rais kikwete atembelea majeruhi wa ajali ya basi la champion, ahutubia baraza la Iddi Dodoma leo.

Wednesday, August 31, 2011
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bwana Winston Chinduge  mkazi wa Gairo,mkoani Morogoro ambaye ni mmoja wa majeruhi wa Basi la Champion lililopata ajali juzi mkoani Dodoma.Majeruhi hao wamelazwa  katika hospitali ya mkoa wa Dodoma

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bi. Ashura Kassala, mkazi wa  Manzese jijini Dar es Salaam aliyelazwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma kufuatia kupata majeraha makubwa kutokana na ajali ya basi La Champion lililopata ajali juzi mkoani Dodoma.Rais Kikwete alikwenda kuwapa pole majeruhi hao baada ya kulihutubia baraza la Iddi  lililofanyika  katika msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma.
 Sheikh Mkuu  na mufti wa Tanzania Issa bin Shabaan Simba akipeana mikono na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Baraza la Iddi lililofanyika katika msikiti wa Gaddafi Mkoani Dodoma. Picha zote na  mdau Freddy Maro wa Ikulu
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baraza la Iddi  lililofanyika katika msikiti wa Gadaffi mjini Dodoma leo jioni.Picha zote na  mdau Freddy Maro wa Ikulu
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Wakazi - WAKATI NDIO HUU

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

KOCHA RAJABU MHAMILA SUPER D AKIWA KATIKA MAPAMBANO YAKE KABLA YA KUA KOCHA


Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila (Super D) kushoto akitangazwa mshindi zida ya bondia Safari Berdard kipindi hicho
 Super D Boxing Coach kushoto Akipambana na Rashidi Ali
Super D Boxing Coach kulia akipambana na Ajibu Salumu.









Mdau Rajabu Mhamila leo katutumia picha hizi kutoka kwenye maktaba yake ya picha,amesema si vibaya tukakumbushana na bondia huyo aliyekuwa machachari na uwezo mkubwa wa kuwasimamisha mashabiki vitini awapo ulingoni.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Rais Kikwete ashiriki Swala ya Iddi Jijini Dar es salaam leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Rais DK.Jakaya Kikwete akiwasalimu waumini walioshiriki swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani leo asubuhi jijini Dar.Picha na Freddy Maro. 
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 1

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI SWALA YA EID EL FITR MNAZI MMOJA jijini DAR leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El- Fitr, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo Agost, 31.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El-Fitr leo, Agosti 31.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo Agosti 31.
Immam Mkuu wa Msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam, Masoud Mohamed Jongo,  akitoa mawaidha baada ya swala ya Eid El-Fitr iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo, Agosti 31, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wajumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Agoost 31
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wajumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Agoost 31.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba (kushoto), wakiwa katika swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Agosti 31.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wakiwa katika swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Agosti 31.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

rais wa zanzibar,Dk shein ahutubia baraza la idd el fitri leo mjini humo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na baadhi ya waumini walioshiriki katika sala ya Idd el Fitri illiyosaliwa katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akiwahutubia wananchi na waislamu katika baraza la Iddi el Fitri lililofanyika huko ukumbi wa Salama hall  Bwawani Hotel mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,(watatu kulia) akijumuika na Viongozi wengine katika sala ya Idd el Fitri ilyosaliwaa katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,Sheikh Khamis Haji,Naibu Kadhi mkuu wa Zanzibar akiongoza sala hiyo.
Wananchi mbali mbali wa Mji wa Zanzibar na Vitongoji vyake wakimsikiliza, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipokuwa akisoma hutuba yake wakati baraza la Idd katika kusheherekea sikuu ya Iddi el Fitri huko ukumbi wa Salama hall Bwawani Mjini Zanzibar  leo.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Idd el Fitri huko katika Ukumbi wa Salama hall Bwawani mjini zanzibar,wakimskiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akisoma hutuba yake katika mkutano huo wa baraza la Idd leo.
Wananchi mbali mbali wa Mji wa Zanzibar na Vitongoji vyake wakimsikiliza, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipokuwa akisoma hutuba yake wakati baraza la Idd katika kusheherekea sikuu ya Iddi el Fitri huko ukumbi wa Salama hall Bwawani Mjini Zanzibar leo.
 Baadhi ya akina mama wa kiislamu walioshiriki katika sala ya Idd el Fitri katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,jana wakisikilidha Hotuba ya sala hiyo iliyotolewa na Sheikh Fadhil Soraga,(hayupo pichani).katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Wananchi mbali mbali wa Mji wa Zanzibar na Vitongoji vyake wakimsikiliza, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipokuwa akisoma hutuba yake wakati baraza la Idd katika kusheherekea sikuu ya Iddi el Fitri huko ukumbi wa Salama hall Bwawani Mjini Zanzibar leo.  Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

 ==========   ========  =========

Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi M, Al Hajj Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali imeandaa mipango kuhakikisha inaongeza fursa zaidi za ajira rasmi na zisizo rasmi Visiwani Zanzibar.

Akihutubia Baraza la Eid-El-Fitri Mjini hapa leo, Dk Shein alisema katika mwaka wa Fedha 2011/2012 Serikali inatarajia kuajiri watu 2,476 kulingana na  mahitaji na uwezo uliopo.

“Tunaelewa kuwa mahitaji ya fursa hizo ni makubwa zaidi…katika kukabiliana na uhaba wa fursa za ajira, Serikali inashajiisha wananchi kujiunga katika vikundi vya Ushirika ili waweze kunufaika” Alisema Rais Dk Shein.

Dk Shein alisema kuwa mkazo umewekwa katika kuvisaidia vikundi vya uzalishaji mali vinavyoanzishwa na vijana na wanawake ili waweze kujiajiri wenyewe wajiongezee kipato na kupambana na umaskini.

Akizungumzia mwezi mtukufu wa Ramadhan, Rais Dk Shein aliwakumbusha waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi wote nchini kuitumia elimu waliyoipata katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kuimarisha mwenendo mwema na kujenga maisha bora ya duniani na akhera.

Dk Shein alisema  suala la kudumisha amani, umoja na kuheshimiana miongoni mwa waislamu na wale wa dini nyengine  kumewezesha kuendesha ibada hiyo katika hali ya amani na utulivu.

Alisema kwamba  kuendeleza mwenendo  mwema na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kuleta matatizo na kusisitiza suala la kujenga uadilifu hasa katika sehemu za kazi kwa wafanyakazi kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Sherehe hizo zilitanguliwa na swala ya Iddi iliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja  na kuhudhuriwa na Makamu wa kwanza wa Rais, Seif Shariff  Hamad, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali  Idd na viongozi wengine wa Serikali, Dini na  Vyama vya siasa.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

FFU wa Ngoma Africa band wamewatia kiwewe washabiki Tuttlingen Festival,Ujerumani

FFU ! wa ngoma africa band wazidi kutia kiwewe washabiki Ughaibuni kwa watoto na wakubwa! wazungu na weusi muziki umewanasa wengi!

Ni hile bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU, Jumamosi ya 27.08.2011 walifanikiwa kuwazoa na kuwatia kiwewe washabiki wa  muziki katika onyesho la Tuttlingen Festival,huko Ujerumani.

Bendi hiyo imekuwa kifyagio cha maonesho mengi makubwa na ndio bendi ya mwanzo ya kiafrika barani ulaya kupata bahati ya kupendwa na kuwa na washabiki wengi wa mataifana umri mbali mbali katika kila kona duniani.

Wakali hao wa muziki wa dansi wanapanda jukwaani tena siku ya jumamosi ya 3.08.2011 katika Onyesho la AFRIKA MARKT litakalofanyika mjini Steinhude am meer,jirani na  Hannover,nchini Ujerumani.wasikilze FFU at www.ngoma-africa.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

eid mubarak kwa wadau wote.

Blog yako ya JIACHIE inawatakia Idd njema wadau wote popote pale mlipo,aidha mnaombwa msherehekee kwa amani,upendo na utulivu,tujitahidi kuepuka ghasia za hapa na pale zenye kuleta machukizo miongoni mwetu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 1

fancis cheka kuzichapa na mada maugo ndani ya UWANJA WA JAMUHURI MOROGORO IDI PILI



MABONDIA Asha Abubakar na Fadhila Adam wanatarajia kudundana katika pambano la kuhamasisha ngumi kwa wanawake litakalofanyika Idi pili katika Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.
 
Pambano hilo litakuwa ni miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Fransic Cheka na Mada Maugo.
Pambano hilo la ubingwa wa UBO linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa Middle huku likisimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania,(PST).
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Promota wa ngumi hizo Kaike Siraju alisema, pambano hilo la kuhamasisha litakuwa la raundi 6 huku katika uzito wa Fly ambalo litakuwa ni moja ya pambano la kivutio siku hiyo.
 
"Wanawake ni wachache sana wanaoshiriki katika mchezo huu hivyo ni naimani watu watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wadada hao," alisema kaike.
Alisema, kwa upande wa Maugo na Cheka kila bondia kajiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuweza kuibuka na ubingwa ili aweze kuendeleza rekodi yake.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
 
"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

watu nane wapoteza maisha kwa ajali ya Basi La Champion,Dodoma

AJALI za barabarani zimezidi kutikisa nchi baada ya jana, basi la Kampuni ya Champion kupinduka na kuua watu nane papo hapo Mkoani Dodoma.Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilitokea mnamo saa 8:00 mchana, katika kijiji cha Nala wakati basi hilo likitoka Mwanza kuelekea jijini Dar es Salaam na kwamba, majeruhi 53 wamelazwa katika hospitali ya mkoa Dodoma.

Eneo hilo la ajali ni kilomita 15 kutoka Dodoma mjini na Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zelothe Stephen amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, lakini akasema, uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo unaendelea.

Hata hivyo, kamanda Stephen alisema taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda zinaeleza chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambaye alishindwa kulimudu gari hilo baada ya kukutana na tuta ghafla.

Kwa upande wa mashuhuda hao, walisema chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni mwendo huo kasi na wakati dereva alipokutana na tuta ghafla tairi la mbele la basi hilo lilipasuka na ndipo lilipopoteza mwelekeo.


Taarifa hizo zilifafanua kwamba, baada ya basi hilo kupasuka tairi moja la mbele na kupoteza mwelekeo tairi lake jingine la mbele pia lilipasuka ndipo likapinduka matairi juu bodi chini.

Mwandishi aliyefika muda mfupi baada ya ajali, alishuhudia baadhi ya miili ikitolewa na baadhi ya marehemu walifariki kutokana na kukosa hewa kutokana na basi hilo kuwafunika wakati matairi yakiwa juu.


Katika tukio hilo, juhudi za kutoa miili ya marehemu katika basi hilo pamoja na majeruhi zilifanyika kwa takriban saa tatu tangu kutokea ajali hiyo hadi mnamo saa 11: 35 jioni.

Katika siku za karibuni nchi imeshuhudia ikitikiswa na ajali za barabarani huku Mkoa wa Morogoro ukiwa umeandamwa zaidi kuanzia ile ya wasanii wa kundi la Five Stars, kati ya lori la Mohamed Enterprises (MeTL) na basi la Hood ambayo magari yote yaliteketea kwa moto. Chanzo:Gazeti Mwananchi. Picha ya Mtandao
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

salamu za Eid kutoka kwa Mustafa Hassanali


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Msondo Ngoma, Twanga Pepeta kukonga nyoyo TCC Club .

Bendi maarufu nchini za Msondo Ngoma na African Stars “Twanga Pepeta” zinatarajia kukonga nyoyo za wapenzi wao zitakapotumbuiza leo na kesho katika ukumbi wa TCC Club Chang’ombe, Temeke Dar es Salaam.
Bendi hizi mbili maarufu nchini hazijafanya maonyesho katika ukumbi huu kwa kipindi chote cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, jambo ambalo limefanya wapenzi wao kuwa na kiu ya burudani.Msondo Ngoma ndiyo itakuwa ya kwanza kutumbuiza leo (Iddi Mosi) mchana kwenye onyesho la Konyagi Idd Bonanza.
Onyesho hilo litaanza saa nane mchana  ambapo mwanamuziki nguli hapa nchini Muhidin Gurumo ataonekana  tena kwenye jukwaa la Msondo Ngoma baada ya kutoonekana jukwaani kwa muda mrefu kutokana na kuugua.
Bonanza hilo pia litatumiwa na Msondo kusheherekea tuzo yao ya kuwa bendi bora ya muziki wa rumba Afrika Mashariki na Kati.
 Baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma.
Wiki iliyopita Msondo ilizibwaga bendi maarufu za JB Mpiana na Werason Ngiama Makandi, kwenye tuzo zilizofanyika Nairobi, Kenya hivi karibuni.Twanga Pepeta, itatumbuiza kesho usiku (Iddi Pili) kwenye ukumbi huo wa TCC Club kwenye onyesho lingine iliyodhaminiwa na Konyagi pia.
Mratibu wa monyesho hayo, Joseph Kapinga, amesema jana kuwa maandalizi ya shoo zote mbili zimekamilika. Maonyesho yote mawili yameaandaliwa na Keen Arts ikishirikiana na Bob Entertainment chini ya udhamini wa Konyagi.
Naye mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka, amesema kuwa onyesho hilo litatumika kutangaza albamu yao mpya inayotarajiwa kutambulishwa rasmi baadaye mwaka huu. 
Nyimbo zilizomo kwenye albamu mpya ya Twanga Pepeta ni pamoja na “Kauli, Kiapo cha Mapenzi, Umenivika Umasikini, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja” na “Penzi la Shemeji.”
Asha alisema kuwa onyesho la TCC pia litatumika kumtambulisha Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis ambaye amejiunga na bendi hiyo kuchukua nafasi ya mnenguaji Aisha Madinda aliyetimkia katika bendi ya Extra Bongo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, August 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Video ya Ras Nas pamoja na Dekula "Vumbi" Kahanga

Tuesday, August 30, 2011

Video ya Ras Nas pamoja na Dekula "Vumbi" Kahanga kwenye tamasha la Mela lililofanyika Oslo, Norway 29 Julai. Ilikuwa kivumbi na jasho. Kikosi cha Ras Nas kilijumuisha wanamuziki kutoka mataifa mbali mbali kama vile DRC, Congo Brazzaville, Ivory Coast, Sudan, Uganda, Norway na Australia.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, August 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

BESIDEI YA MTOTO IMANI PINTO YA KUTIMIZA MIAKA MINNE

Mtoto Imani Pinto (wa pili kulia), akizawadiwa na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuamidhimisha miaka minne ya kuzaliwa kwake, katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Babake mtoto huyo ni Juma Pinto ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concept Tanzania Limited, inayochapa gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania.
Mtoto Imani akiwa katika picha ya pamoja na watoto wenzake wakati wa hafla hiyo
Babake Imani, Juma Pinto pichani kulia akikata keki aliyomwandalia mwanawe. Kushoto ni Mamake Imani, Queen Komanya.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, August 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

REDDS KUANDAA ONYESHO KUBWA LA MAVAZI NA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2011 KUSHEHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU.



Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original imeandaa maonesho makubwa ya mavazi yatakayowashirikisha warembo wa Miss Tanzania 2011 yenye kaulimbiu ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

Redd’s ambayo ni kinywaji rasmi cha shindano la Miss Tanzania 2011 wamedhamiria kutumia maonesho haya kama chachu ya kuwapatia washiriki nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika sanaa ya mitindo.na kuwakutanisha na wadau wa fani ya mitindo ili waweze kujipatia njia mbadala ya kujiendeleza  baada ya mashindano.

Akiwa anaongea kuhusiana na onesho hili meneja wa kinywaji cha Redds Bi. Victoria Kimaro alisema “Redds kama mdhamini aliyeshiriki kikamilifu kwenye mashindano haya ya urembo toka kwenye ngazi za chini za vitongoji imetambua kuwa kuna umuhimu wa kuwapatia washiriki nafasi za ziada za kuonesha vipaji vyao kwenye fani mbalimbali ikiwemo ya ulimbwende na mitindo ili kuwawezesha kuwa na njia mbalimbali za kujipatia mafanikio ya kimaisha. 
 Meneja wa kinywaji cha Redd's (wa tatu kulia) Victoria Kimaro Akiwa amepozi na washindi wa vitongoji mbali mbali.
Maonesho haya ya mavazi yatawakutanisha warembo na wadau mbalimbali wa mitindo kama wabunifu wa mavazi, taasisi za walimbwende na makampuni ya matangazo ili waweze kugundua vipaji vipya na kuvipatia nafasi ya kuviendeleza.” 

Bi. Kimaro aliendelea kwa kusema kuwa “Tasnia ya urembo ina mchango mkubwa kwenye jamii yetu sio tu kwa upande wa burudani bali inawapatia nafasi warembo mbalimbali Tanzania kukuza vipaji vyao na kuwekea msingi ambao wakijipanga vizuri utawajenga na kuwaletea mafanikio mbalimbali kweye maisha yao.  

Maonesho haya ya mavazi ni mojawapo ya fursa ambayo Redds inayowapatia warembo wakuze vipaji vyao kama njia mbadala ya kujipatia maendeleo na mafanikio baada ya shindano la kitaifa.”

Maonesho hayo ambayo yatafanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 2 Mwezi wa 8 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam yatajumuisha wadau mbalimbali wa mitindo, burudani kutoka kwa Banana Zorro na B Band pamoja na mwanadada mkali wa mziki wa kizazi kipya Shaa. 

Warembo wa Miss Tanzania siku ya onyesho watavaa nguo zilizobuniwa na wanamitindo mbalimbali kama Binti Africa,, Kijo na Franco. Onyesho hili pia limemshirikisha mwanamitindo maarufu kutoka mji wa New York ambaye pia amefanya kazi na wabunifu mbalimbali wa kimataifa na nyota mbalimbali wa nchini Marekani Bi. Rosemary Kokuhilwa ajulikanaye kama Fashion Junkii.

Siku ya onesho warembo wataanza na safari ya kutembelea  kiwanda cha Bia Tanzania  (TBL) kilichopo Ilala Dar es Salaam ambapo watashuhudia mtiririko mzima wa upikaji wa bia na kujumuika na wafanyakazi wa kiwandani hapo kwenye chakula cha mchana.

Redd’s Original imeshiriki kikamilifu kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2011 ambapo imefadhili zaidi ya vitongoji 35 na pia kama mdhamini mkuu wa Redds Miss Ilala, Redds Miss Temeke na Redds Miss Kinondoni.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, August 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Eid Mubarak to all

 Hello Tanzanian!
 We would like to share Eid Mubarak  to all of you and welcome all of you to share with us Eid celebration at our attractive zoo at affordable cost for your enjoyment.

Dar es Salaam Zoo has now established seven (7) spacious gardens with adequate day time accommodation to hold Group/Family Celebrations at reasonable costs.  This is apart from the pleasure of enjoying the natural fresh environment, the direct interaction with wildlife and the excitement of recreation celebrities provided at the zoo such as horse/camel riding and motor cycle/go-cart racing in and outdoor games like football, tennis and volleyball .  We just open u horse club with affordable fee to be a membership
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, August 30, 2011 | | Permalink | Maoni 1

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, August 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

MARIAN SCHOOLS BAGAMOYO FUNDRAISING GALA DINNER INVITATION- 4TH SEPT

  Uongozi wa Shule za Marian Bagamoyo unawakaribisha wote kwenye Fundraising hii
ya Kujenga na kuendeleza Shule hizi.

Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba
Wazazi,wanafunzi wa zamani,wenyeji wa Bagamoyo na wote wale wenye Mapenzi mema mnakaribishwa sana sana tarehe 4th SEPT Diamond Jubilee Hall saa Moja jioni.
Asanteni! 
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, August 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Loveness ndiye Vodacom Miss Sports Lady

Vodacom Miss Sports Lady 2011, Loveness Flavian akiwa amepozi kwa picha baada ya kushinda taji hilo na kuwa mrembo wa tatu kati ya warembo 15 watakao tinga katika Nusu fainali za Vodacom Miss Tanzania zinazotaraji kufanyika Septemba 10, 2011 jijini Dar es Salaam
Vodacom Miss Top Model, Mwajabu Juma (katikati) ambaye alikuwa mrembo wa kwanza kuingia hatua ya Nusu Fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011 akiwa na mrembo wa pili kuingia katika hatua hiyo ya 15 bora Vodacom Miss Photogenic Tracy Mabula (kushoto) wakipozi kwa picha na mwenzao wa tatu kutinga katika hatua hiyo baada ya kutwaa taji la  Vodacom Miss Sports Lady Loveness Flavian usiku wa kuamkia jana katika Jumba la Vodacom Dar es Salaam yalipotangazwa matokeo hayo.
Vodacom Miss Sports Lady, Loveness Flavian akipongezwa na warembo wenzake wa Vodacom Miss Tanzania waliofanikiwa kuingia tano bora ya kuwania taji hilo la michezo baada ya mwenzao huyo kutajwa kuwa ndiye mshindi na anakuwa mtrembo  wa tatu kuingia katika hatua ya Nusu fainali za Vodacom Miss Tanzania mwaka huu. Mchujo waa warembo hawa ulifanyika katika siku ya michezo ya Vodacom Miss Tanzania wiki iliyopita.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Vodacom Miss Sports Lady wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutangzwa mshindi usiku wa kuamkia jana. Kutoka kushoto ni Rose Hurbert, Husna Maulid, Loveness Flavian, Salha Izrael na Delillah Ghalib. Mchujo waa warembo hawa ulifanyika katika siku ya michezo ya Vodacom Miss Tanzania wiki iliyopita.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, August 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

AIRTEL YAFUTURISHA WATEJA WAKE jijini MWANZA

Afisa mauzo wa  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kanda ya ziwa, Galus Mgawe akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wateja wake wa makampuni katika Hoteli ya Golden Krest , Mwanza juzi.
Baadhi ya wateja wa Airtel wa makampuni wakifuru  wakati wa FUTARI iliyoandaliwa na Airtel maalum kwa baadhi ya wateja wa makampuni katika  Hoteli ya Gold Crest, Mwanza jana.

=======    =======  =======  ========

   Tumieni SMS 100 za bure baada ya kutuma sms 4 kutakiana Iddi Njema.

 Tarehe 30 agosti 2011, Kampuniya simu za mkononi ya Airtel imewafuturisha baadhi ya wateja wake wa Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuboresha uhusiano na wateja wake walioko kila mahalia.


Akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja katika Hoteli ya Golden Krest jijini Mwanza Afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa , Bw Galus Mgawe alisema “ tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote na ndio maana tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili pia tuweze kujadiliana  na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo kwenye futari hii.

Airtel huwa  tunakutana na wateja wetu katika maswala mbali mbali ya jamii ikiwemo michezo burudani na hata katika kuinua sekta mbali mbali mfano afya na elimu,

Lakini leo ni siku muhimu kwetu Mwanza kwa kuwa tunafuturu pamoja na kutakiana mfungo mwema wa ramadhani na pia tutaitumia fursa hii kutakiana sikukuu njema ya Iddi ambayo imekaribia.

Ahadi yetu kwa wateja wote ni kwamba bado Airtel tutaendelea kuboresha huduma zetu ili ziendelee kuwa na ubora wa hali ya juu kabisa pamoja na kutoa mawasiliano kwa gharama nafuu kushinda yote. Alimaliza kwa kusema Bw Galus Mgawe

Nae afisa Uhusinao wa Airtel Tanzania Bi, Jane Matinde kwa niaba ya Airtel  aliwatakia wateja wote mfungo mwema wa Ramadhani pamoja na maandalizi mema ya sikukuu ya iddi inayokuja

“Airtel tunawatakia mfungo mwema wa ramadhani lakini pia maandalizi mema ya sikukuu!, endeleeeni kufurahia sms 100 za bure baada ya kutuma smsm 4 tu, pia furahieni huduma bora za barua pepe pamoja na  kupiga simu katika kutakiana sikukuu njema kila mahali” aliema Bi Matinde

Airtel Tanzania  imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa   kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.Bado Airtel inampango wa kutoa misaada  katika mikoa ya mbalimbali kwa dhumuni la kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, August 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu