Tuesday, May 31, 2011
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal kesho Jumanne ya Aprili Mosi, 2011 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya Mazingira Duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Ruvuma katika mji wa Songea. Makamu wa Rais Dkt Bilal anamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho hayo ambayo ujumbe wake Kimataifa ni MISITU NI TUNU YA ASILI. Kwa upande wa Tanzani moto ya siku hiyo kwa mwaka huu ni MIAKA 50 YA UHURU, PANDA MITI NA KUITUNZA: HIFADHI MAZINGIRA.

Katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais anatarajia kuzungumzia hali ya Mazingira nchini kwa miaka 50 tangu uhuru, Mazingira ikiwa ni moja ya Idara/Wizara iliyochini ya Ofisi yake. Sambamba na shughuli hiyo Makamu wa Rais atapata fursa ya kukagua mabanda mbalimbali katika Uwanja wa Majimaji ambapo pia atapata kusikia salamu maalum za Mkoa wa Ruvuma katika maadhimisho hayo ambayo yataambatana na ujumbe kutoka kwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Dkt. Terezya Huvisa.

Imetolewa na: Boniphace Makene

Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais

Mei 31, 2011

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, May 31, 2011 | | Permalink | Maoni 3

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA KUTOTUMIA TUMBAKU DUNIANI WILAYANI BAGAMOYO leo

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hadji Mponda akizungumza na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia Tumbaku duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Majengo Bagamoyo. Pamoja na mambo mengine amesema serikali imeandaa mpango mkakati wa miaka 5 kwa lengo la kudhibiti matumizi bidhaa za tumbaku nchini.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bi. Rutgard Kagaruki mmoja wa wahamasishaji walio katika mapambano dhidi ya matumizi ya bidhaa za tumbaku nchini kutoka asasi ya kiraia inayopiga vita matumizi ya bidhaa za tumbaku nchini (Tanzania Tobacco Control Forum) wakati alipotembelea banda la maonyesho la asasi hiyo wilayani Bagamoyo leo.

Wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo wakitoa huduma mbalimbali za Afya kwa Wananchi ikiwemo upimaji wa macho leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani ambayo kitaifa yameadhimishwa leo wilayani Bagamoyo yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “ MKATABA WA KIMATAIFA WA KUDHIBITI MATUMIZI YA TUMBAKU DUNIANI”

Baadhi ya Raia wa kigeni wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia Tumbaku Duniani ambayo kitaifa imefanyika leo wilayani Bagamoyo.
Wanafunzi kutoka shule ya Msingi Majengo iliyoko wilayani Bagamoyo wakifuatilia jumbe mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia Tumbaku Duniani ambayo kitaifa imefanyika wilayani Bagamoyo.

Wanafunzi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASuBA) wakiwasilisha ujumbe unaopiga vita matumizi ya bidhaa za tumbaku wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia tumbaku Duniani leo wilayani Bagamoyo.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, May 31, 2011 | | Permalink | Maoni 1

“Rekodi” ya shuffle yang’arisha tangazo la Vodacom


“Rekodi” ya shuffle yang’arisha tangazo la Vodacom

Kampuni ya Vodacom Tanzania imeanza kutoa matangazo mapya ya televisheni yanayoendana na azma yake ya kuleta mapinduzi katika sekta ya mawasiliano ya simu nchini baada ya kufanya mabadiliko ya rangi kutoka buluu kuwa nyekundu pamoja na nembo ya biashara.

Katika tangazo jipya la kampuni hiyo lililonza kurushwa hewani hivi karibuni na vituo mbalimbali vya televisheni nchini na kupatikana pia katika mitandao ya kijamii ya intaneti – blogs mapinduzi ya utayaraishaji na ubunifu katika matangazo ya biashara vinaonakana.

Aidha kivutio kikubwa katika tangazo hilo ni picha za tamasha la kipekee la uchezaji wa muziki maarufu wa kisauzi - Koito ambapo lililenga kuvunja rekodi ya dunia ya idadi ya watu waliojikusanya na kucheza muziki kwa pamoja kwa wakati mmoja.

Tamasha hilo la wazi la aina yake lililohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa kada mbalimbali lilifanyika Februari mwaka huu katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Kigamboni jijinjni Dar es salaam ambapo bila kujali wingi huo wote walijipanga katika mistari iliyounda msitari mirefu isiyonakifani na kucheza muziki wa Koito kwa pamoja.

Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba, amesema kuanza kurushwa kwa tangazo hilo ni mwanzo wa utekelezaji wa azma ya Vodacom Tanzania kuleta mapinduzi ya jumla katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini yanayokidhi kubadilika kwa sura nzima ya Vodacom Tanzania.

Mwamvita amesema Vodacom Tanzania baada ya kufanya mabadiliko katika rangi na nembo yake ya biashara kinachofuata sasa ni kwa watumiaji wa huduma hizo kunufaika na mabadiliko hayo kuanzia ubora wa huduma na namna ya kufikishiwa ujumbe wa upatikanaji wa huduma hizo na njia mpjawapo ni matangazo ya biashara

“Ukiangalia tangazo letu jipya utaona ni jinsi gani mapinduzi makubwa ya ufikishaji ujumbe kwa wananchi yanavyoanza na hiyo ndio azma yetu kwa sasa wengi walikuwa wanajiuliza ni kwa vipi tumeamua kuwa na vibonzo katika matangazo yetu ile ni njia mojawapo lakini njia nyingi zaidi zeney ubunifu, uhalisia na ubora wa hali ya juu zinafuata na wadau wetu watazifurahia”alisema Mwamvita.

Alisema Vodacom Tanzania imejipanga kuhakikisha kila hatua inayoipiga kwa sasa inaendana na ujumbe wa mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni ndani ya kampuni hususan mabadiliko ya rangi.

Katika tangazo hilo jipya Vodacom Tanzania inawakumbusha wadau huduma mbalimbali inazozitoa kwa ubora wa hali ya juu ikiwemo sauti na data na jinsi huduma hizo zinavyounganisha jamii mbalimbali kwa wepesi,urahisi na uharaka zaidi ya mitandao minginenchini.

“Tumefurahi kwamba wadau wetu na wananchi kwa ujumla wamepokea mabadiliko yetu katika mtazamo mzuri na kwa furaha na Vodacom Tanzania kubakia kuwa mtandao chagua bora zaidi kwa kada zote nchini lakini kwetu tunatambua nini zaidi tunawaandalia kukidhi mahitaji yao katika ubowa wa hali ya juu na kadri ziku zinavyosonga mbele wataendelea kuwa watu wa kujivunia katika soko la huduma za simu za mkononi nchini”alisisitiza Mwamvita.

Mabadiliko ya rangi katika Vodacom Tanzania yana maana kubwa katika utoaji huduma za kampuni hiyo sokoni lengo kuu ni kuwafanya wateja wa kampuni hiyo kuwa katikati ya mipango yote ya kampuni pamoja na utekelezaji wake chini ya kauli mbiu ya Kazi ni kwako ikilenga kuwapa nguvu na mamlaka zaidi wateja katika kuchagua na kurahisisha maisha kupitia huduma za Vodacom.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, May 31, 2011 | | Permalink | Maoni 1

VIWANJA VINAUZWA

VIWANJA VIZURI VINAUZWA

VIPO ENEO LA MBWENI – GEZAULOLE – BLOCK 6.

WILAYA YA KINONDONI.

VINA UKUBWA WA

1. Eneo = 581.19 Sqm

2. Eneo = 648.91 Sqm


VIWANJA VILIPO NI HATUA CHACHE KUTOKA BARABARANI

VIWANJA HIVYO TAYARI VIMEPIMWA NA KUWEKEWA MAWE

NA KUZUNGUSHIWA NGUZO ZA SEMENTI KWA AJILI YA UZIO

PIA VIPO KWENYE RAMANI YA ENEO NA VINA BUILDING PERMITT

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NAMBARI:-

0714 – 940992

0713 - 466935

AU

KWA BARUA PEPE (E-MAIL)

zainul.mzige21@gmail.com

knowledgious@yahoo.com

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, May 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

mkuu wa mkoa wa ruvuma azungumzia maadhimisho ya siku ya mazingira duniani.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk Christine Ishingoma akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Kitaifa ambayo yanafanyika Mkoani Ruvuma ,Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula[Picha na Ali Meja]
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, May 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

MATUKIO YA MISS UNIVERSE YALIVYOKUWA mwishoni mwa wiki

MENEJA WA MAMBO YA NJE WA VODACOM TANZANIA NECTOR FOYA AKIMKABIDHI MISS UNIVERSE 2011 NELLY KAMWELU ZAWADI YA SIMU YA BLACKBERRY YENYE KIFURUSHI CHA MUDA WA MAONGEZI WA MIEZI 6 PAMOJA NA SAMSUNG TABLET (KIFAA CHA INTANET) CHENYE UWEZO WA KUREKODI SAUTI, DATA N.K, ANAYESHUHUDIA KULIA NI MKUU WA UDHAMINI WA KAMPUNI HIYO BW GEORGE RWEHUMBIZA.
Tatu bor ya Miss Universe.

WAREMBO WA MISS UNIVERSE WALIOFIKIA HATUA YA TANO BORA WAKIWA JUKWAANI KATIKA PICHA YA PAMOJA KABLA YA MSHINDI KUPATIKANA USIKU WA SHINDANO HILO,Vodacom walidhamini shindano hilo LILILOFANYIKA GOLDEN TULIP HOTEL MWISHONI MWA WIKI.
Mkuu wa UDHAMINI WA VODACOM TANZANIA GEORGE RWEHUMBIZA AKITETA JAMBO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI HIYO Dietlof Mare WAKATI SHINDANO LA MISS UNIVERSE LIKIENDELEA KATIKA HOTELI YA GOLDEN TULIP MASAKI JIJINI DAR ES SALAAM MWISHoni mWA WIKI.
JOPO LA MAJAJI WAKIONGOZWA NA OFISA MTENDAJI MKUU WA MASOKO NA MAHUSIANO WA VODACOM TANZANIA MWAMVITA MAKAMBA WAKIFUATILIA KWA UMAKINI SHINDANO LA MISS UNIVERSE LILILOKUWA LIKIFANYIKA KATIKA HOTELI YA GOLDEN TULIP NA KUDHAMINIWA NA VODACOM TANZANIA,MWISHONI MWA WIKI.
BAADHI YA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA VODACOM TANZANIA WAKISHUHUDIA SHINDANO LA VODACOM MISS UNIVERSE KATIKA HOTELI YA GOLDEN TULIP JIJINI AMBAPO MREMBO NELLY KAMWELU ALIIBUKA MSHINDI.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, May 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

ziara ya dr. shein pemba leo

Mgugaji wa ng'ombe wa maziwa Riziki Hanmad wa kijiji cha kisiwani kwa binti abeid akitoa maelezo kwa Rais alipokuwa katika ziara ya mkoa kaskazini Pemba.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na wachimbaji matofali ya mawe katika kiji cha Makaani Uwandani Mkoa wa kaskazini Pemba alipowatembelea na kuona athari za mazingira katika maeneo hayo.Picha na Ramadhan Othman.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, May 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

wanne wajishindia mamilioni ya promosheni ya tusker

Washindi wa Promosheni ya Tusker Milioni 500 kwa mashabiki wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya 'Maboss' wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL),leo kwenye ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo zilizopo Oysterbay,jijini Dar.
Pichani wa pili kulia ni mshindi wa promosheni ya Tusker milioni 500 kwa mashabiki.Saimon Mapunda ambaye ni mkazi wa Vigunguti akikabidhiwa mfano wa hundi wa shilingi Milioni Moja,Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Utawala (SBL),Bwa.Eric Adadevoh na wa pili kushoto ni Mkurungezi wa Masoko wa SBL Caroline Ndugu pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Tusker,Rittah Mchaki.

Pichani wa pili kulia ni mshindi wa promosheni ya Tusker milioni 500 kwa mashabiki.Othman Seif ambaye ni mkazi wa Mbezi beach akikabidhiwa mfano wa hundi wa shilingi Milioni Moja,Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Utawala (SBL),Bwa.Eric Adadevoh na wa pili kushoto ni Mkurungezi wa Masoko wa SBL Caroline Ndugu pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Tusker,Rittah Mchaki.
Pichani wa pili kulia ni mshindi wa promosheni ya Tusker milioni 500 kwa mashabiki.Robert Zabron ambaye ni mkazi wa Kigamboni akikabidhiwa mfano wa hundi wa shilingi Milioni Moja,Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Utawala (SBL),Bwa.Eric Adadevoh na wa pili kushoto ni Mkurungezi wa Masoko wa SBL Caroline Ndugu pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Tusker,Rittah Mchaki.

Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL),Caroline Ndugu akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo,kuhusiana na utoaji wa zawadi kwa washindi wanne wa promosheni ya Tusker milioni 500 kwa mashabiki.Anaefuata pichani ni Othman Seif,Robert Zabron pamoja na Saimon Mapunda ambao ndio walijishindio zawadi ya milioni moja kwa kila mmoja.

======= ======= ======= =======
Dar es Salaam, May 31, 2011: Four residents of Dar es Salaam emerged winners in the ten-week Tusker Beer promotion launched on May 5 in Dar es Salaam. The winners walked away with a cool 1m/- each at a brief ceremony held at the Serengeti Breweries office in Oysterbay, Tanzania.

Serengeti Breweries Limited (SBL) Marketing Director, Ms Caroline Ndungu who handed over the cash/ cheques to the winners Othman Seif and Robert Zabron said that the company is committed to value its loyal customers, Mr. Eric Adadevoh, SBL Human Resources Director handed over the cheques to lucky winners Benson Dikson Marick and Saimon Mapunda.

''That is why all our initiatives are always geared towards the achievement of the values by our consumers. Since the promotion began on the 5th of May 2011 we have 1,625 winners of 10,000/-, 188 winners of 50,000, 53 winner of 100,000 and 17 millionairs” Ms Ndungu said.

She said that the company has invested heavily in promotions aimed at making life better to its customers. The company has set aside 500m/- to be won in the promotion in which customers stand chances to win cash prizes amounting to a whooping 500m/-.

Through the marketing drive dubbed “Tusker million 500 kwa mashabiki”, consumers can win various prizes ranging from cash to free beers, according to the SBL Director.Ms Ndungu added that the drive is meant to reward customers for their unwavering support towards the Tusker brand.

“One only needs to purchase a bottle of Tusker and check under the crown to reveal either a free beer which will be redeemable at the nearest outlet or a unique seven-digit alpha numeric code which they can send via a text message to number 15317,” she said. She said that a consumer will then get an SMS response whether he/she has won. Cash prizes such as 10,000/- , 50,000/-, 100,000/- and 1m/-. “This is all about celebrating African spirit, good times and togetherness across cultures”, she said.

On their part, the winners said that the prize would change their lives completely by investing in small-scale businesses. “I thank Serengeti Breweries for this initiative which has made me a young millionaire”, one winner said.

SBL is part of Kenya-based East African Breweries Limited (EABL) and also Diageo, one of the world’s top beer brewers. It provides additional presence for the beverage company to that in Kenya, Uganda and the Great Lakes region.

The company’s main brands include Serengeti Lager, Tusker Malt Lager, Uhuru, The Kick, Malta Guinness and Guinness. It also distributes Diageo spirits brands like Johnnie Walker, Smirnoff, Baileys, Cuervo, Captain Morgan and Richort Brandy.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, May 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Standup Comedy Show - Tue 31 May 2011

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, May 31, 2011 | | Permalink | Maoni 0

serikali ya zanzibar inahitaji kiasi cha dola za kimarekani milioni 123.

Monday, May 30, 2011

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inahitaji kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 123 kuweza kumaliza tatizo la maji safi na salama kwa Mikoa ya Unguja na Pemba.

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Shariff Hamad ameuambia ujumbe wa viongozi wa Jumuiya ya Madhehebu ya Khoja Shia Ithinashir kwamba tatizo la maji safi na salama linafanyiwa kazi na kwa sasa zinahitajika fedha hizo kuweza kukamilisha miradi ya maji. “Kama mnavyofahamu Zanzibar kuna tatizo la maji, Serikali haijakunja mikono, mipango mbalimbali inafanywa kukabili tatizo hilo” Alisema Maalim Seif.

Maalim Seif amesema ikiwa fedha hizo zitapatikana basi matatizo yanayowakabili wananchi wa Visiwa vya Zanzibar kukosa maji safi na salama litakuwa historia hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kuwa na subira. Akizungumzia suala la umasikini,Makamu huyo wa kwanza wa Rais amesema Serikali imedhamiria kuwakwamua wananchi wake katika dimbwi la umasikini kwa kubuni mipango mbalimbali yenye tija kwa umma.

Maalim Seif amesema kuwa Zanzibar ni miongoni mwa nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na hali ya umasikini, lakini pamoja na hali hiyo, bado kuna matumaini ya kupunguza kwa kiasi kikubwa hali hiyo chini ya mpango mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini(MKUZA) Sekta kadhaa zimetajwa chini ya mikakati ya kupunguza umasikini katika
Visiwa vya Zanzibar huku kiwango cha elimu kikitarajiwa kuimarishwa sanjari na ukuzaji wa Sayansi na Teknolojia.

Makamu huyo wa kwanza wa Rais, amesema masuala ya afya ya jamii yamekuwa wakipewa kipaumbele ili kujenga jamii yenye afya bora ambayo itashiriki katika uzalishaji mali. Alisema kwa kuwa na watu wenye afya bora kunasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wan chi kwani muda mwingi utatumika katika uzalishaji mali na sio kwenye matibabu, hivyo aliwahakikishia msimamo wa Serikali kuimarisha sekta ya afya Zanzibar.

Maalim Seif amepongeza uamuzi wa Jumuiya hiyo kujenga kituo cha afya ambacho kinatumika na wananchi wote ambacho kinazingatia zaidi utoaji huduma kwa njia isiyo ya kibiashara.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, May 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

rais kikwete azindua Rasmi Barabara ya Misungwi-Geita yenye urefu wa kilometa 90 leo.

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Barabara ya Usagara Geita leo asubuhi.Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 90 imejengwa kwa thamani ya zaidi Tshs.78bn/ zilizotolewa na serikali ya Tanzania.Wengine katika picha, Kutoka Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro,Katibu Mkuu Ujenzi Balozi Herbert Mrango,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli, Mbunge wa Misungwi ambaye pia ni naibu Waziri Sayansi na Teknolojia Charles Kitwanga na Mkurugenzi Mkuu TANROADS injinia Patrick Mfugale.Picha na Freddy Maro.


 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, May 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

kumbu kumbu ya kifo cha Mary Donata.

Ni miaka miwili toka mama yetu mpendwa Mary Donata Watondoha kututoka,daima watoto,wajukuu ndugu jamaa na marafiki tunakukumbuka.Ulipendwa sana hapa duniana ila mwenyezi wa yote alikupenda zaidi na tunakuombea upumzike kwa Amani.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, May 30, 2011 | | Permalink | Maoni 1

mwakalebela atoa msaada kwa watoto wenye saratani Muhimbili.

Familia ya Mwakalebela wakiwatembelea na kuwapa pole,kuwafariji vilevile kuwasaidia watoto wenye saratani katika Hospitali kuu ya taifa ya Muhimbili jana

Mwakalebela akiwa na familia yake wakishusha baadhi ya vitu walivyovitoa kwa ajili ya msaada kwa watoto wenye saratani katika Hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili hapo jana
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, May 30, 2011 | | Permalink | Maoni 6

NAFASI ZA KAZI.

MaishaMema Education & Training Centre ni kituo cha Elimu, Mafunzo, Utafiti na Ukuzaji Maarifa...Kituo kinatangaza semina ya siku moja kuhusu MBINU ZA UANDISHI BORA WA VITABU... Semina imelenga katika kuwajengea washiriki uwezo wa kufanya kazi na kituo katika mradi wa SEXUALITY EDUCATION AND AWARENESS PROJECT CAMPAIGN ( SEA Project ), mradi unao ratibiwa na kusimamiwa na kituo na ambao umelenga katika kutoa elimu ya ujinsia, afya, uzazi wa mpango, haki,wajibu na kujitambua kwa wanawake kwa njia ya vitabu.

SIFA ZA WASHIRIKI.
Awe mwanamke mwenye sifa zifuatazo:
1. Umri miaka 18 hadi 40.
2.Elimu kidato cha nne, sita na kuendelea.
3.Mchapakazi na anayejituma na awe mwenye wito wa kweli wa kazi ya uandishi vitabu.

ADA YA USHIRIKI: Shilingi Elfu Ishirini na Tano Tu ( Tshs. 25,000/=).

LINI: Jumamosi, tarehe 04/06/2011

MUDA : Saa nne kamili asubuhi.

WAPI: PERFECT VISION SECONDARY SCHOOL.

IDADI YA WASHIRIKI WANAO HITAJIKA: Thelathini na Tisa Tu. ( 39 )

FAIDA ZA KUSHIRIKI KATIKA SEMINA HII: Washiriki wote thelathini na tisa watapata nafasi ya kuungana na wenzao kumi na moja ambao tayari wameshapatiwa mafunzo katika kufanya kazi ya uandishi wa vitabu katika mradi huu, ambao unaanza rasmi tarehe 01 June 2011 kwa washiriki kumi na moja ambao tayari walishapatiwa mafunzo

Fomu za kujiandikisha katika semina hii zinapatikana kuanzia leo, ijumaa, tarehe 27/05/2011.

Fomu zinapatikana katika ofisi zetu zilizopo katika shule ya sekondari PERFECT VISION iliyopo nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA...

Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 03/06/2011.... ..

WAHI FOMU YAKO MAPEMA, KWANI IDADI YA WATU WANAO HITAJIKA IKIKAMILIKA, TUTASITISHA KUTOA FOMU.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA: 0652458398 AU 0788363058..

NATANGULIZA SHUKURANI ZANGU ZA DHATI KWAKO. ASANTE NA KAZI NJEMA.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, May 30, 2011 | | Permalink | Maoni 1

BREAKINGNEWS :TOSAMAGANGA SEKONDARI HIVI SASA SI SHWARI ,FFU WATUMIA MABOMU.

Polisi wakiwaweka chini ya ulinzi wanafunzi eneo la Kitwiru nje kidogo na manispaa ya Iringa hapo ilikuwa ni kabla ya kuanza kupiga kurusha mabomu ya machozi.

Mwanakijiji kushoto akiwa na mwandishi wa habari wa Radio Ebony Fm wakifuta machozi kutokana na mabomu yaliyopigwa na askari hao kuwatawanya wanafunzi hao Mwandishi wa habari wa radio Ebony Fm akikimbia moshi ya mabomu ambayo yalikuwa yakipigwa na askari hao kutawanya wanafunzi hivi punde
Wanafunzi wa Sekondari ya Tosamaganga wakikimbia moshi ya mabomu yaliyokuwa yakipigwa na polisi
Hapa wakikimbia porini kunusuru afya zao chini ni vifaa vya wanafunzi vilivyotelekezwa

Hali ya usalama si shwari katika shule ya sekondari Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivi sasa wanafunzi zaidi ya 10000 wapo porini wakikimbizwa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ambao wanatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa katika maandamano ya amani kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuulalamikia uongozi wa shule hiyo.

Hadi hivi saa mabomu zaidi ya 10 ya machozi yamepigwa kuwatawanya wanafunzi hao ambao baadhi yao wanadaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na miti wakati wakikimbia porini kukwepa mabomu hayo huku wananchi wa Mseke wakikimbia nyumba zao .

Polisi wamewazuia waandishi wa habari akiwemo mmiliki wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao waliokuwepo eneo hilo wakifuatilia tukio hilo kuendelea kuchukua habari hiyo .

Undani wa habari hii ya picha zaidi zitakujia hivi punde katika mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com,japo kwa sasa binafsi macho yanauma sana kutokana na moshi ya mabomu hayo kunikuta pamoja na mwanahabari mwenzangu wa Radio Ebony Fm.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, May 30, 2011 | | Permalink | Maoni 2

aliyekwambia usingizi una mapozi a.k.a swaga nani.??!






 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, May 30, 2011 | | Permalink | Maoni 8

Miss Tabata watembelea mbuga za Mikumi.

Na Ripota Wetu, Mikumi.


Warembo 22 watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Tabata 2011 jana waliondoka Dar es Salaam kwenda kutembelea mbuga za wanyama huko Mikumi.


Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa lengo la ziara hiyo ni kukuza utalii wa ndani. “Lengo la ziara hii ni kutangaza utalii wa ndani. Tunataka warembo wetu wajue wanyama na vivutio vingine vinavyopatikana kwenye mbuga zetu hasa Mikumi,” Kapinga alisema.


Alisema kuwa wakiwa Mikumi, warembo hao wapata fursa ya kuwajua tabia za wanyama na ndege wote waliyomo kwenye mbuga hiyo.Miss Tabata imepangwa kufanyika Juni 10 katika ukumbi wa Da’ West Park.


Warembo waliyoondoka ni Marion Augustino (19), Neema Marwa (18), Catherine Julius (20), Lilian William (20), Godliver Mashamba (22) na Dorice Mutabingwa (21). Wengine ni Sweetlily Suleiman (21), Maria John (21), Happyness Emmanuel (18), Cresensia Haule (20), Mariam Manyanya (21), Agustina Mshanga (20), Nasra Salim (21), Faiza Ally (19) na Edina Mnada (21). Pia wamo Angela Fortunatus (21), Lucia Joseph (20), Lilian Brayson (22), Rita Mvungi (21) na Willieth Wilson (22).


Miss Tabata 2011 inadhaminiwa na Dodoma Wine, Vodacom, Redds Original, Integrated Communications, Paris Pub, Fabak Fashion, Freditto Entertainment, Chicken Hut, Travel Partners, Ben Expedition, Screen Masters, Sean Entertainment, Screen Masters, Michuzi blogspot na Anech Stationary.


Consolata Lukosi ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.

Mrembo huyo alikuwa nambari tatu mwaka jana kwenye shindano la taifa (Miss Tanzania) kabla ya kushinda taji la Redds Ambassador.

Mashindano hayo ya urembo yanaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, May 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

gazeti lako makini la dira leo liko mitaani kwa sh 500 tu.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, May 30, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Mdau saleh ally akiaga chama cha ukapera rasmi.

Sunday, May 29, 2011
Wafanyakazi wa Global Publishers walijumuika na ndugu, marafiki wa wageni mbalimbali katika kusherehekea harusi ya Mhariri Kiongozi wa magazeti ya Championi, Saleh Ally alipofunga pingu za maisha na mrembo Sarah Pima, jana (Jumamosi) katika Hoteli ya Lion iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam.Blog ya JIACHIE inakutakieni kila lakheri kwa hatua mpya mlioichukua katika Maisha yenu,Mungu awatie nguvu na kuyabariki maisha yenu mapya ya ndoa.Picha kwa hisani ya Globalpublisherstz.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, May 29, 2011 | | Permalink | Maoni 1

Wanaochakachua Haleluya Collection wasakwa,Atakayewafichua kulamba milioni 1/-



Na Ripota Wetu jijini.

UONGOZI wa Kampuni ya Msama Promotions, umeanza kazi ya kutawanya maofisa wake sehemu mbalimbali nchini kuwasaka wajanja 'wanaochakachua' cd za kazi za wasanii. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama,alisema maofisa wake tayari wameanza kuingia mitaani kuwasaka wanaodurufu kazi za albamu ya Haleluya Collection pamoja na kazi nyingine zilizofanywa na kampuni hiyo.

"Tayari tumeshaanza kuwasambaza maofisa wetu mitaani, kwani wapo wajanja walioanza kudurufu kazi za albamu hiyo iliyotoka hivi karibuni na kuzinduliwa wakati wa tamasha la Pasaka. "Mchakato huo umeanzia Dar es Salaam, na hivi karibuni maofisa wetu watahamia
mikoani kuanza kuwasaka wajanja hao wa kazi za wasanii," alisema Msama.

Msama aliwataka wajanja walioanza 'kuchakachua' kazi za albamu hiyo ya Haleluya Colletion, kuacha mara moja kabla hawajakamatwa na maofisa hao walioenea Dar es Salaam kwa sasa. Alisema kutokana na kazi za Haleluya Collection na albamu nyingine zilizotolewa na kampuni hiyo kuanza kudurufiwa na wajanja, tayari wamepata taarifa kutoka sehemu mbalimbali kuwa wapo 'wachakachuaji' wa albamu hizo wanaoziuza mitaani kwa bei poa.

Mkurugenzi huyo alisema albamu halisi ya Haleluya Collection ina kasha gumu ambalo halipo katika mfuko wa nailoni, tofauti na zile ambazo zinatengenezwa na wajanja wachache hivi sasa.
"Tayari tumetoa namba zetu za 0786 383838 kwa watu mbalimbali ili kufanikisha urahisi wa kuwabamba wajanja hao… pia tutatoa zawadi ya kati ya sh. 100,000 hadi sh. milioni 1 kwa atakayefanikisha kupatikana kwa 'wachakachuaji' hao," alisema Msama.

Alisema kazi hiyo ya maofisa wa Msama Promotions kuwasaka wachakachuaji hao itafanyika nchi nzima na hivi sasa wameanza na Dar es Salaam kabla ya kuhamia mikoa mingine. Albamu ya Haleluya Collection ilizinduliwa hivi karibuni wakati wa tamasha la Pasaka lililofanyika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, May 29, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Man u waibuka kidedea tamasha la serengeti fiesta bonanza mkoani Tanga

Timu ya mabingwa wa Mwendelezo wa Msimu Dhahabu unaoendelea na Serengeti Soka Bonanza Mkoani Tanga mashabiki wa Manchester United wakiinua juu kombe lao, mara baada ya kushinda katika mchezo uliowakutanisha dhidi ya wapinzani wao wa kweli timu ya mashabiki wa Barcelona mkoani humo na Barcelona kufungwa kwa penati tatu kwa moja baada ya kutoka suluhu katika dakika za kwaida kwenye bonanza lililofanyika leo kwenye uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga.Mashabiki wa Man U wakiwa wamemnyanyua mmoja wa wachezaji wao mara baada ya kufunga mkwaju wa penati na kuwa ndio mwisho wa mashabiki wa timu ya Barcelona,mchezo huo umefanyika leo kwenye bonanza la Serengeti Fiesta Soka, uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Mchezaji wa mashabiki wa Man U akimtoka mchezaji wa timu ya Barcelona.
Uwanja wa Mkwakwani leo ilikuwa ni vute nikuvute,kwani bonanza lilionekana kunoga na kuwavutia mashabiki wengi wa vilabu vya nje hapa nchini,kiasi cha kujitokeza kwa wingi kwenye bonanza hilo la Serengeti Fiesta soka bonanza,ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Mashabiki wa vilabu vya nje nchini,timu ya Barcelona wakiwa na kikombe chao mara baada ya kuibuka nafasi ya pili katika tamasha la Serengeti Fiesta Soka Bonanza lililofanyika leo kwenye uwanja wa Mkwakwani,mkoani Tanga na kuhudhuriwa na wakazi kibao wa mji huo.
Mashabiki wa Bwawa la Maini wakishangilia timu yao ilipokuwa ikibinjukwa uwanjani
Wafuasi wa timu ya Arsenal nao hawakuwa nyuma na masha sham yao.
Mmoja wa wasanii kutoka kundi la Bai Koko la Mkoani Tanga,akionesha manjonjo yake ya kupuliza filimbi kwa mtindo wa kipekee kabisa na kupata mlio uliokuwa ukiburudisha vilivyo kwa washabiki wa bonanza hilo.

Pichani juu na chini ni baadhi ya mashabiki mbalimbali wa vilabu vya nje nchini waliojitokeza kwa wingi leo ndani uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga,katika tamasha la kuisaka timu itakayoibuka kinara katika msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta Soka Bonanza katika mkoa wa Tanga.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, May 29, 2011 | | Permalink | Maoni 1
Idadi ya watu