wadau wakijadiliana na kupata msosi ndani ya mgahawa wa mara dishes-musoma.

Thursday, June 30, 2011
Jombaa Dick Kinyongo akiteta na mmiliki wa Mgahawa wa Mara Dishes,jina kapuni kwa sasa.! Kulia ni OPM wa Kampuni ya Prime Time Promosheni Ltd,Bwa.Balozi Kindamba akisikiliza kiaina.



Pichani kulia ni Balozi Kindamba kutoka Kampuni ya Prime Time Promotions Ltd akiwa sambamba na Mwenyeji wake ndani ya Mji wa Musoma,mkoni Mara,Bwana.Dick Kinyongo,walipokuwa wakipata mnuso wa mchana kwenye mgahawa maarufu sana ndani ya Musoma,Mara Dishes.Jombaa Dick Kinyogo pia anashiriki kuratibu tamasha la Serengeti Fiesta 2011 kwa namna moja ama nyingine,tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kesho katika uwanja wa mpira wa miguu wa kumbukumbu ya Karume.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

je unahitaji nyumba ya kupanga mahali popote pale jijini Dar?

"kwa yeyote anayehitaji nyumba ya kupanga popote Dar es Salaam, unaweza kuwasiliana nasi kwa namba ya simu pichani na utatafutiwa chap chap.".
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 1

taswira zangu nilizozinasa leo mchana nikitoka Mwanza kwenda Musoma mkoani Mara.








 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 1

NEW cosmetics ShOp In DAr!! AK Classic Cosmetics.


Guys, If you happen to be in Dar es salaam, Tanzania make sure you stop by a new hottest cosmetics shop in town, AK Classic Cosmetics located in Sinza-Kumekucha Kituoni. The shop has a wonderful selection of cosmetics from Victoria sectrets,Bath and body works,MAC, Mary Kay and Avon just to mention a few. Store hours are Monday- Saturday from 9am -9pm. Phone: 0713-468393/0753-482909.

Tupo Sinza-Kumekucha Kituoni. Mnakaribishwa wote.Tuna mahitaji yako yote ya urembo na kama hatuna tunachukua SPECIAL ORDER!!Tuna bidhaa za Victoria's Secret,MAC,Mary Kay, Avon,Perfumes na Colognes za aina mbalimbali kutoka kwa madesigners wa kimataifa na vilevile kuna sehemu ya Resale ambapo utapata first class
;-office wear,outing dresses,handbags,viatu etc.

Muda wa duka kuwa wazi 9am-9pm-Jumatatu hadi Jumamosi. Simu 0713-468393/0753-482909.
tutembelee www.akclassicosmetic.blogspot.com
Mwambie rafiki yako / jirani yako. Karibuni nyote!!!!





 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

HOTUBA YA Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi wa umma na utawala bora. 2011/2012

 NA NAFISA MADAI
KUTOKA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kupandisha kima cha chini
cha mishara kwa asilimia 25. Aidha  kwa upande wa wale wafanyakazi  wa kima ambacho wanaendelea na utumishi wao pamoja na wale wa ngazi nyengine, mbali na kurekebisha
mishahara yao kwa mujibu wa ngazi zao zqa mishahara yao itakuwa na
ziada itakayozingatia elimu na muda wa utumishi wao kazini.

Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya rais, utumishi wa umma na
utawala bor Mhe Haji Omar Kheri wakati alipokua akiwasilisha Hakadirio
ya mapato na matumizi ya  ofisis yake katika kiako cha baraza la
wawakilishi  mbweni nje kidogo wa mji wa zanzibar.

amesema kuwa upandishaji huo wa  mishahara umezingatia pia nyongeza
walizozikosa wafanya kazi tokea mwaka 2007,ingawa hakutokuwa na
malimbukizo  yaani AREA

Mh kheiramesema  kwa kuzingatia ufinyu wa bajeti utekelezaji wa
mabadiliko hayo ya mishahara mipya bil ya malimbkizo utafanywa kuanzia
mwezi wa octoba 2011. Aliendelea kwa kusema upandishaji jhuo wa mishahara umekwenda sambamba na Ahadi za Rais wa Awamu ya saba Dk Ali Mohd Shein  katika kampeni za
kuomba ridhaa ya kuongoza nhini aliahidi kupitia ilani ya uchaguixi ya
CCM kuimarisha mazingirz bora ya kazi na maslahi ya watumishi wa umma
serikalini.

Aidha alisema rasilimali watu ni nyezo muhimu katika kuhakikisha kuwa
utekelezaji wa sera na mipango mabalimbali ya kitaifa inapiga hatua. 
Hata hivyo  waziri huyo ailsema katika kuzingatia hilo Serikali imekua
ikichukua hatua  mbalimbali za kuwaendeleza kielimu na maslahi kwa
wafanya kazi wake.

Akizungumzia Utalawa Bora Mhe Kheri amesema ilani ua uchaguzi
inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa Umoja
wa Kitaifa ibara ya 186 imeweka msisitizo wa kusimamia utawala bora
nchini kwa kuimarisha demokrasia  pamoja na kulinda hai za binadamu.

Wizara  ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeomba
idhinishiwe jumla ya shiling bilion 4,855,246,000=/ kwa mwaka wa fedha
2011/2012 kwa ajili ya matumizi ya ofisi hiyo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Miss Africa Scandnavia atoa misaada mbalimbali kwa vituo vya watoto yatima.



Mrembo wa Afrika katika nchi ya Scandnavia, Michelle Jeng, akitoa msaada katika moja ya vituo vitatu vya watoto yatima   alivyotembelea hivi karibuni wakati akiwa Tanzania.  Ataondoka kurejea Sweden tarehe 2 July.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Senior Bachelor kufunga pazia la wiki ya maonyesho ya filamu mjini tanga.

Filamu ya Senior Bachelor imepangwa kufunga pazia la wiki ya maonyesho ya wazi ya filamu yanayoendelea katika viwanja ya Tangamano Mjini Tanga. Filamu hiyo ambayo itaonyeshwa jumaamosi hii katika Tamasha la Grand Malt la wazi la filamu linaloendelea viwanjani hapo imeongozwa na Single .

Mtambalike(RICHIE) na  production manager ni Suleiman Said Barafu.  Akiongea nasi Musa Kissoki Mkurugenzi wa Sofia Production waandaaji wa Tamasha hilo amesema anaamini filamu itasisimua wengi kwenye maonyesho hayo hasa kutokana na uigizaji wake.

"JB ni moja ya waigizaji wenye mbwembwe sana, hivyo hii imetoka kuwa moja ya kazi zake nzuri ambazo tutazionyesha katika tamasha hili la GrandMalt la wazi la filamu Tanzanial.

MUIGIZAJI wa filamu hiyo Jacob Stiven maarufu kama JB amejizolea umaarufu kutokana na filamu hiyo hadi kupelekea kupachikwa jina la Erick Ford alilotumia katika muvi hiyo;

Senior Bachelor ni moja ya filamu pendwa kuonyeshwa katika Tamasha hili JB anatarajiwa kuwepo mjini Tanga kufungua filamu hiyo katika hadhara kwa ajili ya maonyesho yake.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Majumlisho ya bajeti ya Waziri wa nchi ofisi ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Mwinyihaji Makame


Na Nafisa Madai              
Maelezo zanzibar                   
30/06/2011.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyi Haji Makame ameliambia baraza la Wawakilishi kuwa Tume maalum imeundwa ya kuchunguzi watendaji wa Baraza la Manispaa chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Khalid Mohammed.

Hayo yamesemwa jana na waziri huyo alipokuwa akifanya majumuisho ya hotuba yake huko katika Baraza la Wawakilishi kwa wajumbe wa baraza hilo ambapo wengi wao walipokua wakichangi bajeti walilitaka baraza la manispaa kuwajibika kwa kutowatendea haki wananchi wa Zanzibar

Aidha Dk. Mwinyi alisema Baraza la Manispaa lina mamlaka kama ilivyo vyombo vyengine na kulifahamisha Baraza hilo kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ni Mtendaji mkuu katika serikali hivyo na yeye anawajibu wa kufanya jambo lolote ndani ya mamlaka yake iwapo sheria itamruhusu.

Dk Mwinyi aliwaomba wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa wastahamilivu hadi pale tume iliyoundwa ya kuchunguza watendaji wa manispaa itakapomaliza kazi zake walizopangiwa  na kuwataka iwapo kutakuwa na malalamiko juu Mkurugenzi  wachukulie kama ni ubinadamu na ipo haja ya kurekebishwa na sio kuchukuliwa hatua kwa haraka.

Akizungumzia suala la mazingira Waziri huyo alikiri mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa ni kweli mji wa Zanzibar hauridhishi hata kidogo kutokana na kuzidiwa na idadi kubwa ya watu  ambapo alisema serikali kupitia  manispaa wameandaa mipango maalum ya kudhibiti hali hiyo.

Sambamba na hayo Dk. Mwinyi alisema licha ya kuwa Serikali imejipanga katika kudhibiti hali hiyo lakini bado suala la usafi ni la jamii nzima na sio Serikali peke yake, hivyo alitaka jamii nayo ijenge tabia ya kujiwekea mazingira mazuri katika maeneo yao.

Akigusia usalama wa Nchi Waziri huyo amesema hivi sasa Wizara yake imejipanga kwa kuhakikisha nyumba za viongozi zipo katika hali ya ulinzi wa kutosha tofauti na hapo awali ilivyokuwa ikionekana nyumba hizo zinaegeshwa magari kama sokoni.

Kwa upande wa ahadi za Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Haji,amesema kitengo maalumu kipo cha mawasiliano ikulu ambacho kitafuatilia ahadi  na kuhakikisha utekelezaji unafanyika awamu kwa awamu katika maeneo ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Kuhusu suala la kitaifa na kikanda, Waziri huyo aliwatoa hofu kubwa walioyokuwa nayo wajumbe hao ambao walitaka kujua Zanzibar kama ni nchi itafaidika vipi?ambapo alisema Zanzibar itafaida na mpango huo mara tu mabadiliko ya katiba yatakapofanywa.

Hutuba hiyo ya bajeti  katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ilibahatika kuchangiwa na wajumbe 39 ambao walitaka ufafanuzi wa kina kuhusu matumizi ya fedha katika taasisi zake ilipitishwa jana mchana kwa tabu kwa baadi ya vifungu kuwa gumzo kubwa kwa wajumbe hao
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

K-MONDO SOUND KUWABURUDISHA WANAFUNZI WA KISUTU.

Bendi ya muziki wa dansi ya K-Mondo Sound inatarajia kuwatumbuiza wanafunzi mbalimbali waliowahi kusoma katika shule ya msingi Kisutu iliyopo mjini Dar es Salaam.
Kiongozi wa bendi hiyo, Richard Mangustino amesema mjini Dar es Salaam kuwa onyesho hilo litafanyika Julai 17 kwenye hoteli ya Giraffe kuanzia saa 12 jioni.

“Mmoja wa wanafunzi waliosoma Kisutu alitueleza kuwa wanataka kukutana na kukukumbushana mambo mbalimbali pamoja na kutengeneza umoja wao, awali walikutana mara ya kwanza Januari mwaka huu wakaazimia kukutana tena shuleni kwao lakini haikufanyika sasa wameamua kurudi Giraffe na sisi tumewaandalia burudani ya nguvu,” alisema.

Alisema wanafunzi hao ni wale waliosoma kati ya mwaka 1980 hadi miaka ya tisini wakati shule hiyo ikiwa chini ya serikali baada ya kutaifishwa kutoka kwa jumuiya ya wahindu.
Awali walionza kukutana ni wanafunzi waliomaliza Kisutu mwaka 1990 lakini watu wengi zaidi wakajiunga katika kundi hilo ambapo pia taarifa mbalimbali zinapatikana katika mtandao wa Facebook kwenye ukurasa wa waliosoma Kisutu na Kisutu Primary School.

Kwa upande wa K-Mondo, Mangustino alisema watatambulisha pia mtindo wao mpya wa kiuno na bega huku pia wakimtambulisha pia mpiga gitaa la rythim Victor Victory pamoja na mpiga besi aliyerejea tena kwenye bendi hiyo Joshua Bass. K-Mondo Ijumaa hii itatumbuiza kwenye ukumbi wake wa nyumbani wa Triz Motel, Mbezi Beach wakati Jumamosi watakuwa Green Palm Resort Kunduchi.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

CHANGAMOTO YATOLEWA KWA VIJANA WANAOMALIZA MASOMO KUJIAJIRI.

Na. Aron Msigwa
MAELEZO.
Moroni, COMORO.
Vijana wanaomaliza masomo katika fani mbalimbali wametakiwa kutumia ujuzi walioupata kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini jambo  litakalopunguza idadi kubwa ya vijana wasio na kazi.
Akizungumza na wanafunzi  na walimu wa kituo cha Mafunzo cha EMDAD cha mjini Moroni nchini Comoro, mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) mama Salma Kikwete ,alisema vijana wengi wanaomaliza masomo katika vyuo mbalimbali wanashindwa kujiajiri wenyewe wakati ujuzi wa kufanya kazi mbalimbali wanao.
Alisema hivi sasa nchi nyingi zinakabiliwa na changamoto ya idadi kubwa ya vijana ambao humaliza masomo katika fani mbalimbali ambao wanauwezo wa kujiajiri  wenyewe lakini hawafanyi hivyo.
“Vijana wengi wanaomaliza masomo yao wengi husubiri kuajiriwa badala ya kujiajili wenyewe, natoa wito mnapomaliza masomo yenu mnakuwa tayari na ujuzi mjiajiri wenyewe na kuajiri wengine” alieleza.
Akiwa ameambatana na mwenyeji wake mke wa rais wa Comoro, mama Salma Kikwete alipata fursa ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanachuo na walimu wa chuo hicho huku akivutiwa na madarasa mawili moja likiwa la mafunzo ya kompyuta  na lingine la ushonaji kwa vijana wa kike ambao  hufundishwa kuajiajiri wenyewe pindi wanapomaliza masomo yao.
 Kaimu mkuu wa chuo hicho Bw.Mohammed Jalal alimweleza mama Salma Kikwete kuwa mfumo wa elimu unaotolewa katika madarasa hayo unalenga kumjenga kijana  uwezo wa kujiajiri  badala ya kutegemea ajira za serikali.
Alisema wanafunzi katika madarasa hayo hufundishwa kwa muda wa miezi sita na wanapomaliza hupatiwa vyeti vya ufaulu huku wale wanaoshindwa kufaulu kwa kiwango kilichowekwa hulazimika kurudia masomo yao.
Aliongeza kuwa wanachuo wanaofaulu vizuri zaidi ya kupewa vyeti hupewa mitaji ya fedha, vifaa au mikopo kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha shughuli mbalimbali za kuwapatia kipato.
“Mfumo wa elimu chuoni hapa unalenga kumjengea uwezo mwanachuo kuweza kujiajiri,kwa wale wanafaulu masomo yao vizuri hasa katika fani ya ushonaji tunawawezesha kwa vifaa vya kufanyia kazi na wakati mwingine tunawapatia mikopo ili waweze kuanzisha shughuli zao” alifafanua Bw. Jalal.
Pia akiwa chuoni hapo mama Salma Kikwete alipata fursa ya kutembelea karakana ya ufundi wa kutengeneza simu za mkononi ambapo aliweza kuona shughuli mbalimbali za masomo yaliyokuwa yakitolewa kwa wanachuo waliokuwepo.
Mwalimu wa darasa hilo Bw. Mohamed Reza alieleza kuwa vijana wengi wengi wanavutiwa na masomo yanayotolewa na karakana hiyo huku akibainisha kuwa mwamko wa kujifunza miongoni mwa vijana umekuwa mkubwa hali iliyopelekea wawe na muda tofauti wa vipindi vya masomo kutokana na uhaba wa madarasa.
“ Hivi sasa tuna vijana wengi wanakuja kuanza mafunzo, na hivi sasa tuna idadi ya vijana wapatao 100 katika karakana yetu ni ndogo, tumelazimika kuwa na madarasa 4 kwa muda tofauti ili kuwawezesha vijana wote kupata muda wa kujifunza” alibainisha Bw. Reza.
Kwa upande wake mke wa rais mama Salma Kikwete akihitimisha ziara yake chuoni hapo aliwapongeza wanachuo wote kwa kuamua kujifunza  huku akiwataka kusoma kwa bidii  ili pindi watakapomaliza masomo yao wajiajiri wenyewe badala ya kutegemea ajira za serikali ambazo ni chache.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

berryblack kushiriki semina kubwa ya muziki huko Boston.


"BERRYBLACK NITAWAKILISHA PANDE HIZI ZA TANZANIA/ZANZIBAR KATIKA KONGAMANO NA SEMINA KUBWA YA SIKU 3 INAYOHUSU MUZIKI NA SANAA ITAKAYOFANYIKA KATIKA MJI WA BOSTON MAREKANI,NATARAJIA KUSAFIRI WIKI IJAYO KUELEKEA AMERIKA ,ASANTENI NDG ZANGU"!!
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

NAPE ATEMBELEA MAGAZETI YA MWANANCHI NA GLOBAL PUBLISHERS

Nape akizungumza na wafanyakazi wa Global Publishers katika chumba cha habari cha Global. Wengine ni Mrisho, Ndauka, Sixtus na Ally.
Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akizungumza na Wahariri wa magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, alipofaya ziara katika ofisi za kampuni hiyo, Tabata Dar es Salaam.Wa pili kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda na  Kshoto ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Theophil Makunga,Mhariri Mrendaji gazeti la Mwananchi Dennis Msacky, na Mhariri wa Mwanaspoti Frank Sanga.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye(kulia) akikumbatiana kwa fraha na Mhariri Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Daniel Msacky,alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Ltd, Tabata, Dar es Salaam, 29/6/2011. Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Sixtus Mapunda.
                         Mhariri wa Habari wa Mwananchi, yahya Charahani akiwa kazini.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Kiu, Ijumaa na Champion, Abdallah Mrisho, baada ya kuwasili Ofisi za kampuni hiyo,Mwenge, Dar es Salaam.jana. Wapili kulia ni Mhariri Kiongozi wa kampuni hiyo    na Mhariri Kiongozi Oscar  Ndauka na Mwandishi wa kampuni hiyo Luqman Maloto na wapili kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda.
Nape akiwa katika ofisi za Global Publishers.Kushoto ni  Abdallah Mrisho Wengine kutoka kulia ni, Sixtus Mapunda, Maloto,Ndauka na Mhariri kiongozi wa michezo wa Global Saleh Ally.Picha Bashir Nk0rom0.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

REDD’S YAFADHILI VITONGOJI ZAIDI YA 35 KWENYE MISS TANZANIA 2011.



Meneja wa cha Redd's Victoria Kimaro (tsheti nyekundu) Akiwa na washindi wa vitongoji,kushoto ni Faidha Alli Miss Tabata,Naomi miss Sinza 2, Stella.     

Redds Original imeimarisha ufadhili wake wa miss Tanzania mwaka huu wa 2011. Kinywaji cha Redds kimefadhili vitongoji zaidi ya  35 nchini kote trangu uzinduzi wa Miss Tanzania 2011 ambavyo vimejumuisha kanda za Kusini, Kaskazini Mashariki na Kaskazini Magharibi .

Akiwa anaongea na waandishi wa habari meneja wa kinywaji cha Redds Bi. Victoria Kimaro alisema “mwaka huu tumeshiriki kikamilifu kwenye mashindano haya ya Miss Tanzania kwani tunaelewa umuhimu wa kuimarisha mashindano haya tangu ngazi za vitongoji. Tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa tunawapa waandaaji msaada wanaohitaji.  Warembo wamepatikana kwa kiwango kikubwa sana na wanaonyesha sifa zinazostahili kushindania kinyang’anyiro cha Miss Tanzania.” Bi. Victoria aliendelea kusema kuwa “ Sasa tumefikia ngazi ya mikoa na tunaendelea kushirikiana na waandaaji kuhakikisha kuwa wanakamilisha zoezi hili kiuhakika. Redds kama kinyaji rasmi cha Miss Tanzania 2011 imejikita ipasavyo tangu ngazi za mwanzo mpaka ngazi ya mwisho ya kumtafuta  mrembo wa  Tanzania.” 

Mpaka sasa REDDS imefanikisha na inaendelea kufanikisha mashindano ya Kanda ya kanda zifuatazo; Kusini ambayo ni Sinza, Chang’ombe, Tabata, Dar Indian Ocean, Dar Inter- College, IFM, UDSM,UDOM, Mzumbe, SUA, Kibaha, Ifakara, Dodoma, Morogoro, Ilala, Temeke, Kinondoni, Higher Learning, Central Zone na Easten Zone. Kusini ya juu vitongoji ni Higher Learning Inter College Iringa, Mbeya, Ruvuma, na Southern highland. Kanda ya Kaskazini mashariki vitongoji ni Arusha, Kilimanjaro (Moshi), Singida, Tanga na Northen zone.

Kaskazini magharibi ni Kahama, Tabora, Mara, Mwanza, Shinyanga, Kagera na Lake zone.
Balozi wa Redds Consolata Lukosi amewapongeza washindi wote waliopatikana mpaka sasa na kuwapa moyo kwenye mashindano ya ngazi inayofuatia kwa kusema kuwa “ mbinu kuu ya mashindano ya Miss Tanzania ni kujiamini na kuwa na nidhamu. Upendo kwa washiriki wenza pia ni kitu muhimu sana kwani unavyoonyesha upendo na ushirikiano kwa wenzako ndivyo unavyoongeza mvuto wa urembo wako kwa ujumla. Nawatakia washiriki wote mafanikio mema na wajione wote ni washindi kwa namna moja au nyingine.”

Redds imekuwa mstari wa mbele kwa miaka mingi kufadhili mashindano ya Miss Tanzania na imetoa mchango mkubwa kuhakikisha kuwa mashindano haya yanaboreshwa kadri miaka inavyoendelea na imefanikisha kwa kiasi kikubwa sana kunyanyua sanaa ya urembo nchini.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 2

RAIS,WENYEVITI NA WAKURUGENZI WA KAMPUNI MBALIMBALI ZA NCHINI MAREKANI WAANZA KUWASILI NCHINI KWA AJILI YA KUTENGENEZA DIPLOMASIA YA UCHUM

Rais wa kampuni ya Ahmed's Moving Express,Inc  Bw Ahmed Issa
akizungmza na wanahabari jana usiku baada ya kuwasili katika uwanja wa
KIA.
Mkuu wa CAMDEN hosptality group ,Bw Munir Walji akizungumza na
wanahabari jana usiku baada ya kuwasili katika uwanja wa KIA.
Mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya PIKE Electronic
corporation,Bw J,Eric Pike akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili
uwanja wa KIA.
Afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw Suleiman akizungumza
jambo na mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya PIKE,Bw J,Eric
Pike.
Afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw Suleiman akizungumza
jambo na mmoja wa wageni hao ambaye ni mke wa rais wa kampuni ya
Ahmed's Moving Express,Inc Bw Ahmed Issa.
Baadhi ya wageni hao wakikamilisha taratibu mbalimbali katika jengo la
VIP katika uwanja wa KIA.
Baadhi ya wageni hao wakikamilisha taratibu mbalimbali katika jengo la
VIP katika uwanja wa KIA.
Wakurugenzi wa kampuni mbalimbali za nchini Marekani wakiwasili jana
usiku uwanja wa ndege wa KIA.

========  ======  ======= ========   =======

Na Dixon Busagaga,Arusha.


UJUMBE wa wenyeviti na wakurugenzi wakuu wa kampuni mbalimbali za
nchini Marekani umeanza kuwasili nchini ukiwa na lengo la kutengeneza
diplomasia ya uchumi pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali vya
utalii hapa nchini.

Ujio huo ambao umeandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
unafahamika kama V.I.P Safari ambapo kundi la kwanza la wakurugenzi
hao limewasili jana majira ya saa 5:00 za usiku katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)likitokea nchini Marekani.

Waliowasili jana ni pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha umeme
ya PIKE Electronic Corporation ,Bw J.Eric Pike na mkurugenzi wa
kampuni ya CAMDEN Hospitality group inayojishughulisha na masuala ya
Hotel ,Bw Munir Walji.

Ugeni mwingine ni Bw Ahmed Issa,rais wa kampuni ya Ahmed’s Moving
Express,Inc ambayo pia ni wakala wa kampuni ya Wheaton World Wide
Moving ikijishughulisha na masuala ya usafirishaji.

Ugeni huo utakuwa nchini kwa muda wa takribani siku 10 kuzungumza na
viongozi mbalimbali akiwemo rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,
Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na rais wa Zanzibar ,Dk Ally Mohamed
Shein.

Mbali na viongozi hao pia ujumbe huo unatazamiwa kula chakula cha
pamoja na wafanyabiashara mbalimbali nchini kitakacho julikana kwa
jina la Bussness Lunch itakayofanyika kesho mjini Arusha.

Mbali na hayo pia ugeni huo utakula chakula cha pamoja na mkuu wa mkoa
wa Arusha na baadae utaendelea na safari ya kuelekea jijini Dar es
salaam na kisha kuhitimisha safari hiyo kwa kutembelea Zanzibari.


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

tangazo

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Nchi Ya Wapiga Porojo Itaendelea Kwa Muujiza Upi?

Na Nova Kambota
 
Kama kuna jambo linalowaumiza vichwa watanznia basi ni swali kuwa kwanini kila wanalopanga halifanikiwi? au kwanini wananchi ni masikini licha ya maliasili zilizojaa kila kona yanchi hii? Wakiangalia elimu hoi watoto wanafeli, wakija kwenye afya hakuna kitu, wakienda kwenye kilimo na hata umeme tabu tu kwa kifupi hakuna jipya ni uduni na ubabaishaji mtupu.  Katika lindi la mawazo ya namna hii au maswali mengi yasiyojibika tunawatazama viongozi wetu na uwajibikaji wao usiokidhi viwango kiasi kwamba wamepwaya mno , wajuzi wa kuzungumza bila kutenda, ni watu wa blah blah na porojo tu.

Kwakweli Tanzania imetawaliwa na wapiga porojo hebu angalia kwenye hiyo kaulimbiu ya “kilimo kwanza”inavyotangazwa na kupigiwa chapuo na viongozi wetu kasha nenda huko vijijini kwenye mashamba utaona hata mabwana shamba hakuna na hizo pembejeo zenyewe za kilimo hakuna, sasa utasema hapo kuna kilimo kwanza au porojo tu?

Geukia elimu nddio utashangaa kabisa kulivyooza huko lakini cha ajabu ni kuwa viongozi wetu bado wna ujasiri wa kusimama kwenye majukwaa na kudai kuwa serikali imeboresha elimu, elimu gani? Shule za kata? Si ndio hizi zinatoa sifuri? Nasikia siku hizi zinaitwa mtambo wa sifuri, ajabu sana! Yaani serikali inajenga majengo tupu bila walimu,madawati wala maabara kasha wanaita sekondari halafu wanazidi kuboronga wanafuta mitihani, tuziiteje hizi? Hizi ni porojo za watawala wetu, porojo porojo kila mtu anapiga porojo tu.

Njoo kwenye hizo huduma za afya , tunaambiwa kuwa Tanzania bila maralia inawezekana tena kwa mbwembwe kwa matamasha makubwa lakini hivi mtu wa kule kijijini analala chini hana hata hiko kitanda je hiyo neti atachomeka wapi? Au motto wa mtaani analala kwenye vichochoro huyu neti atachomeka wapi? Sasa hizo Zahanati za vijijini kama kweli zinaviwango mbona vifo vya akina mama wajawazito bado vinaendelea? Hakika hizi ni porojo za viongozi wetu!

 Halafu anaibuka kiongozi mkubwa wa nchi anadai msongamano wa magari jijini Dar es salaam ni ushahidi wa kukua kwa uchumi wetu, hizi sasa porojo, uchumi wetu na nani? Mafisadi? Au Brigedia Al Adawy na Dowans? Uchumi umekua na ombaomba wameongozeka ndiyo magari yameongezeka na umasikini umekithiri , sasa huo uchumi uliokua umemnufaisha nani? Mawaziri na wabunge? Au rais na waziri mkuu? Hizi ni porojo tupu.

Serikali nayo imeshindwa kuweka huduma za nishati ya umeme wa uhakika, sasa naona ina mchoko naam! Huu ni mchoko ndio maana kila kwenye hotuba tunapigwa kalenda mpaka mwaka huu au ule tatizo la umeme litakuwa historia halafu mda huohuo umeme ni wa mgao, waziri wa nishati nay eye hana jipya bado watu tunateseka kwa sababu ya kukosa ubunifu na uzalendo , mwenyekiti wa kamati ya bunge ya nishati anataka tuwashe mitambo ya Dowans, watu wanahoji anataka turudi tulipotoka? Hizi kama sio porojo nini basi? Nchi ipo gizani viongozi wanapiga porojo inasikitisha sana.

Tabia ya kupiga porojo inaendelea kudidimiza nchi , hata kwenye michezo tunapiga porojo halafu tunataka kucheza kombe la Dunia,bungeni kuna porojo kiasi kwamba bunge linafanywa sehemu ya kupigana vijembe na mipasho halafu na sisi tunaamini iko siku tutakuwa kama wenzetu wa Ulaya na Marekani ambao tayari wamefuta blah blah na porojo kwenye kamusi za vichwa vyao wanafanya mambo kizalendo na kwa kujituma, haiwezekani !

Matokeo ya porojo yanapoonekana viongozi wetu hawachelewi kusikitika na kuhidi kujirekebisha, ona matokeo ya kidato cha nne yalivyowaumbua viongozi sasa wanajifanya wamejifunza hakuna kitu porojo tu , mabasi yanakimbia yanavyotaka wenye jukumu la kulinda usalama barabarani wanapiga porojo watu wanakufa utadhani ni msimu wa ajali.

Siku hizi hadi viongozi wa dini wamekumbwa na tabia ya kupiga porojo , badala ya kutetea wanyonge wao wanagombana wenyewe kwa wenyewe, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kujigeuza miungu watu wanadanganya masikini na kuwakamua hata kidogo walichonacho na wengine wamejigeuza watabiri wanatabiria watu kufa? Hizi ni porojo tupu.

Sasa katika muktadha huu ndio maana najiuliza kuwa nchi hii iliyolewa kwa wingi wa porojo itaendelea vipi?  Badala ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma kwasababu ya porojo zisizokwisha na hazina mipaka hata kwenye mambo ya msingi tunapiga porojo au ndio tunategemea  kuendelea kwa miujiza ya Mussa?  Tafakari!

Nova Kambota Mwanaharakati,
0717 709618 au +255717 709618
Tanzania, East Africa,
June 30, 2011
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, June 30, 2011 | | Permalink | Maoni 4

Baba joniii yupo kanda ya ziwa,kuna lolote la kumwambia..?!

Wednesday, June 29, 2011
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 29, 2011 | | Permalink | Maoni 22

mandhari ya jiji la Mwanza jioni ya leo.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0

HOT NEW RELEASES FROM TALENT AFRICA.


What's Up Africa!

Find below three hot new releases from Talent Africa Group (formerly Talent 256).  Talent Africa Group is an entertainment company that operates in multiple areas of the entertainment industry including; talent management, booking agency, events management, promotion, audio/video production, record label, PR and graphic design. Talent Africa operates all over East Africa but headquarters are located in Kampala, Uganda.  We represent most of the top names in the music industry from all over Africa and beyond... 

If you get these emails it means you are on our African Music Industry Email list where you receive new music releases, newsletters and the releases about what is happening on the East Africa Music Scene.  If you wish not be a part of this list please email and let us know so we remove you from future emails.

Song: Kawa (East Africa Remix) 
Artist: Lilian (BLU 3) featuring P Unit, Navio and AY
Producer: Oboi @ Market Makers
Artist Management and Agency: Talent Africa 
Description: Kawa the original was massive!  
And now here comes the remix featuring East Africa's top MCs from Kenya, Uganda and Tanzania. An EA anthem in the making...   
Song: Mama 
Artist: Richy 
Producer: Kingsley @ Talent Africa
Artist Management: Talent Africa
Description: Richy is Uganda's youngest music sensation. Can you believe this guy is only 19. So versatile he can crossover from RnB to Hip Hop to Soul and Reggae. Talent defined!
Song: Air UG
Artist: Klear Kut (Navio, The Mith, and JB)
Producer: Samurai @ Talent Africa 
Artist Management and Agency: Talent Africa
Description:  Klear Kut is back! 
While all the members have solo projects 
they are also working on a new group album and "AIR UG" is the first single. 
Get aboard Klear Kut Airlines.
Official Video coming soon
Enjoy!
Talent Africa Group

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 29, 2011 | | Permalink | Maoni 2

Mdundo wa FFU wa Ngoma Africa band umekubalika na wengi! kwa watoto,Vijana na wazee ! Freudenstadt City !

Ndivyo hilivyokuwa Jumapili ya 26.06.2011 ! mjini Freudenstadt,kusini mwa ujerumani,kwamba bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU wamejikuta wakiwa na shughuli pevu jukwaani baada ya washabiki wa umri mbali mbali kunaswa na mdundo wa bendi,wapo washabiki walioshindwa kujiziwa kabisa..hadi walipokwea jukwaani na kujimuhika na FFU katika kuyasheza magoma,tukio la kushangaza palitokea mtoto mdogo mwenye umri unaokisiwa kuwa miaka 3 au 4 naye aliwalazimisha wazazi wake lazima wampeleke jukwaa akalisakate gwaride la FFU!
Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kilianza kutumbuiza jukwaani kuanzia saa 10 alhasiri ahadi 12 jioni, washambuliaji wa kike wa bendi hiyo akina dada Bedi Beraca aka Princess Bedi Bella Bella na Severn Okomo,wakienda sambamba na Kamanda Ras  Makunja,hawakutoa nafasi ya washabiki kuketi !Mshambuliaji Chris B aka "Mshenzi wa solo" na mpini wake alikuwa anapeleka mashambulizi kila kona katika onyesho hilo kikosi hiko cha FFU kimeuteka mji wa Freudenstadt,Ujerumani na kuliweka dansi lao katika kila moyo wa mshabiki
kulikwa na pata shika na nguo kuchanika katika Onyesho la "Afrika Tage" mjini Freudenstadt,nchiniujerumani,siku ya jumapili 26.06.2011 kikosi kazi Ngoma Africa band aka FFU kilifanikiwa kwa mara nyingine kuwadatisha akili washabiki wake,kiasi cha washabiki kushindwa kijiziwia na kuvamia jukwaa la FFU na kwenda sambamba na gwaride la mziki.wasikilize ffu at www.ngoma-africa.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Wednesday, June 29, 2011 | | Permalink | Maoni 1
Idadi ya watu