Sehemu
ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa
mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
|
Mgombea
mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na wasanii na wananchi wengine alipokuwa akiwasili katika
viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi leo Mjini Korogwe ambapo alifanya
mkutano wa kampeni.
|
Mgombea
mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akiwapokea baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM katika
mkutano wa kampeni uliofanyika leo Korogwe. Jumla ya wanachama 25
walijiunga na CCM katika mkutano huo.
|
Sehemu
ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa
mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
|
Baadhi
ya wasanii waigizaji, Wema Sepetu (kulia) na Bibi Mwenda wakizungumza
na WanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza
kuwashawishi waichague CCM kutokana na mazuri mengi iliyowafanyia
wasanii.
|
Mgombea
mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akimtambulisha na kumuombea kura mgombea ubunge wa Jimbo la
Bumbuli, January Makamba (katikati) katika mkutano wa hadhara wa kampeni
wa mgombea mwenza uliofanyika Lushoto Jimbo la Mlalo. Kulia ni mgombea
wa ubunge Jimbo la Lushoto, Shaban Shekilindi.
|
Mgombea
Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Pius Chatanda akizungumza na
wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo walipojitokeza kwenye mkutano wa
hadhara wa mgombea mwenza leo viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi.
|
Mgombea
Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Pius Chatanda akizungumza na
wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo walipojitokeza kwenye mkutano wa
hadhara wa mgombea mwenza leo viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi kunadi
sera za CCM, huku mgongoni akiwa amebandika kipeperushi cha mgombea
urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
|
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Profesa 'Maji Marefu' akizungumza
na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza
uliofanyika Korogwe Mjini leo.
|
Sehemu
ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa
mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
|
Mwenyekiti
wa CHADEMA Kata ya Kwagunda, Salehe Abdullah (kushoto) akizungumza mara
baada ya kujiunga na CCM leo kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea
mwenza na kukikimbia chama chake cha CHADEMA.
|
Mgombea
mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanaCCM na
wananchi wa jimbo la Korongwe Mjini walipojitokeza kwenye mkutano wa
hadhara wa mgombea huyo leo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi.
|
Baadhi
ya wananchi wakiwa wamemsimamisha njiani mgombea mwenza wa CCM, Bi.
Samia Suluhu Hassan eneo la Mombo ili asikilize kilio na changamoto zao
kabla ya kuendelea na safari kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni Wilaya
ya Lushoto.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza huku wakiendelea na biashara zao sokoni hapo.
|
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza huku wakiendelea na biashara zao sokoni hapo.
|
Sehemu
ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha njiani mgombea mwenza wa
CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan eneo la Soko la Soni Lushoto ili asikilize
kilio na changamoto zao hasa akinamama kabla ya kuendelea na safari
kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni Wilaya ya Lushoto.
|
Mgombea
ubunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba (kushoto) akibadilishana
jambo na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Lushoto, Balozi Abdul Mshangama
leo katika Jimbo la Mlalo.
|
Sehemu
ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa
mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo katika Jimbo la Mlalo, Lushoto.
|
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mlalo, Shaban Omar Shekilindi akizungumza na wapiga kura wake jimboni Mlalo.
|
Mgombea
ubunge Jimbo la Bumbuli, January Makamba akizungumza na umati katika
mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza, Makamba akizungumza aliwaomba
wananchi wasikipe kura chama cha Chadema na ushilika wao wa UKAWA kwani
wapo kwa ajili ya mabadiliko ya nafsi zao na si vinginevyo.
|
Sehemu
ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa
mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo katika Jimbo la Mlalo, Lushoto.
|
Mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu (katikati) akimtambulisha mgombea ubunge wa Jimbo la Lushoto, Shaban Shekilindi.
|
Mgombea
mwenza, Bi. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge
wa Jimbo la Mlalo, Shaban Omar Shekilindi alipokuwa akizungumza na
wapiga kura wake jimboni Mlalo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com |
No comments:
Post a Comment