna na Sean Paul alihusika kuandaa wimbo huu na staili ya uchezaji wa tembo.
“Tuufanye mwaka 2016 mwaka wa tembo – mwaka ambao hatimaye tutakumbuka kuwa hatimaye tuikomesha ujangii wa tembo na kuwapa tembo nafasi ya kuishi” alisema Burnside. “Tusaidie kuokoa maisha ya wanyama hawa wazuri,” alisema Burnside. Kwa mujibu wa shirika la WildAid wimbo huo hautatumika kibiashara na unapatikana bure kwa mashabiki kupakua au kusikiliza kweye mtandao wa www.yearoftheelephant.org Uzinduzi wa wimbo huo umeenda sambamba na kampeni ya #jointheherd inayofanyika kupiti mitandao ya kijamii ikiongozwa na wau maarufu mbalimbali wakiwemo muigizaji Lupita Nyong’o, Jackie Chan na Jacqueline Mengi ambao wanaendelea kuhamasisha watu kupitia www.yearofthelephant.org ambapo watu huweza kujitengenezea picha zao na kuzitumia kwenye mitandao ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad