jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEZWA KUWA NI ZAUONGO

Share This
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA KWA UMMA
Hivi karibuni zimeibuka taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikimnukuu Waziri wa Nishati na Madini, George B. Simbachawene  akisema kuwa mitambo yote ya uzalishaji umeme nchini inamilikiwa na Kampuni binafsi.

Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa taarifa hizi ni za uongo kwani Waziri Simbachawene hajawahi kutoa tamko la kuwa mitambo ya kuzalisha Umeme yote nchini ni ya kampuni binafsi bali alichosema ni  kuwa, baadhi ya mitambo ni ya kampuni binafsi na mingine inamilikiwa na Serikali.

Mitambo inayomilikiwa na Serikali ni:-

1    Kinyerezi I (Gesi) yenye uwezo wa MW 150 ambapo MW 35 zimewashwa leo 12 Oktoba 2015;
2    Ubungo I (Gesi) yenye uwezo wa MW 102 ambayo kwa sasa inazalisha MW  85;
3    Ubungo II (Gesi) yenye uwezo wa MW 105 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;
4    Tegeta (Gesi) yenye uwezo wa MW 42 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;
5    Nyakato (Mafuta) yenye uwezo wa MW 60 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;
6    Kidatu (Maji) yenye uwezo wa MW 204 ambayo kwa sasa inazalisha MW 27;
7    Kihansi (Maji) yenye uwezo wa MW 180 ambayo kwa sasa inazalisha MW 45;
8    Pangani (Maji) yenye uwezo wa MW 68 ambayo kwa sasa inazalisha MW 17;
9    Nyumba ya Mungu  (Maji) yenye uwezo wa  MW 8 ambayo kwa sasa inazalisha MW 5;
10 Hale (Maji) yenye uwezi wa MW 21 ambayo kwa sasa inazalisha MW 4; na
11Mtera (Maji) yenye uwezo wa MW 80 ambapo mitambo yake imezimwa (MW-0);

Kwa hiyo, Jumla ya kiasi cha umeme kinachopatikana katika mitambo hiyo kwa sasa ni Megawati 337 kati ya Megawati 870 zinazotakiwa kuzalishwa.


Mitambo inayomilikiwa na watu binafsi ni:-

1    IPTL (Mafuta) yenye uwezo wa MW100 ambayo kwa sasa inazalisha MW 80;
2    Aggreko (Mafuta) yenye uwezo wa MW 70 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;
3    SONGAS(Gesi) yenye uwezo wa MW180 ambayo kwa sasa inazalisha MW 158; na
4    Symbion (Gesi) yenye uwezo wa MW 112 ambayo kwa sasa inazalisha MW 74.

Hivyo mitambo hii ya watu binafsi inazalisha umeme wa kiasi cha Megawati 382 kati ya Megawati 462 zinazohitajika.

Ieleweke kuwa Serikali inajitahidi kuiwasha mitambo hiyo yote inayomilikiwa na Serikali na Binafsi ili izibe pengo la umeme wa maji ambao umepungua kutoka MW 561 hadi MW 88. Ili nchi  isiwe na mgawo wa umeme zinahitajika  MW 1332 ambapo kwa sasa kiasi cha umeme kinachopatikana ni Megawati 719.

Awali tulikuwa na upungufu wa megawati takribani 450 lakini tumefanya juhudi za kuwasha mitambo mbali mbali tangu wiki iliyopita na sasa upungufu uliobaki ni kati ya MW 200 na 250.

Serikali kupitia TANESCO inatoa rai kwa Watanzania kuendelea kuvumilia kipindi hiki cha mpito kwani inajitahidi kwa hali na mali kuwasha mitambo iliyobaki ya gesi ya Kinyerezi yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150 hivyo hadi ifikapo tarehe 20 Oktoba, 2015 hali ya upatikanaji wa umeme itaanza kutengemaa.

 Asanteni na poleni kwa usumbufu unaojitokeza.

Imetolewa na;

WIZARA YA NISHATI NA MADINI



Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad