JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MSANII WA WA AFRIKA KUSINI K.O ATUA DAR KWA ZIARA

Share This
  Msanii maarufu nchini Afrika Kusini, K.O akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya ziara ya ktembelea vyombo mbalimbali vya habari hasa Televisheni na Redio na kuangalia mziki wa hapa nchini katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.
 Msanii maarufu nchini Afrika Kusini,K.O (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ziara yake nchini leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Tsholofelo Moremedi  wa Cashtime Life Menagement na Kulia Afisa Mtendaji Mkuu wa Cashtime Life, Thabiso Khati.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Msanii K.O juu ya ziara yake nchini katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya JamiiMSANII marufu nchini, Afrika Kusini,K.O  ametua nchini kwa ziara katika vyombo vya habari kuona jinsi wanavyoshirikiana na wasanii nchini.

Akizungumza na waandishi habari jijini,K.O  amesema ziara hiyo anatarajia kupita katika vyombo vya habari  vilivyo nchini na kuona jinsi gani wanavyofanya nano kazi wasanii.

K.O ameingia nchini jana ambapo kazi yake imeanza jana na itaendelea hadi Septemba 16 mwaka  huu na kuangalia uwezekano wa kushirikiana na wasanii nchini.

Msanii huyo ameshinda tuzo mbalimbali na ametamba wimbo wa Caracara na ameweza kushirikiana na baadhi ya wasanii nchini akiwemo Vanessa Mdee katika wimbo  Nobody but me.

K.O kufanya ziara nchini ni ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na akitoka nchini anaratarajia tena kufanya ziara nchini Kenya pamoja na kufanya onyesho la mziki katika ukumbi wa Ebony Mjini humo.

Amesema Tanzania inakuwa kwa kasi katika sekta ya mziki Afrika na wasanii wana vipaji vinavyoonekana na kufanya waweze kujulikana kimataifa na kuongeza kuwa anatarajia kutengeneza  mziki mpya atakao washirikisha wasanii watanzania.

K.O anasimamiwa na Kampuni ya Cashitime Life ya nchini inayojihusisha  burdan ambapo kampuni hiyo imeweza kumtangaza ndani ya nchi huyo pamoja na nje.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad