JERRY MURO afutiwa kesi yake ya kudaiwa kutaka kupokea rushwa ya sh mil 10,aachiwa huru.

Wednesday, November 30, 2011

Namshukuru Mungu,niko huru sasa.!



Jerry Muro na mke wake wakitoka mahakamani.


Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Pascal Kamara wakili wa Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama ya kisutu.
=====  =====  =======
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewaachia huru kwa mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jarry Muro na wenzake wawili.

Hakimu Frank Moshi, alisema anawaachia washitakiwa hao kwasababu upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi shaka.

Muro, Edmond Kapama pamoja na deogratius Mgasa walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba na kutaka kupokea rushwa ya Sh milioni 10 toka kwa aliyekuwa Muhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage. Mashitaka yao yalikuwa ni ya kula njama, kuomba rushwa na kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU shitaka linalowakabili Mgasa na kapama.

Muro baada ya kutoka mahakamani alitangaza kwa wanahabari kuwasamehe wabaya wake wote ambao ni viongozi wa serikali baadhi na baadhi ya maafisa wa polisi na kuwataka waandishi wa habari kushikamana kuendelea kuibua uozo unaoendelea bila woga.

Katika hukumu, hakimu Moshi alisema baada ya kuangalia ushahidi mahakama ilikuwa na maswali ya kujiuliza kama upande wa jamuhuri uliweza kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa ambapo shitaka la kula njama kwa nia ya kuomba rushwa ambalo linawahusu washitakiwa wote, ushahidi ulikuwa wa Wage.

Shahidi huyo wa tatu wa jamuhuri lisema alikutana na Muro kwenye mgahawa wa Califonia ambapo mawasiliano kati yao yaliendelea kwa njia ya simu ya mkononi.  Ushahidi huo ulikuwa hafifu kwasababu upande wa mashitaka haukuweza kuwasilisha karatasi ya mawasiliano kati yao kutoka kwenye kampuni ya mtandao wa simu (printout).

Vile vile alisema picha za CCTV iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa ni kivuli kisichoonyesha sura za watu badala yake wangeleta CD kuonyesha kwenye video ili watu waweze kutambulika kwa urahisi.  Mawasiliano ni jambo la msingi kwasababu ili kula njama ni lazima mawasiliano yafanyike hivyo kuna mapungufu makubwa katika shitaka hilo.

Dereva aliyemwendesha wa Wage alidaiwa kuwa na Wage pale mgahawa wa Califonia walipokutana na Muro, alitakiwa kuletwa athibitishe kama Wage na Muro walikutana upande wa mashitaka hawakumwita shahidi huyo.

Katika shitaka la kuomba rushwa lilowakabili wote katika ushahidi wake Wage, alieleza Muro na wenzake walimtaka awapatie Sh milioni 10 watamsaidia kwenye tuhuma zinazomkabili lakini hakuwa nazo akawapa sh milioni moja mbali na ushahidi huo hakuna ushahidi mwingine wa serikali unaoonyesha kuwa walipokea fedha hiyo. “Mahakama ilitegemea kuwe na ushahidi wa mawasiliano kama haupo wa kuona lakini hayo yote hayakufanyika,” alisema hakimu Moshi.

Muro alikamatwa ndani ya gari, mahakama haielewi ni kwanini kulikuwa na haraka hiyo kwanini asingeachwa wakakutana na Wage. Kwa upande wa hotel ya Sea Cliff ni sehemu ya watu yoyote anaweza kwenda. Washitakiwa Mgasa na Kapama hakimu Moshi alisema hawakukamatwa eneo la tukio walikamatwa na kuunganishwa na halikufanyika gwaride la kuwatambua na cheti kuletwa mahakamani.

Shitaka la linalowakabili Mgasa na Kapama la kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU mahakama ilisema halikuthibitishwa lina mashaka. Alisema washitakiwa walijitambulisha kwa moja anaitwa Dr na mwingine Musa.

Upande wa mashitaka ulitakiwa kufatilia mtaani kama majina hayo washitakiwa walikuwa wakiyatumia lakini hilo halikufanyika. “Wage kama msomi ngazi ya uhasibu aliwezaje kukubali mtu ajitambulishe kwa mdomo kama afisa wa TAKUKURU bila kuonyeshwa vitambulisho na akakubali mahakama inapata mashaka”. 

Aliongeza hakimu huyo hakuna vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha bila kuacha shaka hivyo wanaachiwa huru kwa mashitaka yote. Alisema Moshi risiti, pingu na miwani havikuwa na mgogoro katika kesi na kwavile vilipatikana kwa risiti basi arudishiwe muhusika na upande unataka kukata rufaa wana ruhusiwa. Wakili kiongozi wa kesi hiyo Boniface Stanslaus alisema taafifa atampelekea Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ataamua kama watakata rufaa.

Washitakiwa walifikishwa mahakamani Februari 5 mwaka jana kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu mkazi, Gabriel Mirumbe.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, November 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

independence night ndiyo mpango mzima desemba 2.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, November 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira akutana na balozi wa swedeni nchini leo jijini dar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Lennarth Hjelmaker kuhusu Masuala ya Mabadiliko ya Tabia Nchi na Mkutano utakaofanyika Durban Nchini Afrika kusini .[Pcha na Ali Meja]
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, November 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

UBWA SALUMU AJIFUA KUMKABILI MUSTAFA DOTO DESEMBA 25

Bondia Ubwa Salum (kushoto) na Omari Bayi wakioneshana umwamba wa kutupa masubwi wakati wa Mazoezi ya Kambi ya Ilala Dar es salaam jana Ubwa anajiandaa na mpambano wake na Mustafa Doto Desemba 25 mwaka huu (picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, November 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

mkuu wa mkoa wa pwani,Mwantumu Mahiza afungua mafunzo ya Afya ya Jamii CHF/TIKA KIBAHA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba, Mkurugenzi wa Hamashauri hiyo, Jenifa Omole na Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi  wa halmashauri hiyo, baada ya kufungua mafunzo hayo leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza (kulia) akiagana na  Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Hamis Mdee baada ya kufungua mafunzo kwa ajili ya uanzishaji wa  wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA), kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mjini Kibaha, leo. Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifa Omole.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza (kulia) akihutubia wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa ajili ya uanzishaji wa  wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA), kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mjini Kibaha, leo. Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifa Omole.
 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba akizungumza wakati wa kumkarisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza mafunzo hayo.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael, akijitambulisha wakati wa mkutano huo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee  (kushoto), akielezea umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA), wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa ajili ya uanzishaji wa Mfuko huo kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani leo.Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza  na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifa Omole.
 Diwani wa Kata ya Maili Moja, Kibaha, Andrew Lugano, akitoa shukrani baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, kufungua mafunzo hayo. 

Baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha wakiwemo madiwani, wakihudhuria mafunzo hayo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, November 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Makamu Wa Rais Aiwakilisha Tanzania Kwenye Mkutano Wa Wakuu Wa Nchi Za Afrika Mashariki

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania, nchini Burundi, Dkt. James Mwasi, baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliliana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Jan Ping, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Golf  kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akiwa katika Ukumbi wa Golf, wakati akimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifunga rasmi Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya kufunga Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, kwenye Ukumbi wa Golf, Bujumbura Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza (katikati) na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Jan Ping, wakisimama kwa heshima wakati ukipigwa wimbo maalum wa Afrika baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Golf kwa ajili ya kufunga rasmi Mkutano wa  Nchi za Maziwa Makuu, uliokuwa ukijadili Uendelezwaji wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika, uliomalizika jana Novemba 29, Bujumbura Burundi.
Picha  na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilish Tanzania katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika mjiniBujumbura, Burundi Novemba 29 - 30, 2011. Makamu wa Rais alifika mjini hapa jana ambapo aliwakuta Mawaziri kadhaa wa Tanzania waliotangulia kuhudhuria mikutano ya ngazi za Mawaziri wakiongozwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Manaibu Waziri Deo Mfutakamba, Lazaro Nyalandu na Adam Malima.
Katika mikutano ya awali katika ngazi ya Mawaziri, Tanzania ilijumuika na nchi nyingine za ukanda huu kutazama namna ya kusaini Protokali ya Ulinzi wa pamoja, protokali inayotaka nchi wanachama wa Jumuiya hii kushirikiana kijeshi pale inapokubalika ama inapoonekana kufaa baada ya nchi mwanachama kuwa katika hatari ya vita.
Hata hivyo mjadala huu ulikuwa ni mkali huku Tanzania ikitaka protokali hii isainiwe mara tu pale itakapokuwa na kipengele kinachobainisha kuwa, nchi wanachama watatakiwa kushirikiana ama kusaidiana baada ya kila nchi mwanachama kupima aina ya hatari na mchango wa hatari hiyo kwa nchi mshiriki ambaye ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Pia, mkutano huu ulikuwa na kazi ya kupitisha maelekezo ya wataalam yanayolenga kuongeza kasi ya kuundwa kwa shirikisho la Afrika Mashariki. Msimamo wa Tanzania katika agenda hii ni kuwa zoezi hili halijafikia muda muafaka na kwamba kuna mambo mengi yanayotakiwa kufanyika kabla ya Jumuiya hii kuunda shirikisho.
Hata hivyo nchi nyingine  za Afrika Mashariki zimekuwa zikishirikiana kwa lengo la kuongeza kasi na kuishinikiza Tanzania kukubali kuundwa kwa shirikisho, jambo ambalo linapingana na taratibu na kanuni za Jumuiya hii, zinazotokana maamuzi yote yafanyike kwa makubaliano yanayotoka kwa wananchi wa jumuiya hii na kwa kila taifa husika. Kwa mujibu wa ujumbe wa Tanzania, suala la shirikisho lilipingwa katika kamati ya Wangwe na hadi wakati Tume hiyo ilipokusanya maoni, hadi sasa hakujawa na tofauti ya mtazamo.
Tanzania inahitaji kufanyika kwanza maafikiano katika soko la pamoja na mataifa ya jumuiya hii kutazama namna yatakavyoweza kunufaika kabla ya kukimbilia ushirikiano wa kisiasa ambao kama utakimbiliwa bila mazingira kujengwa, ni rahisi kwa jumuiya hii kuvunjika kama ilivyowahi kufanyika huko nyuma.
Makamu wa Rais pia alikuwa na kazi ya kufunga mkutano wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukijadili mahusiano na uendelezaji wa Ukanda za Ziwa Tanganyika ambapo katika mkutano huo, alifafanua namna Tanzania inavyoshiriki kwa ukamilifu kuunganisha mikoa yake na nchi za mipakani hasa katika ujenzi wa barabara za lami, na namna ushirikiano kati ya nchi za SADC, EAC na COMESA unavyolenga kukuza biashara sambmba na uchumi kwa nchi wanachama.
Makamu wa Rais anarejea nyumbani kesho Desemba Mosi ambapo atakuwa na kazi ya ufunguzi wa barabara jijini Dar es Salaam Desemba pili, 2011. 
Imetolewa na: Idara ya Habari Ofisi ya Makamu wa Rais
                         Novemba 30, 2011
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, November 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Msondo, Sikinde kupambana Krismasi TCC

Bendi pizani za Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae)  

zitapambana siku  ya sikukuu ya Krismasi mwaka huu kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Temeke. Mpambano huo umeandaliwa na kampuni za Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi. Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la funga mwaka na kuamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka 2011.

Kapinga alisema ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa, hasa kwenye upangiliaji wa milio ya vyombo, kila bendi itatumia jukwaa lake kwa kupiga kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda jukwani.

“Litakuwa pamabano la aina yake ukizingatia kuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa bendi hizi pinzani kupambana siku ya sikukuu ya Krismasi tangu zianzishwe” alisema Kapinga.

“Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwao kushindana katika wilaya ya Temeke ambao ndiyo inaongoza kuwa na wapezi wao.” Kwa kawaida Msondo Ngoma hufanya maonyesho yao kila Jumamosi kwenye viwanja vya TCC Club, Chang’ombe wakati Sikinde hufanya maonyesho yao kwenye viwanja hivyo hivyo siku ya Jumapili.

Kapinga alisema kampuni yake inafanya mipango ya kuwasafirisha wapenzi wa bendi hizo kutoka mikoa ya karibu kuja Dar es Salaam kushuhudia mpambano huo ambao pamoja na kusherehekea sikukuu ya Krismasi pia utakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya kinywaji cha Konyagi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, November 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

NGOMA AFRICA BAND KUVAMIA MÜNCHEN JUMAMOSI 3 Dec 2011


FFU wa Ngoma Africa Band kutoa burudani ya kukata na Mundu
CD ya "50 Uhuru Anniversary" inatamba Redioni


Watanzania wanaoishi Ujerumani ! na Full Shangwe ya Miaka 50 ya Uhuru !
 Kuanzia München hadi Berlin  Chereko !Chereko !

Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) kuzinduliwa rasmi ! 10-12-2011 Berlin!

Watanzania waishio Ujerumani wameanza shamra shamra za kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara, kwa kasi kubwa inayotingisha kila kona,sherehe hizo zinaanzia mjini München siku ya 3 Dec 2011 ambapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya bidhaa za Tanzania,mavazi,na mdahalo rasmi na usiku kutakuwa na muziki wa Ngoma Africa Band  katika mtaa wa Siebold Str,11 ndipo penye ukumbi.

Kuanzia 9 hadi 10-Dec-2011 mjini Berlin ambako ndipo hupo Ubalozi wa Tanzania na ndio mji mkuu wa Ujerumani,kutakuwa hapatoshi kwani sherehe hizo zitaambatana na ufunguzi wa UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU) siku ya jumamosi 10-12-2011,umoja huo unawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani,ulitiliwa nguvu na balozi Mh.Ngemera, umeshasajiliwa na viongozi wake ni Bw.Mfundo Peter Mfundo(mwenyekiti) na Bi.Tullalumba Mloge (katibu),utaratibu unaonyesha kuwa sherehe hizo mjini Berlin zitaanza saa 9 mchana  hadi usiku usio kwisha ambapo Ngoma Africa Band aka FFU,watatumbuiza na muziki wao,mahala patakapo fanyika sherehe Apostelkirche 1, 10738 Berlin, 

UMOJA NI NGUVU WATANZANIA JITOKEZENI ! KUSHREKEA MIAKA 50 YA UHURU !
sikiliza muziki at www.ngoma-africa.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, November 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

RAIS KIKWETE ATIA SAINI MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2011

Tuesday, November 29, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho  Kikwete leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari
ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge
kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao
kilichopita cha Bunge.

Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu
katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na
Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi
Desemba 31, mwaka jana, 2010.

Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na
mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria
hiyo.

Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye
maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru
kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

*Imetolewa na*:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

*DAR ES SALAAM*.

29 Novemba, 2011
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0

waziri mkuu mizengo pinda azindua kiwanda kipya cha serengeti breweries mjini moshi leo.

Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda kipya cha bia cha Serengeti Breweries,mjini Moshi mkoani Kilimanjaro,huku viongozi waandamizi mbalimbali wa kampuni hiyo na wageni waalikwa wakiwemo wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakilishuhudia tukio hilo,lililofanyika mapema leo mchana.
Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa kiwanda kipya cha bia cha Serengeti Breweries,mjini Moshi mkoani Kilimanjaro,jioni ya leo,Wanaoshuhudia shoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilamanjaro,Mh Leonidas Gama,Waziri wa Nairobi Metropolitan,kutoka nchini Kenya,Mh.Njeru Githae,Mwenyekiti wa bodi ya SBL,Jaji Mark Boman sambamba na viongozi waandamizi mbalimbali wa kampuni hiyo na wageni waalikwa wakiwemo wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakilishuhudia tukio hilo,lililofanyika mapema leo mchana.
 Waziri Mkuu,Mh Pinda baada ya uzinduzi makofi ya furaha na shangwe yakatawala kama hivi pichani.
Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda pichani kati akipiga makofi mara baada ya ufunguzi wa kiwanda hicho,shoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa EABL,Seni Adetu,kulia ni Waziri wa Nairobi Metropolitan,kutoka nchini Kenya,Mh.Njeru  na wageni waalikwa mbalimbali wakishuhudia tukio hilo,lililofanyika jioni ya leo mjini Moshi,mkoani Kilimanjaro.
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa EABL,Seni Adetu akimuonyesha Waziri Mkuu,Mh Pinda chupa ya bia ya Serengeti,namna inavyotengenezwa kiwandani hapo,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Usambazaji,Bw.Mark Taylor sambamba na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa kiwanda hicho jioni ya leo.
Namna ya kinywaji cha Serengeti kinavyozalishwa na kupakiwa ndani ya chupa tayari kwenda kwa watumiaji.
Mkurugenzi wa Usambazaji,Bw.Mark Taylor akimuelekeza mgeni rasmi,Waziri Mkuu,Mh Pinda namna bia hiyo ya Serengeti inavyotengenezwa kiwandani hapo.
Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,wa pili kushoto,Mh Leonidas Gama wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wakuu wa kampuni ya SBL,wa pili kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Diane Corner
Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya SBL wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kiwanda hicho,uliofanyika jioni ya leo mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro.
Mgeni rasmi,Waziri Mkuu,Mh.Mizengo Pinda akipana mti kwenye moja ya viunga vya kampuni hiyo,ikiwa ni sehemu ya kielelezo cha utunzaji mazingira huku baadhi ya viongozi waandamizi wa kampuni hiyo na wageni waalikwa mbalimbali wakilishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Serengeti Breweries,Jaji Mark Boman akimkabidhi Wazir Mkuu ,Mh Mizengo Pinda zawadi,Shoto ni Waziri wa Kenya (Nairobi Metropolitan Development),Mh.Njeru Githae na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa EABL,Bw.Seni Adetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa EABL,Bw.Seni Adetu (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Kenya (Nairobi Metropolitan Development),Njeru Githae huku Waziri Mkuu Pinda (kulia) akishuhudia sambamba na Balozi wa Uingereza nchini,Mh Diane Corner.
Waziri Mkuu ambaye pia ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa kiwanda cha SBL,Mh Pinda akisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Waziri wa Kenya (Nairobi Metropolitan Development),Njeru Githae akisoma hotuba fupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali.
Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya SBL,Mh Jaji Mark Boman akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho,iliyofanyika jioni ya leo mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa EABL,Bw.Seni Adetu akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho,iliyofanyika jioni ya leo mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SBL,Bw.Richard Wells akitoa maneno machache ya shukurani kwa Mgeni rasmi,Waziri Mkuu Pinda pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha SBL,mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Mawasiliano/Mahusiano,Bi.Teddy Mapunda akimkaribisha Mgeni rasmi,Waziri Mkuu Pinda pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa kiwanda kipya cha SBL,mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mapema leo mchana.
Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria tukio hilo la uzinduzi wa kiwanda kipya cha SBL.
Baadhi ya Viongozi Waandamizi wa kampuni ya SBL,wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri meza kuu.
 Picha ya pamoja.
 Ziara imefanyika ya kutembelea kiwanda 


Waziri Mkuu,Mh Pinda ambaye ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi wa kiwanda hicho akipokelewa na wenyeji wake maraa baada ya kuwasili,shoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya SBL,Mh Mark Bomani na shoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh. Leonidas Gama. 
 Pyeeee pyeeeee......!!!
 Kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza wageni waalikwa.
Pichani ni sehemu ya kiwanda cha SBL-Moshi kikizinduliwa mapema leo mchana.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu