WAWEKEZAJI KUTOKA RUSSIA WAKUTANA NA WAZIRI MKUU jijini dar leo

Friday, September 30, 2011
Hapa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mmoja wa wafanyabiashara wawekezaji kutoka Russia walipomtembelea ofisini kwake leo.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wawekezaji toka Russia ambao wanakusudia kuwekeza nchini katika sekta ya madini na gesi Ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 30,2011.(Picha na OFisi ya Waziri Mkuu).
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

wanamuziki watakaotumbuiza tusker all stars 2011 watamba kulitikisa jiji la nairobi hapo kesho ndani ya carnivo grounds.


Eve E akiwa amepozi kiaina.
wwwoooooowww..! I cant believe it...Eve..!
Msanii Alpha akitimiza moja ya ndoto zake  katika anga ya muziki.
Waratibu na wadhamini wakiwa katika picha pamoja na wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011,kwenye viwanja vya Carnivo hapo kesho,tamasha hilo linatarajiwa kuanza mapema mnamo saa nane mchana  na kuendelea,aidha ndani ya tamasha hilo mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 haruhusiwi.
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya EABL-Kenya ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Tusker All Stars,kupitia kinywaji chao cha Tusker akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo ndani ya moja ya ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena akiwa na wanamuziki wote ambao watatumbuiza kwenye tamasha hilo,ambalo limekuwa na msisimko mkubwa hapa jijini Nairobi.
Mwanamuziki Shaggy akifafanua jambo mbele  ya Wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na tamasha la Tusker All Stars 2011,kulia kwake ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya EABL-Kenya ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia kinywaji chao cha Tusker.
Baadhi ya wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011 wakiwa kwenye mkutano na wanahabari ndani ya Serena hotel kuhusiana na tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Carnivo,jijini Nairobi.Shoto ni Msanii Amani,Jaguar pamoja na Alpha.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Entertainment,Ruge Mutahaba pichani kulia akizungumza jambo na Shaggy leo mchana nje ya hoteli ya Kimataifa,Serena,jijini Nairobi.
Mwanamuziki kutoka nchini Jamaica,anaefanya kazi zake za kimuziki nchini Marekani,Orville Richard Burrell a.k.a Shaggy akiwa amepozi mara baada ya kutia saini bango lenye tangazo la kampeni mpya ya East African Breweries Ltd, iliozinduliwa hivi karibuni kwa ajili ya kuielimisha jamii kuhusiana na suala la ulevi wa kupindukia ijulikanayo kama "Unywaji pombe kistaarabu" ama " RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN"
Mwanamuziki nyota kutoka nchini Marekani,Eve Jihan Jeffers a.k.a Eve E akitia saini kwenye bango lenye tangazo la kampeni mpya ya East African Breweries Ltd,iitwayo "Unywaji pombe kistaarabu" ama " RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN"
Msanii kutoka nchini Angola,Ivon Manuel Lemu a.k.a Cabo Snoop, akitia saini kwenye bango lenye tangazo la kampeni mpya ya East African Breweries Ltd,iitwayo "Unywaji pombe kistaarabu" ama " RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN"
Msanii mmojawapo wa Tusker All Stars 2011 akitia saini kwenye bango lenye tangazo la kampeni mpya ya East African Breweries Ltd,iitwayo "Unywaji pombe kistaarabu" ama " RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN"
Paparazi wakiwa kazini  kunasa tukio hilo leo mchana,pichani Mwanamuziki akiwa ndani ya Tax.
Baadhi ya wanamuziki waliojitokeza kuunga mkono kampeni mpya ya EABL-Kenya ( RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN),wakiwa wamepozi picha pamoja kwenye baadhi ya Tax zenye kuhamasisha kampeni hiyo jijini Nairobi,kulia ni Davies,Eve E,Peter Msechu,Cabo Snoop pamoja na Shaggy.
Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya EABL akitoa maelekezo mafupi kwa Wanaumuziki namna kushiriki ama kuunga mkono kampeni mpya ya kupambana na suala zima la ulevi kupindukia.
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa EABL-Kenya,Caroline Ndungu sambamba na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa na wanamuziki watakaotumbuiza kesho kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011,wakitoka nje ya hoteli ya Serena,iliopo katikati ya jiji la Nairobi,Kenya mapema leo mchana kwa ajili ya kuunga mkono kampeni mpya ya Unywaji pombe kistaarabu " RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN",ambayo nchini Tanzania ilizinduliwa hivi karibuni (kwa picha ya tukio hilo bofya hapa).
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

rais wa zanzibar dr shein akutana na balozi wa italy nchini Tanzania.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Italy nchini Tanzania Peirliugi Velardi,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar.(30/09/2011)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Italy nchini Tanzania Peirliugi Velardi,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar.(30/09/2011) .Picha na Ramadhan Othman IKulu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Ajali ya moto Mbeya, Exim waanza kuwawezesha Wanawake

Na Ripota Wetu, Mbeya

BENKI ya Exim (T) Ltd, kupitia programu ya uwezeshaji kwa wanawake (WEF), inatarajia kuwawezesha takribani wanawake 300 waliounguliwa na vibanda vyao vya biashara katika soko la Sido la jijini Mbeya, kwa kuwapatia sehemu ya mtaji kwa ajili ya kurejesha biashara zao katika hali ya kawaida.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Programu hiyo Felister Simba alipokutana na kina mama zaidi ya 500 walipofanya ziara ya kuwapa pole waathiriwa wa ajali hiyo iliyotokea wiki mbili zilizopita na kuteketeza soko hilo lililoko eneo la Mwanjelwa jijini hapa. 

Akizungumza na kina mama hao Simba alisema kuwa benki hiyo iliguswa na tukio hilo na ndio maana ikafikia uamuzi wa kuwasaidia waathirika hao ikianza kwanza na kina mama, ambapo alisema kuwa msaada wa benki hiyo utakuwa katika makundi mawili.

“Uongozi wa Exim kwa ujumla umeguswa na tukio hili na tunajua ni kiasi gani limeathiri shughuli za kiuchumi katika mji wa Mbeya na ndio sababu tumeona umuhimu wa kushirikiana nanyi katika kuona shughuli zenu zinarejea katika hali ya kawaida kwa kuwawezesha kina mama kwanza japo kwa kiasi kidogo ambacho tumejaaliwa” alisema meneja huyo wa WEF.

Akifafanua zaidi kuhusu msaada huo, Meneja Msaidizi wa Masoko wa benki hiyo Anita Goshashy alisema kuwa benki yao itawafungulia kina mama hao akaunti maalum za Tumaini na kuwawekea kila mmoja kiasi cha shilingi 50,000/= akaunti ambazo zitawawezesha kukopeshwa na benki hiyo baada ya muda mfupi.
Alisema masharti ya huduma za mikopo za benki hiyo kwa walengwa hao yamelegezwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hao wanajikwamua na kurejesha shughuli zao za kibiashara katika hali ya kawaida.

Aliongeza kuwa mbali ya kundi hili la kina mama ambao ni wajasiriamali wadogo wadogo, kundi jingine la kina mama litakalokuwa katika mpango wa kuwezeshwa ni lile la wajasiriamali wa kati na wa juu ambao wana uhitaji wa mikopo mikubwa Simba alisema kuwa watakutana nao kwa ajili ya kusikiliza vilio vyao na kisha kuangalia namna ya kuwawezesha kwa masharti nafuu, lengo likiwa ni kuwezesha shughuli za kiuchumi kwa ujumla kurejea katika hali ya awali.

“Tunaamini kuwa kwa kuanzia na akina mama, kidogo kidogo tutaweza kufanikisha mpango wa kurejesha shughuli za kiuchumi katika jiji la Mbeya kwenye hali ya kawaida kama ilivyokuwa awali kabla ya ajali ya moto” alisisitiza.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Bw. Evance Balama, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, aliwaasa wafanyibiashara hao kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano wa dhati na benki ya Exim ili kufanikisha mpango wa benki hiyo wa kuwezesha urejeshwaji wa shughuli mbalimbali katika soko hilo kwenye hali yake ya awali.

“Tuthamini mchango wa wenzetu wa Exim katika kulia pamoja nasi, tusitumie kipindi na msaada huu kwa malengo yasiyokuwa mahususi kwani hili litafanya juhudi za pamoja baina ya Exim, uongozi wa mkoa na ule wa soko, kutokuzaa matunda yaliyokusudiwa ambayo ni kuurejesha mji wetu katika hali ya kawaida kibiashara” alisema mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa akimuwakilisha mkuu wa mkoa Bw. Abass Kandoro.
Balama, aliushukuru uongozi wa benki ya Exim kwa kuonyesha kuguswa kwao na tukio hilo na kuwaomba kuendelea kuwa karibu na wananchi kila nyakati kwani wananchi hao ndio nguvu ya ukuaji wao, na akazitaka taasisi zingine mbalimbali nchini kuiga mfano wa Exim katika kushirikiana na wananchi wanapokuwa wamekumbwa na majanga mbalimbali.

Kwa upande wao, akina mama wanaofanya biashara katika soko hilo ambao hivi sasa wako kwenye pilika pilika za kujenga upya vibanda vyao, kupitia kwa mwakilishi wao Asina Nyigu, waliishukuru benki ya Exim kwa msaada huo na kuahidi kushirikiana nayo bega kwa bega ili kuhakikisha jiji la Mbeya linasonga mbele kiuchumi.

Huu ni msaada wa pili kutolewa na benki hiyo katika kipindi cha mwezi mmoja ambapo mwanzoni mwa mwezi walitoa msaada kwa waathirika wa ajali ya meli ya MV. Spice Islander, iliyotokea Zanzibar na kusababisha vifo vya mamia ya Watanzania.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

mwanamuziki eve e awasili asuhi hii jijini Nairobi,tayari kwa tusker all stars 2011 concert.

  Mwanamuziki Eve E akiwasili kwenye hotel ya Kimataifa,Serena Hotel asubuhi hii .
 Mwanamuziki Eve E akiwasili kwenye hotel ya Kimataifa,Serena Hotel asubuhi hii .
Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Eve E akiwasili mapema leo asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta,jijini Nairobi,Kenya akiwa amepokelewa na mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd  kutoka Tanzania,Bwana Balozi Kindamba (shoto) na kulia ni mmoja wa wanausalama wa Eve E,Ujio wa Mwanamuziki huyo anaungana na wanamuziki wengine akiwemo Shaggy,Cabo Snoop pamoja na nyota wa Tusker All Stars Peter Msechu,Davis pamoja na Alpha wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye jukwaa moja hapo kesho (jumamosi) kwenye viwanja vya Carnivo jijini Nairobi ndani ya tamasha la Tusker All Stars 2011.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

ndani ya jiji la Nairobi asubuhi hii.

Pichani ni mtungo wa foleni ndan ya jiji la Nairobi asubuhi hii,Kiukweli mtungo wa jiji la Dar tuuvumilie hivyo hivyo,una unafuu mkubwa sana ukilinganisha na hapa jijini Nairobi,mtungo muda wote,wakati huko Dar angalau foleni ina muwa wake.Nairobee ni balaaaa...!
Fujo kama kawa kwa road.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

BongoFlavalink sasa kuitwa BongoFlavaMusic (BFM)

 
Tunaomba msamaa kwa wadau kwa siku hizi mbili kwa kutokutuelewa katika blog yetu.Ni kutokana na mabadiliko ya blog na jina pia.Kwa sasa blog hiyo itakuwa inaitwa BONGO FLAVA MUSIC kutoka jina la BONGO FLAVA LINK hadi jina jipya, Ila link itabaki vilevile. http://bongoflavalink.blogspot.com/ Ukiwa na habari,Tangazo au nyimbo mpya tuma kupitia mail hii: salimmore@yahoo.com ua wasiliana nami kuhusu matangoza: +255 712 222244
Ahsante kwa ushirikiano wako nami.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

House For Rent: Mbezi Beach, Kinondoni - DAR ES SALAAM

Features

Property Code : PROP_149
Price: USD 3,500
Listing Type : For Rent
Bedrooms : 9
Bathrooms : 6
Car Parking : YES
Fence: YES
 
Habari zaidi Bofya Hapa
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 1

USIKU WA RUSHA ROHO UKISINDIKIZWA NA OFFSIDE TRICK JUMAMOSI HII YA 1/10/2011 NDANI YA MJI WA READING SHOW YA MWISHO KWA UK WOTE MNAKARIBISHWA...

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

BLIND TIGER TO SERVE (BEER) COCKTAILS AT THE KILIMANJARO BEER FEST THIS WEEKEND!!


BLIND TIGER TO SERVE (BEER) COCKTAILS AT THE KILIMANJARO BEER FEST THIS WEEKEND!!

