VODACOM YAJA NA MUONEKANO MPYA WA HUDUMA YAKE YA M-PESA

Sunday, July 31, 2011
Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania  Bi. Mwamvita Makamba wanne kutoka kushoto na Mkuu wa kitengo cha huduma za kifedha wa kampuni hiyo Bw. Jacques Voogt kushoto kwake,wakishikana mikono kuashiria uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma  ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.
Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania  Bi. Mwamvita Makamba akimsikiliza kwa umakini,Mkuu wa Kitengo cha huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania Jacques Voogt akiongea wakati wa uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma  ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali.
Wafanyakazi mbalimbali wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye mfano wa vazi analovaa"Superman" wakati wa uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma  ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma  ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom wakifuatilia kwa makini uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma  ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, July 31, 2011 | | Permalink | Maoni 1

RISALA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein, akisoma risala ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuwatakia wananchi kheri kati mfungo huo kwasalama,pia kuwataka wajitahidi katika kufanya ibada kwa wingi,kuzidisha imani katika jamii.Picha na Ramadhan Othman IKuLu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, July 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

UFUNGUZI WA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM MJINI DODOMA leo.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akiingia katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma, leo Julai 31, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama.
Mwenyekiti wa CCM taifa, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Aman Abeid Karume (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa (kulia) na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama, wakiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu kilichofunguliwa leo Julai 31, katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu  kilichoanza leo Julai 31, 2011 katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Jakaya Mrisho Kikwete,akiendesha kikao cha kamati Kuu ya CCM kilichofanyika leo katika ukumbi wa Makao Makuu ya Chama hicho Mjini  Dodoma.
Waziri Mkuu wa Tanzania pia jumbe wa kamati Kuu ya CCM akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe, Vuai Ali Vuai,kabla ya kuanza kwa Kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo Dodoma.Picha na Ramadhan Othman Dodoma
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, July 31, 2011 | | Permalink | Maoni 2

AFISA BIASHARA MKUU WA KAMPUNI YA AIRTEL TANZANIA AWATAKA WANAMASOKO KUJIPANGA KULETA TIJA NCHINI.

Maafisa masoko nchini wametakiwa kuwa wabunifu ili kuyawezesha makampunia yao kuendelea kufanya vizuri katika mazingara ya sasa ambayo yanaushindani mkubwa wa kibiashara.Akiongea katika usiku maalum wa maafisa masoko uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Chiruyi Walingo ambaye in afisa biashara mkuu wa kampuni ya airtel Tanzania alisema  fani ya masoko ina changamoto nyingi ambazo zinahitaji ubunifu ili kukabiliana nazo.

"Idara ya masoko ni moja ya idara nyeti sana katika kampuni yoyote ile. Idara hii naweza kusema ndiyo roho ya kampuni kutokana na ukweli kuwa kufanikiwa kwa kampuni yoyote kunategemea sana juhudi za watu wa masoko ," alieleza

Walingo aliwaeleza washiriki wa usiku wa wanamasoko kuwa  ushindani mkubwa ni moja kati ya changamoto ambayo inamuhitaji afisa masoko afikiri sana na kuwa mbunifu ili aiwezeshe didhaa ya kampuni yake iendelee kuwepo na kufanya vizuri sokoni.

"Ni muhimu sana kwa afisa masoko kuwa mbunifu na kuwa tayari kupambana na changamoto za kimasoko. Unaweza katumia muda wa mwezi mmoja kufikiria na kugundua bidhaa mpya lakini mshindani wako akaikopi kwa dakika moja tu. Lakini hii ni changamoto ya kukufanya wewe ufikiri zaidi," alieleza.

Alisema maafisa masoko wanakiwa kuwa na washauri ambao wamekuwa kwenye fani kwa miaka mingi kwa ajili ya kuwapa ushauri na kupitia uzoefu wa siku nyingi wa watu hao wanaweza kujikuta wakijifunza mambo mengi amabayo yatazidi kuwajenga kitaaluma.

"Wakati mwingine unaweza kujikuta hujafikia lengo ulilojiwekea au kuwekewa na inaweza kukufanya ukate tamaa. 
 
Mshauri ni muhimu sana kwa vile atakusaidia kwa  kukupanua mawazo kupitia uzoefu wake wa siku nyingi na hivyo kujikuta unazimudu vyema changamoto na kuwa mwenye mafanikio katika kazi yako," alieleza
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, July 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

umegundua nini kwenye hii picha??!

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, July 31, 2011 | | Permalink | Maoni 9

tamasha la serengeti fiesta 2011 lateka hisia za wengi usiku huu,shangwe na miluzi yalindima kila kona.

Saturday, July 30, 2011
Mwanamuziki Ludacris akitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye viwanja vya Lidaz Club,ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2011.ambalo kwa sasa limetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake,aidha tamasha hili limeandaliwa na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions kwa kushirikiana na Clouds FM,huku mdhamini mkuu wa tamasha hilo ikiwa ni kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake cha Serengeti premium lager.
 Luda akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu.
 Watu walikuwa kibao,halafu shangwe kila kona na miluzi ya haoa na pale ilitawala usiku.
 Ludacris akikamua jukwaani usiku huu.
 Pichani shoto ni Mwanamuziki Ludacris sambamba na mwanamuziki mwenzeke wakianza kulishambulia jukwaa usiku huu,kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,ambalo linatimiza miaka 10 sasa,tangu kuanzishwa kwake.
 Dj wa Mwanamuziki Ludacris akiwema mambo sawa,kabla ya Luda kupanda jukwaani.
 Kutoka kulia ni Mdau Emilian Rwejuna, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Richard Wells, Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager, Allan Chonjo na Mkurugenzi wa Masoko SBL Ephraim Mafuru, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kilele cha msimu wa dhahabu wa Serengeti Fiesta 2011,ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar usiku huu.
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Masoko SBL,Ephraim Mafuru, Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga, Muwakilishi wa kampuni ya Push Mobile,Omar,aliyekuwa Mkurugenzi wa Masoko SBL, Caroline Ndungu pamoja na Mdau Emilian Rwejuna.
Mkurugenzi mtendaji wa SBL Richard Wells akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Teddy Mapunda.
 Umati wa wati ukifuatilia kilochokuwa kikiendelea jukwaani usiku huu.
 Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akiendeleza ukongwe wake jukwaani pichani kati,huku baadhi ya wasanii wenzake wakimpa tafu akiwemo mwanadada machachari kabisa,Dayna
Ana majina kibao msanii huyu,ukimuita Binam kwakwe sawa,ukimwita Mwana FA aaah ndio kabisa,jina lake halisi anaitwa Hamis Mwinyjuma,akionyesha umahiri wake wa kurap jukwaani mbele ya maelfu ya watu waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,kwenye viwanja vya lidaz Club,Kinondoni jijini Dar usiku huu.
Mmoja wa wasanii nyota katika miondoko ya Hip hop hapa Bongo,Fd Q akitumbuiza jukwaani mbele ya maelfu ya watu waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,kwenye viwanja vya lidaz Club,Kinondoni jijini Dar usiku huu.


Mandojo na Domokaya wakizikumbushia enzi zao jukwaani.

























Msanii mahiri wa Kike kutoka nyumba ya vipaji THT,aitwaye Lina akicheza jukwaa na mmoja wa madensa wake kwa namna ya kipekee usiku huu,ambao shangwe za hapa na pale ikiwemo miluzi kibaoo.
Nyomi la Watu
Kijana mdogo hivi lakini mambo yake ni makubwa awapo jukwaani,anaitwa Beka Boy kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani.
Msanii wa kike Mwasiti pamoja na msanii mwingine anayeibukia vilivyo katika anga ya hip hop bongo,Gozilla wakilishambilia jukwaa la Serengeti Fiesta 2011 usiku huu.
Wakazi wa jiji la Dar ambao wametoka kila kona wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011.
Msanii mwimbaji na mtunzi kutoka THT aitwaye Amin akiwa na kundi lake wakionyesha umahiri wa kucheza jukwaani kwa namna ya kipekee kabisa usiku huu.
Msanii mahiri wa kizazi kipya Ben Paul akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu.
Pichani ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Serengeti Breweries Limited,Tedd Mapunda,Mkurungenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafuru pamoja na Mdau wakiwa wamepozi huku wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea jukwaani usiku huu kwenye viwanja vya Lidaz Clud,Kinondoni jijini Dar.

Umati wa watu uliofurika usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz Club,wakishangilia majotro yanayaoendelea hivi sasa,ama kwa hakika ni full kujiachia watu ni wengi na ulinzi upo wa kutosha kabisa.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Saturday, July 30, 2011 | | Permalink | Maoni 6
Idadi ya watu