JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHEREHE ZA MKONDO WA BAA ZANOGESHA PROMOSHENI YA TUSKER FANYA KWELI KIWANJANI

Share This
 Mkazi wa Mikocheni na mpenzi wa kinywaji cha Tusker Bw. Gaspar Makongoro (38) (katikati) akizungumza na mshereheshaji wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash (kushoto) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam katika promosheni ya Tusker fanya kweli kiwanjani .Anaeangalia (kulia) ni balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi.
  Msimamizi wa Mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Sinza na Mwenge Anitha Moshi akimvalisha fulana mkazi wa Changanyikeni Honest Oscar kwenye hafla ya kuzipongeza baa 7 zilizo kwenye mkondo mmoja ambazo kwa pamoja ziliibuka baa za wiki kwenye shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani lililofanyika katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam. Baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.
 Mkazi wa Sinza Bw. Nasib Ngoya (kulia) akionyesha zawadi yake  ya mfuko wenye fulana aliopewa katika hafla ya kuzipongeza baa 7 zilizo kwenye mkondo mmoja ambazo kwa pamoja ziliibuka baa za wiki kwenye shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani lililofanyika katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam. (Katikati) ni Mtangazaji wa redio Efm na mshereheshaji wa Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash na Anaeshuhudia (kushoto) ni Meneja mipango na Matukio-SBL Lulu Mduma.
 Mpenzi wa kinywaji cha Tusker na mkazi wa Sinza Rosemary John (Kulia) akifurahi kwa pamoja na Meneja Mipango na matukio-SBL Lulu Mduma (kushoto) baada ya kukabidhiwa zawadi ya fulana kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ambayo ilifunga kambi katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam kusherekea ushindi wa baa zaidi ya sita zilizo kwenye mkondo mmoja ambazo kwa pamoja ziliibuka washindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker. Baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.
 
 Mkazi wa Sinza, Prosper Minja akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Meneja Mipango na Matukio-SBL Lulu Mduma katika shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam ambapo baa 7 zilizopo kwenye mkondo mmoja ziliibuka baa za wiki kwenye promosheni hiyo ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.

KAMPUNI ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kwa udhamini wa bia bora Afrika ya Tusker wiki hii imekuja na mvuto wa aina yake baada ya kuzikutanisha na kuzifanyia sherehe baa mbalimbali zilizopo kwenye mkondo/mtaa  mmoja.

Tukio hilo ambalo lilionekana kuwafurahisha wapenzi wa bia ya Tusker lilifanyika wikiendi ya Jumamosi katika mtaa wa Legho, Sinza jijini Dar es salaam ambapo baa zaidi ya 6 zote kutoka Sinza ziliungana kushiriki katika sherehe hizo. Baa hizo ni:- Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa sherehe hizo, Meneja Masoko  wa bia ya Tusker Bi. Nandi Mwiyombella alisema mpaka kufikia sasa kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani imepokelewa vyema na wateja wa bia hiyo jijini Dar na hata mikoani ambapo kampeni hiyo pia inaendelea. 

“Promosheni hii ni muendelezo wa Kampeni ya Tusker Fanya Kweli  kama inavyoonekana kwenye mabango na matangazo ya radio pia ni kampeni inayolenga kuleta muamko wa hamasa kwa watanzania waweze kutekeleza malengo yao waliyoyapanga“.

Alisema kuwa katika maisha baadhi ya malengo yanayotarajiwa  ni pamoja na kujenga nyumba, kufunga ndoa, kununua gari  kuanzisha biashara na kadhalika. Mafanikio ni hatua na kila hatua inastahili pongezi na kusherehekea matunda ya mafanikio hayo,bia ya Tusker inatambua juhudi za watanzania ambapo juhudi lazima ziendane na utekelezaji na katika kufanya hivyo basi mtanzania anapiga hatua hivyo kupitia Kampeni hii Bia ya Tusker inampongeza mtanzania kwa kila hatua anayopiga. 

Tunaamini kwamba kupitia Kampeni hii ujumbe huu utawafikia watanzania wote kwa urahisi zaidi.Bia ya Tusker inatoa hamasa na kusema tufanye kweli na Tusker inatambua kila hatua ya maendeleo iliyopigwa.

Bi. Mwiyombella aliongeza kuwa sherehe za Tusker Fanya Kweli Kiwanjani pia zinalenga kujenga uaminifu kwa wateja na kurudisha shukrani kwao huku wakisherekea kwa pamoja na bia waipendayo ya Tusker. Sherehe hizi za mkondo wa baa tofauti ni muendelezo wa kampeni ya Fanya Kweli Kiwanjani; ikiwa na mkusanyiko wenye ari na muamko zaidi na hivyo ni burudani zaidi sambamba na zawadi nyingi zaidi kwa wateja.

Kampeni ya Fanya Kweli Kiwanjani itaendelea mpaka mwisho wa mwezi wa kumi huku sherehe za mkondo wa baa zikitegemewa kuwafikia pia mashabiki wa bia ya Tuskerwaliopo Arusha na Mwanza kabla ya kampeni kufikia tamati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad