shirika la unfpa lasherehekea kilele cha dunia kufikisha watu bilioni 7,yatoa msaada wa vifaa mbalimbali hospitali ya temeke jijini dar leo.

Monday, October 31, 2011
Pichani shoto ni Muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr . Julitta Onabanjo akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo,kwenye hospitali ya Wilaya ya Temeke, jijini Dar Es Salaam,ambapo Dunia ilikuwa inatimiza idadi ya watu Billioni 7,anayetazama pichani kulia na Mama wa Mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kulwa Juma. 
Dr . Julitta Onabanjo akiwapa pole na hongera kwa akina mama wazazi waliojifungua usiku wa kuamkia leo,kwenye hospitali ya Temeke,ambapo Dunia ilikuwa inatimiza idadi ya Watu bilioni 7
Dr . Julitta Onabanjo akiwa na akina mama 7 waliojifungua usiku wa kuamkia leo,ambapo kupitia shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania lilitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa akina mama hao ikiwemo pia hospitali  hiyo kwa kupatiwa vifaa mbalimbali vya watoto.
Mgeni rasmi,ambaye pia ni muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo akiwa ameambatana na wenyeji wake wakiwa kwenye wodi ya Wanawake kwa ajili ya kutoa misaada kwa akina mama saba walijifungua usiku wa kuamkia leo,ambapo Dunia ilikuwa inatimiza idadi ya watu bilioni saba,na Tanzania ilikuwa inatimiza idadi ya watu bilioni 44.
 Mgeni rasmi pichani kati akiwa na wenyeji wake wakielekea kwenye wodi ya akina mama wazazi,kwa minajili ya kutoa msaada kwa wazazi saba waliojifungua watoto,ambapo dunia ilikuwa ikitimiza idadi ya watu bilioni 7.
 Mgeni rasmi,muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo akikabdhi sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na shirika hilo kwa Mganga mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dr. Sylvia Mamkwe,, mapema leo asubuhi kwa ajili ya hospitali hiyo.
Pichani Dr. Husna Msangi kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Temeke Hospitali jijini Dar,akimkabidhi hotuba fupi aliyokuwa akiisoma mbele ya Mgeni rasmi,ambaye ni muwakilishi wa UNFPA-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo kwenye hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya hospitali hiyo,iliyofanyika mapema leo asubuhi,ambapo Dunia ilikuwa ikitimiza idadi ya watu bilioni 7.
Muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr . Julitta Onabanjo akifafanua jambo mapema leo asubuhi wakati hafla fupi ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa hospitali ya Temeke.
Pichani Dr. Husna Msangi kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Temeke Hospitali jijini Dar,akisoma hotuba fupi mbele ya Mgeni rasmi,ambaye ni muwakilishi wa UNFPA-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo na wageni wengine waalikwa  mbalimbali waliokuwa wamefika (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya hospitali hiyo,iliyofanyika mapema leo asubuhi,ambapo Dunia ilikuwa ikitimiza idadi ya watu bilioni 7.
 Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla hiyo.

 
Mganga mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dr. Sylvia Mamkwe akiwakaribisha wageni waliofika katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, kutoka kulia ni Dr. John Bwana- Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dr. Heavengton Mshiu-MOHSWI RCH (Programe Officer- Safe Motherhood International), Muwakilishi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania, Dr. Julitta Onabanjo pamoja na Dokta bingwa wa watoto- Temeke hospitali Dr. Solanki Rajeshi.
Pichani ni baadhi ya misaada mbalimbali iliyotolewa na shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania kwa hospitali ya Temeke.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na gogoro la simba sc.

                        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KATIKA baadhi ya vyombo vya habari jana na leo, kumeripotiwa taarifa za kuwapo kwa ugomvi baina ya wachezaji wawili wa Simba, Emmanuel Arnold Okwi na Haruna Moshi Shaaban (Boban). Ugomvi huo umeripotiwa kutokea mara baada ya pambano la watani wa jadi lililofanyika jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Vyombo hivyo viliripoti kuwa chanzo cha ugomvi huo ni madai ya hujuma na kutoaminiana ndani ya timu. Kwa masikitiko makubwa, Simba Sports Club (SSC) inapenda kukanusha kwa nguvu zote kuwapo kwa ugomvi wa aina yoyote baina ya wachezaji au viongozi wa klabu mara baada ya pambano la jana.

Mara baada ya mechi, hali iliyotamalaki ilikuwa ni ya fadhaa na huzuni kwa wote wanaohusika na Simba, wakiwamo wachezaji na washabiki. Habari hizo za ugomvi wa wachezaji ni uzushi unaoenezwa na watu wasioitakia mema SSC.

Kuna mambo mawili yanayoweza kubainisha kuwa habari hizo hazikuwa za ukweli. Kwanza, kwamba vipo vyombo vilivyodai kuwa Okwi alipigwa hadi kuvimba uso. Ukweli ni kuwa Okwi yuko salama, buheri wa afya na hajavimba popote mwilini mwake, achilia mbali usoni.

Pili, kuna magazeti yaliyoandika kuwa Okwi alipigwa vichwa vinne Boban kabla hawajaamuliwa. Mengine yakaripoti kichwa kimoja. Kuna redio imeripoti kuwa vilikuwa vichwa vitatu. Tukio moja, taarifa tofauti lukuki. Kikubwa ni kuwa, hakuna mwandishi wa habari hata mmoja aliyeshuhudia tukio hilo na kulithibitisha pasi na shaka zaidi ya kusimuliwa na wale waeneza uongo.

SSC inashukuru kwa ushirikiano mzuri inaopata kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje. Tunawaomba wana Simba wawe watulivu katika kipindi hiki na tujipange kwa ajili ya mechi yetu ijayo ya VPL dhidi ya Moro United. Kama tutashinda, tutaongoza ligi hadi mwakani.

Timu inarejea kambini leo tayari kujiandaa na pambano hilo la mwisho la raundi ya kwanza ya VPL.

Ezekiel Kamwaga
Msemaji
SSC

 
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Vodacom yawekeza milioni 90 kwa shule 20 za msingi mkoa wa Dar es Salaam.

Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi msaada wa madawati Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwongozo  Elly Shuma  kwa niaba ya walimu wenzake wa shule tano zilizonufaika na msaada huo wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni shirini na ishirini na tano elf(20,25,000)kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimsisitiza jambo Mwanafunzi wa  Shule ya Msingi Mwongozo  darasa la kwanza Sara Uhuru  mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni ishirini na ishirini na tano elf(20,25,000)kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwongozo iliyopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dares Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 20,25,000,kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwongozo iliyopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dares Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 20,25,000,kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
 
===============   ========  ===============

Vodacom yawekeza milioni 90 kwa shule 20 za msingi mkoa wa Dar es Salaam.

*       Leo Vodacom Foundation imekamilisha kwa kutoa madawati 225 kwa shule 5 za Wilaya Ilala na Kinondoni ikiwa ni zoezi lililoanza mwezi wa nne la kutoa msaada wa madawati 1000 katika Mkoa wa Dar es salaam.

Tatizo la uhaba wa madawati katika shule mbalimbali za msingi hapa nchini ambalo limekuwa kwa namna moja ama nyingine likichangia kukosekana kwa mazingira dhabiti mashuleni linazidi kupata msukumo wa kutatuliwa kutoka kwa taasisi na mashirika binafsi nchini. Moja ya mashirika hayo ni mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambao leo umekabidhi madawati mia mbili na ishirini na tano yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na ishirini na tano elf,ikiwa ni utekelezaji wa muendelezo wa utoaji wa madawati katika shule za msingi za  mkoa wa Dar es salaam.

 Akizungumzia mradi huo Afisa Mkuu wa masoko na uhusiano wa kampuni hiyo Bi. Mwamvita Makamba  amesema mradi huo ni sehemu ya kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wa kitanzania kama nyenzo muhimu ya kuwajengea mazingira bora ya kuja kujisaidia katika maisha yao na kulisadia pia taifa katika fani  mbalimbali.

Vodacom Foundation imekuwa ikiweka mkazo kusaidia sekta ya elimu kama eneo muhimu la kuchangia nguvu na juhudi za serikali katika ustawi wa jamii nchini, hii ni awamu ya pili kwa mwaka huu na ni imani ya Vodacom kwamba madawati hayo yatapunguza uhaba katika shule ambazo zitaguswa.
 
  "Tunatambua ukubwa wa tatizo na kwamba lipo takribani nchi nzima na tunaguswa nalo kama kampuni yenye kujali maisha ya watanzania na ndio maana kila mwaka tumekuwa tukiendesha kampeni maalum ya kuchangia madawati ni imani yetu kwamba ipo siku changamoto hii itabakia kuwa historia"Aliongeza Mwamvita Amesema ukosefu wa madawati nchini ni changamoto ambayo dhahiri ahitaji kufumbiwa macho wala kuzibiwa masikio inahitaji nguvu za pamoja za kila wadau ili kuwawezesha wanafunzi ambao ndio nguvu kazi ijayo ya taifa kuwa na mazingira bora, salama na kuwawezesha kufanya vema katika masomo yao.

"Inaumiza sana unapoona watoto wameketi sakafuni au kubanana katika dawati moja darasani, hii lazima itapunguza uwezo wao wa uelewa na ufuatiliaji masomo darasani ndio maana tukaamua kama kampuni inayoungwa mkono na watanzania kuonesha upendo wetu kwa kuwa na kampeni kabambe ya kusaidia madawati mashuleni"Amesema Afisa Mkuu wa  Masoko na uhusiano wa Vodacom. Awamu hii imenufaisha shule za msingi tano ambazo ni Maarifa shule ya Msingi (Ilala) Kombo shule ya Msingi (Ilala) Vingunguti Shule ya Msingi (Ilala) Mwongozo Shule ya Msingi (Kinondoni) Kimara B Shule ya Msingi (Kinondoni).


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

BLANDINA NYONI AFUNGA KONGAMANO LA WANAHABARI LA BIMA YA AFYA MORGORO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni  (kushoto) akihutubia alipokuwa akifunga kongamano la wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu taarifa za tafiti za upatikanaji  wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya   (NHIF) nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika mjini Morogoro.
Mganga Mkuu wa Serikali, Mtasiwa akifafanua mambo mbali mbalimbali kuhusu masuala ya dawa na tiba.
 Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Lauden Mwambona akiongoza  mijadala ya tafiti hizo. Kutoka kushoto ni Benny Mwaipaja wa TBC  Manyara na Saiboko wa Daily News.
Cosmas Nadimi wa MSD, akijibu maswali mbalimbali ya wanahabari  kuhusu usambazaji wa dawa nchini
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akitoa majumuisho ya  mapendekezo yaliyotolewa na wadau kwenye kongamano hilo.

 Blandina Nyoni akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Clement Mshana (kulia) pamoja na Mhariri  Mtendaji wa New Habari, Deodatus Balile. .
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni  (kushoto) akizungumza na wanahabari baada ya kufunga kongamano la  wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu taarifa za tafiti za  upatikanaji wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima  ya Afya (NHIF) nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika mjini  Morogoro.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika kongamano hilo mjini Moro.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

rais wa zanzibar,Dr Shein azindua tawi la benki ya wananchi wa zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Chake chake Pemba wakati wa uzinduzi wa tawi la benki ya wananchi wa Zanzibar PBZ, Pemba,ambapo huduma ya ATM pia itapatikana kwa saa 24.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Kaimu Waziri wa Fedha Dk Mwinyihaji Makame,akitoa nasaha kwa wananchi na kuwataka kuweka fedha zao katika benki ya watu wa Zanzibar tawi la Chake chake leo,wakati wa uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akitoa pesa kutoka huduma ya ATM mara baada ya kulizindua  Tawi jipyala PBZ huko Chake chake,Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akionesha pesa alizotoa kupitia matandao wa ATM kwa benki ya watu wa Zanzibar PBZ,baada ya kuzindua rasmi tawi jipya la chake chake Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akitoa pesa kutoka huduma ya ATM mara baada ya kulizindua  Tawi jipyala PBZ huko Chake chake,Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akitia saini fomu za kuweza kupatiwa ATM card ya kutolea pesa katika Benki ya watu wa Zanzibar katika sehemu lilipo tawi la Benki hiyo,wakati wa uzinduzi wa tawila PBZ Chake chake Pemba jana,(kushoto) Mkurugenzi mtendaji Juma Amour.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benki ya watu wa Zanzibar PBZ Juma Amour,wakati wa sherehe za uzindu wa   Tawi jipyala PBZ huko Chake chake,Mkoa wa Kusini Pemba.
Baadhi ya waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la Benki ya watu wa Zanzibar PBZ,wilaya ya Chake chake Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi katika sherehe za uzinduzi wa tawi hilo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wasoma utenzi wakati wa uzinduzi rasmi w2a tawi la PBZ leo huko Chake chake Pemba.Picha na Ramadhan Othman Pemba.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

SIKU YA KWANZA YA CLINIKI YA SOKA YA AIRTEL RISING STAR UWANJA WA TAIFA VIJANA WAKIFULIWA

 Kocha wa soka ya vijana kutoka Manchester United, Paul Bright akionyesha kwa vitendo namna ya kusakata kabumbu wakati wa mafunzo ya kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana ya 'Airtel Rising Stars' yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Katikati ni Graham Naftali na Samir Omary (kulia).
 Mshiriki wa kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, Naomi Njeri akimtoka mshiriki mwenzake Emily Auma wakati wa mafunzo ya kliniki hiyo yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi mkuu wa kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana ya 'Airtel rising Stars', Billy Miller kutoka klabu ya manchester United ya Uingereza, akijadili jambo na kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Vijana ya Tanzania, Kim Poulsen, wakati wa mafunzo hayo yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

gazeri lako mahiri kwa habari za uchambuzi wa kina,dira liko mitaani sasa kwa sh 500/=

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

francis miyayusho bingwa mpya wa ubo,amchakaza vilivyo mbwana matumla.

Bingwa Mpya wa UBO katika uzito wa Bantum,Francis Miyeyusho akifurahia ubingwa wake huo wakati akivishwa mkanda wake na Mlezi wa Mchezo wa Ngumi hapa nchini,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Afande Suleiman Kova huku Diwani wa Kinondoni,Mh. Abbas Tarimba akiangalia.Francis Miyeyusho kanyakuwa ubingwa huo baada ya kumchakaza vibaya Bingwa wa Zamani UBO,Mbwana Matumla katika mchezo uliomalizika jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubile,jijini Dar.
Bondia Francis Miyeyusho akimrushia konde zito mpinzani wake,Mbwana Matumla wakati wa mchezo wao uliomalizika jana usiku katika ukumbi wa Diamond Jubilee .Francis Miyeyusho kanyakua ubingwa katika mchezo huo kwa kumshinda Mbwana Matumla kwa point.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Matukio mbali mbali ya Safari Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel katika kuelekia Fainali za mrembo wa Dunia.

Hapa Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa kwanza kushoto akiwa katika Vazi la Ufukweni na Wenzake katika maonesho ya Mavazi hayo hapo jana.
 Miss Vodacom Tanzia 2011 Salha Israel  aliye vaa Nguo za Njano katika Mazoezi  ya nguvu kabisa wakati wa maandalizi ya shindano la Miss World Tanzania
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Kumi kutoka kulia akiwa na wenzake katika Dina la nguvu Huko Scottish maeneo ya Scottish Hydro.
 Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa pili kutoka kulia akiwa Edinburgh Castle hivi karibuni katika safari ya kuelekea katika mashindano ya kumsaka Mrembo wa Dunia.
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Pili kutoka kulia akiwa anapiga Chiazi  na wenzake .. katika safari  ya kuelekea kumtafuta Mrembo wa Dunia.
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Tatu  kutoka kulia akifurahia kwa Shangwe wakati wa  Highland Games kuelekea kinyang'anyiro cha Mrembo wa Dunia.
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa kwanza kushoto aliye simama akiwa katika picha ya pamoja na wenzake .Kwa picha zaidi Tembelea:  www.fredynjeje.blogspot.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, October 31, 2011 | | Permalink | Maoni 1
Idadi ya watu