Ever tried a beer cocktail??? You'd be suprised!! Come and try the world's most humble beverage in a truely innovative fashion at the very first Oktoberfest to hit Tanzania this weekend!

However, fear not - Blind Tiger will also be serving fruity frozen cocktails, cooling classics and other heavenly delights to offset the beer blitz that will be the Kilimanjaro Beer Fest, and provide a more refined drinking experience for those less inclined towards the amber brew! The Blind Tiger menu would of course be incomplete without tasty mocktails, exciting shooters, and an array of Bacardi Breezer flavours!

Come and find the Blind Tiger tent, from 10am this Saturday the 1st of October to late on Sunday 2nd October at Leaders' Club, Kinondoni.

Karibuni sana!

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

NIGERIAN MUSIC STARS JOIN CAST OF MTV SHUGA

NIGERIAN MUSIC STARS JOIN CAST OF
SHUGA: LOVE , SEX, MONEY ON LOCATION IN NAIROBI

Nairobi, 27 September 2011: Nigerian musicians Banky W and Wiz Kid jetted into Kenya this week to appear in Shuga: Love, Sex, Money, the critically acclaimed sex-and- relationships TV series brought to you by MTV Base, The Staying Alive Foundation, the U.S. President's Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) and The Partnership for an HIV-Free Generation.

Banky W and Wiz Kid will both play themselves in the series, performing during emotionally hard-hitting club scenes shot at luxury Nairobi hangout, Skylux Lounge.   Nigerian viewers will get the chance to see Wiz Kid and Banky W in action from 14 February 2012 when Shuga: Love; Sex; Money premieres on MTV channels around the world.

Joining Banky W and Wiz Kid in the series will be Kenyan singer Avril (Miss B’have) and cast members Sharon Olago (Violet), David Omwange (Skola), Nick Mutuma (Leo), Antony Mwangi (Kennedy) and Valerie Kimani (Sindi), Nick Ndeda (Angelo), Nancy Wanjiku (Baby), Brenda Wairimu (Dala), Edward Nyanaro (Rayban), Ikubese Emmanuel - a.k.a. 9con - (Femi), Christopher Otieno (Slim) and Wairugi Mutero (Njoki). 

Shuga: Love; Sex; Money is directed by South African veteran director Teboho Mahlatsi and Lupita Nyong’o, who played the pivotal character of Ayira in the first series of Shuga. Nyong’o, an award-winning documentary maker and actress, returns on the other side of the camera as co-director and will also be making a brief cameo appearance in the series.

The first series of Shuga was filmed in Kenya in August-September 2009.  Starring a young cast of upcoming Kenyan actors and actresses, Shuga told a bitter-sweet tale of love, loss, sex, heartbreak and relationships, set in the clubs, bars, campuses and hangouts of contemporary Nairobi. With a raw and uncut view on the lives of sexually active young Kenyans, Shuga spot lit the risks associated with unprotected sex and the party-hard lifestyles of urban Kenyan youth, told through the interlinked characters and storylines.

Read more »
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Friday, September 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

CABO, SHAGGY, ALPHA, MSECHU AND DAVIS PLANT TREES AT KARURA

Thursday, September 29, 2011
The Tusker All Stars prime guests Shaggy and Cabo Snoop and icons Msechu, Alpha and Davies, today joined the East African Breweries Ltd E-Green Team at the Karura Forest for a tree planting session as part of Karura Forest Conservation efforts. 

The Stars, who are in Kenya for East Africa’s biggest musical fete, the Tusker All Stars Concert, planted a selection of various indigenous trees and took time off to enjoy serenity and bond with nature at one of the country’s most famous conservation names. 

Speaking during the tree planting event, EABL’s Marketing Director, Kenya, Caroline Ndungu said, “Environmental conservation, as one of the EABL Foundation key pillars, is not only an initiative that we invest a lot of resources into but also a calling that is deeply embedded in our corporate social responsibility mission,” “Bringing the Tusker All Stars to Karura Forest, one of our country’s greatest environmental assets, therefore gives them the crucial and memorable opportunity in lending a hand in its conservation.” She added.

Adding his voice during the exercise, American musician, Shaggy said he was excited to be part of the initiative.”Sustaining the environment is an obvious concern across the world and as responsible global citizens, each one of us has a responsibility to play in ensuring that we do all it takes to conserve the planet for future generations,” Shaggy said. “I thank EABL for giving us the opportunity to join them in this very symbolic and historical initiative,”
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, September 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Rais Kikwete Apokea Msaada Wa Millioni 25 Kutoka Kanisa la The Synagogue Church Of All Nations kwaajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Island iliyozama kisiwani pemba.

Mwakilishi wa Emmanuel Televisheni na Kanisa la The Synagogue Church Of All Nations Bi. Martha Harvey akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jumla ya shilingi milioni ishirini na tano 25,000,000/- kwaajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Island iliyozama katika mkondo wa Nungwi huko Unguja na kusababisha vifo vya watu wengi hivi karibuni.mchango huo uliokabidhiwa leo ikulu jijini Dar es Salaam umetolewa na Kiongozi wa Kanisa hilo Nabii Themitope Balogun Joshua ambaye anaishi katika Makao makuu ya Kanisa hilo jijini Lagos Nigeria.Picha na Freddy Maro-IKULU
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, September 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Kaseba na Mtambo wa Gongo wakumbushwa kufuata sheria


Mabondia Japhert Kaseba (kushoto) na Maneno Osward wakitunishiana misuri walipokutana, Dar es salaam leo kukumbushwa sheria mbalimbali zitakazotumika katika mpambano wao utakaofanyika jumamosi hii katikati ni Katibu, wa Chama cha mchezo wa ngumi kinachosimamia mpambano huo. PST. Anton Lutta. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, September 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Tusker All Stars 2011 yazidi kupamba moto ndani ya jiji la nairobi.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group/Prime Promotions Ltd,Joseph Kusaga akibadilishana mawazo na crew ya Shaggy leo,wakati wa zoezi la upandaji miti kwenye msitu wa hifadhi ya miti,Karura Forest ilioko nje kidogo ya jiji la Nairobi,Kenya.
Mwanamuziki kutoka  nchini Marekani,Shaggy akiwa amepozi na Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya East African Breweries Ltd,Caroline Ndungu.
Shaggy na Cabo Snoop.
Shaggy na Alpha.
Alpha na Peter Msechu.
Shaggy na Mdau kutoka EABL.
kwa pamoja wakishoo love.
Cabo Snoop na mdau wake.
wwooowww....!
Shaggy na shabiki wake.
Pichani ni Wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011,linalotarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Carnivo,jijini Nairobi mnamo Oktoba 1.Kulia ni Davis,Alpha,Shaggy,Peter Msechu,pamoja na Cabo Snoop.kama vile haitoshi msanii mwingine wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Eve E ambaye anatarajiwa kuwasili usiku wa leo ndani ya jiji la Nairobi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, September 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0

nafasi za kazi

MAMBO  MEDIA  CENTRE
Mambo  Media  Centre  ni  kampuni  mpya  inayojishughulisha  na  masuala  ya   utoaji  wa  habari  mbalimbali, kuanzia  habari  za   michezo, burudani, siasa, uchumi  hadi  habari  za  uchunguzi..  Tunatangaza  nafasi  za  kazi   ya  uandishi, utafutaji  na  usomaji  habari  kwa  waombaji  wenye  sifa  zifuatazo.

1. Umri  miaka  18  hadi  30.
2. Awe na  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne, sita  na  kuendelea.
3. Akiwa  na  elimu  ya  ziada  inayohusiana  na  masuala  ya  habari, itakuwa  ni  added  advantage  kwake.
4..Awe  na  uwezo  wa  kuzungumza  na  kuandika  kwa  ufasaha  lugha  za  kiswahili  na  kiingereza.
5. Awe  maridadi, mtanashati  na  anayejiamini..
6. Awe  tayari  kufanya  kazi  katika  mazingira  magumu.

Usaili, utafanyika   tarehe   05.OKTOBA  2011,  katika  ofisi  zetu  zilizopo  eneo  la  Changanyikeni  karibu  na  Chuo  cha  Takwimu  kuanzia  saa  tatu  kamili  asubuhi.

KWA  MAELEZO  ZAIDI  WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA

                      0767010756   AU  0787010756
 
Au  tembelea  Blogu  yetu : http://www.mambomediacentre.blogspot.com//
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, September 29, 2011 | | Permalink | Maoni 1

Madhara yatokanayo na ARVs nchini yatafutiwe ufumbuzi wa haraka


Taarifa kwa Umma 29 Septemba, 2011
MADHARA yatokanayo na dawa za ARV kwa baadhi ya watumiaji hapa nchini yanahitaji ufumbuzi wa haraka ili kuweza kuondokana na tatizo hilo.

Hivi karibuni, vyombo vya habari vimeripoti tukio la kusikitisha lilitokea mkoa wa Mtwara kwamba kuna mwanaume anayeishi na virusi vya UKIMWI amebadilika maumbile yake na kuota matiti kama mwanamke katika kifua chake baada ya kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV). Alipotoa taarifa kwa daktari aliambiwa hali hiyo ni ya kawaida kwa watu ambao wanatumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo kwa muda mrefu.

Sikika imeguswa na matukio yanayotokana na utumiaji wa dawa hizo na kufuatilia suala hilo kwa ukaribu zaidi. Pamoja  na baadhi ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU), kutoa taarifa ya kuwa dawa wanazotumia zinawaletea madhara makubwa, bado baadhi wa watoa huduma husika wamekuwa hawachukui hatua yoyote juu ya ubadilishaji wa  dawa hizo kwa WAVIU.

Kutokana na taarifa kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa dawa hizo wamepatwa na madhara mengi ambayo ni uzito kupungua, mwili kuchoka, miguu na mikono kufa ganzi, mapele, kucha kubadilika rangi kuwa nyeusi na pia baadhi yao kubadilika kimaumbile pindi tu wanapoanza kutumia dawa hizo. Utaratibu uliopo ni kwamba mtumia dawa hizo anapoona athari zinaanza kutokea anapaswa kutoa taarifa kwa muuguzi wake ili aweze kubadilishiwa dawa nyingine lakini imegundulika kuwa mgonjwa anapotoa taarifa juu ya madhara hayo humchukua zaidi ya miezi sita kabla ya kubadilishiwa dawa na wakati mwingine huambiwa kuwa hali hiyo ni ya kawaida na itaisha.
Sikika pia imegundua kuwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma hizo havina mashine za CD4. Kifaa hiki ni muhimu kwa ajili ya kujua maendeleo ya mgonjwa na kutoa ushauri katika kinga za mwili na pia kuendelea na aina ya dawa wanazotumia. Tatizo hili limeendelea kuwa sugu hasa katika maeneno ya vijijini ambapo WAVIU wanalazimika kwenda mwendo mrefu sana kwa ajili ya vipimo vya hivyo. 
 
Suala hili limeonekana wazi katika wilaya za Kondoa na Mpwapwa ambapo baadhi ya vituo vya afya havina mashine za CD4. Vituo hivyo ni Kisese, Hamai, Songolo, Busi na Kwa Mtoro vinavyopatikana wilayani Kondoa na vituo vya afya vya Kibakwe, Rudi, Mima na Pwaga vilivyopo wilaya ya Mpwapwa.Ukosekanaji wa kifaa hiki kwa kiasi kikubwa unachangia mgonjwa kuendelea kutumia aina ya dawa moja  ambayo huenda haimfai tena kulingana na CD4 zake kutojua kama zimepanda au zimeshuka.

Sikika inapendekeza kuwa hatua kali zichukuliwe kwa watoa huduma ambao hawafuati utaratibu wa maadili ya kazi zao. Wizara husika pia iwajibike katika kuwasaidia wale ambao wameathirika kutokana na madhara ya utumiaji wa dawa hizo. Mfumo wa sasa wa kusikiliza matatizo ya watumia huduma uimarishwe ili kupunguza athari kubwa zinazotokana na madhara ya kutumia madawa hayo kutokana na wahudumu wengi kutumia lugha chafu.

Pia serikali inapaswa kuweka mashine za CD4 kwenye vituo ambavyo havina na kuzifanyia matengenezo haraka pale zinapoharibika ili zitumike kuwapima wagonjwa maendeleo ya kinga zao za mwili kabla hawajaanza matumizi ya dawa hizo ili kuondokana na tatizo hilo kubwa.

Mr. Irenei Kiria
Mkurugenzi wa Sikika, P.O.Box 12183 Dar es Salaam,
Simu: +255 222 666355/57,
Nukushi: 2668015, 
Barua pepe: info@sikika.or.tz, 
Tuvoti: www.sikika.or.tz
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, September 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0

jipatie gazeti lako makini la dira kwa sh 500,liko mtaani sasa.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, September 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu