Na Ally Daud –Maelezo
Dar es salaam
MWILI wa marehemu wa aliyekuwa Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Ompeshi Kombani (56) umeagwa leo Katika Viwanja vya Karemjee jijini Dar es salaam.
Waziri huyo ambae pia alikuwa mgombea ubunge Jimbo la Ulanga Mashariki amefariki dunia Septemba 24, mwaka huu katika hospitali ya Apollo Nchini India kutokana na ugonjwa wa saratani ya kongosho.
Maelfu ya waombolezaji yakiongozwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Galib Bilal pamoja na Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere na Mke wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete katika hafla fupi ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirisha kuelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi .
Wawakilishi wa mashirika na viongozi mbalimbali wa nchi walihudhuria katika viwanja hivyo wakiwemo mawaziri wa Tanzania Bara na Visiwani wakiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda ili kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Marehemu Kombani anatarajiwa kuzikwa kesho katika shamba lake huko Morogoro baada ya waombolezaji kupata nafasi ya kutoa heshima za mwisho katika viwanja wa Jamhuri mjini humo.
Aidha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda ametoa pole kwa wafiwa na kusisitiza kwamba jamii iendeleze ya yaliyoachwa na marehemu kwa ajili ya kujenga Taifa letu kwani alikuwa mstari wa mbele katika kupigania kuondoa malipo hewa ya watumishi wa Umma, kufanyakazi kwa bidii na kujawali watu .
Mbali na hayo Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wamepokea taarifa hizo kwa mstuko mkubwa kwani hawakutarajia kuachiwa pengo na Celina Kombani.
Vile vile Mwenyekiti na mwakilishi wa kituo cha kulelea yatima Good Hope Family ya Kigamboni Bw. Omari Rajabu amewaasa viongozi waliobakia kutowasahau kwani wamepoteza mama yao wa dunia ambaye alikuwa mstari wa mbele kuwapigania watu wasiojiweza.
Marehemu Kombani ameacha mume , watoto watano na wajukuu wanne pia ameacha pengo kubwa katika Serikali ya Jamhuri wa Muungano Wa Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mume wa marehemu Celina Kombani, aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ahmad Pangolani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Mawaziri wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mama Maria Nyerere, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Spika wa Bunge la Jamhuri, Mama Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria shughuli hiyo wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho wakati wa kuagwa mwili huo, kwenye Viwanja vya Karimjee, leo.
Mama Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Askari wa Bunge wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Celina Kombani, wakati likiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya shughuli la kuagwa kabla ya kusafirishwa kuelekea mkoani Morogoro kwa maziko.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na wananchi na baadhi ya Viongozi wakati wa shughuli ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria shughuli hiyo wakiwa kwenye Viwanja vya Karimjee wakisubiri kutoa heshima za mwisho. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment