tamasha la bongo 50 lafana vilivyo usiku huu,kila mmoja auga mwaka kwa aina yake.!
Saturday, December 31, 2011
Sir Juma Nature akiliongoza kundi lake la Wanaume Halisi kutoka Temeke,akikamua jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Bongo 50,ndani ya viwanja Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo wakazi wa jiji hilo na vitongoji vyake walijumuika pamoja katika mpango mzima wa kuuaga mwaka kwa shangwe,tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel,kupitia huduma yake mpya ya Airtel Money.
Mmoja wa wasanii kutoka kundi la Wanaume Halisi Jb akikamua jukwaani.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mwana FA sambamba na Mwanadada Linah kutoka THT wakiimba kwa pamoja wimbo wao 'Yalaiti'.ambao kwa mara kwanza uliimbwa na mwanamuziki Mkongwe nchini,Bibi Kidude lakini wao wakaimba remix.
![]() |
| Mwanadada Linah akiwarusha vilivyo mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha la Bongo 50,ikiwemo na kuusubiria mwaka mpya. |
![]() |
| Mkali wa mashairi,Simba Mzee a.k.a Uncle Virus Afande Sele akikamua viulivyo usiku huu mbele ya mashabiki wake waliopagawa vilivyo,huku wakiungoja Mwaka mpya kwa hamu kubwa. |
![]() |
| Uncle Virus,Afande Sele akiwarusha vilivyo mashabiki wake usiku huu. |
![]() |
| Wadau,Pichani kulia Sebastian Maganga kutoka Clouds FM na rafiki yake nao walikuwepo kuuaga Mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012 ndani ya tamasha la Bongo 50,kwenye viwanja vya Lidaz Club. |
Watu mbalimbali wakiuaga mwaka kwa staili yao,mara ilipotimu saa sita kamili kabaaaaa....fataki na mayowe,shangwe kama kawaida.
Msanii mdogo kiumri lakini kipaji cha usanii kimekaa mahali pake,anaitwa Asley anayetamba na wimbo wake Naenda Kusema,akijiachia jukwaani na miondoko ya kiduku huku akiwakuna vilivyo washabiki na wapenzi waliokusanyika usiku huu kwenye viwanja vya lidaz Club,jijini Dar ambako tamasha la Bongo 50 linafanyika kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel.

Mmoja wa Ma-Dj Mahiri kutoka Clouds FM,Dj Zero akikamua vilivyo jukwaani na kuwarusha mashabiki kibao waliofika kwenye uwanja wa lidaz club katika mpango mzima wa kuuaga mwaka.
Washabiki wakiendelea kufuatilia makamuzi yanayoendelea jukwaani hivi sasa,wakati huo huo walioko majumbani wanaweza kuangalia onesho hili kupitia Clouds TV.
Wasanii wa kundi la Uswahilini Matola wakitumbuiza jukwaani hivi sasa na wimbo wao wa Kosa la Marehemu
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake wakiendelea kujitokeza usiku huu kwenye viwanja vya lidaz club,ambako tamasha la Mkusanyiko wa wasanii Bongo 50 concert linafanyika,pia ikiwa ni sehemu ya kuuaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka mpya.



















































