




UKUMBI WA DIAMOND WAANDALIWA TAYARI KWA MAONYESHO YA HARUSI 2011 YANAYOTARAJIWA KUANZA KESHO TAREHE 1 MPAKA 3 MWEZI APRIL.
Maandalizi motomoto ya Maonyesho harusi kwa mwaka 2011 yanaendelea mchana huu ndani ya ukumbi wa Diamond , huku washiriki wakimiminika ukumbini hapo ili kuhakikisha mabanda yao, na kila kitu kiko sawa.
Hatua za mwisho za maandalizi ya ukumbi huo uliopambwa kwa mabanda ya rangi nyeupe na mazulia mazuri ya kibuluu, inaufanya ukumbi huo kung'aa na kuuweka tayari kwa maonyesho hayo yanayoanza kesho tarehe 1 hadi 3 mwezi April.
Haya ni maonyesho ya aina yake, yanayochukua sura ya kimataifa huku yakitarajiwa kutembelewa na viongozi mbalimbali toka serikalini na sekta binafsi.
Kwa kweli si maonyesho ya kukosa kwa wadau na wale wote wanaotarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
Baadhi ya washiriki wa maonyesho wa mwaka huu ni: Lotus Creative Concepts, Nadd House Events Hire, Zanzibar Weddings, Fannina Investments, Endepha Events Planners,Luxe Papers, Paper Designs, Vayle Springs, Upper Zonal Trading, River Blues Tanzania Ltd, MH Gallery,Kinara Mobile Studio, Dar City, Slice of Wedding,Markham Executive Suites,The Flying Chefs, Mustafa Hassanali Wedding, Malaika Event Designs & Rentals, GRM Production, Bluecheriemoe, DIA’s, Metro Fashion, Rose Fashion Designer, TANZANIA HAIR INDUSTRY, NORBROS Collection, Manju Msitta, Caros Cakes& Hot Brades, Moevenpick Royal Palm Hotel, Sheer Illusion and Daily News, nk.
Maonyesho ya Harusi kwa mwaka huu yamedhaminiwa na Clouds FM, Daily News, Habari Leo, Global Outdoor Systems, Image Masters, Ultimate Security, Vayle Springs, Eventlites na 361 degrees.

Habari Bro Michuzi Jr .
Tunashukuru sana kwa kuwekea tafiti yetu kwenye blog yako. Leo ndio ile siku ya kutangaza matokeo. Chini ni ujumbe unaoambatana na link ya kwenye maoni. Pia tumeattach picha ambayo unaweza kuambatanoisha na hii post. Tunatanguliza shukrani mkuu.
..............................
MATOKEO : MAONI YA WATU KUHUSU TIBA YA BABU LOLIONDO
Kwa niaba ya Bongo Promotions tunapenda kutoa shukrani zetu kwa wale wote walioshiriki katika survey tuliyoitangaza siku ya jumatatu (28.03.11). Lengo la kufanya huu utafiti mdogo ni kuangalia mitizamo ya wananchi kuhusu tiba ya babu Loliondo.
https://spreadsheets0.google. Tunashukuru kwa ushirikiano wako BONGO PROMOTIONS Team
Tumepata maoni mengi sana kutoka kwa watu zaidi ya 180. Takwimu zinaonyesha wengi wamependekeza kwamba taratibu za kitaalam zifanyike kuthibitisha kama dawa inatibu, wengine wanasema kuwa hili ni suala la imani zaidi. Wapo walio fedheheshwa na juhudi za vingozi kutokuwa za kuridhisha katika kufuatilia suala hili na badala yake wao kuwa ni miongoni wa wanaojitokeza kwenda kupata kikombe. Unaweza kupata maelezo zaidi na report kamili ya hii tafiti ndogo kupitia link hiyo hapo chini.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI APRILI MOSI 2011
Tarehe Mosi Aprili kila mwaka ni SIKU YA TAIFA YA KUPANDA MITI. Maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupanda Miti yalifanyika kwa mara ya kwanza tarehe Mosi Januari mwaka 2001 kutokana na Waraka wa Waziri Mkuu Namba 1 wa mwaka 2000 uliomtaka kila mwananchi kupanda miti kwa manufaa yake.
Kutokana na kiwango cha uponaji wa miti iliyopandwa kuwa kidogo, yaani kati ya asilimia 50 na 60 hasa kwenye maeneo kame kinachosababishwa na kupungua kwa mvua na athari za tabianchi, Waziri Mkuu alitoa Waraka mwingine Namba 1 wa Mwaka 2009, uliobadilisha Siku ya Taifa ya Kupanda Miti kuwa tarehe Mosi Aprili kila mwaka badala ya Januari Mosi. Mwezi Aprili ni mwezi ambao sehemu nyingi nchini zinapata mvua, hivyo ni wakati muafaka wa upandaji miti.
Mwaka jana Siku ya Taifa ya Kupanda Miti iliadhimishwa kitaifa Aprili Mosi kwa mara ya kwanza mkoani Shinyanga. Mwaka huu maadhimisho haya yatafanyika katika ngazi za mikoa yote nchini.
Kiutaratibu tarehe Mosi Aprili ni siku ya uhamasishaji pamoja na kupanda miti michache kama sehemu husika haitakuwa na mvua za kutosha. Kama kawaida, kila Mkoa umepanga siku maalum ya kupanda miti mingi zaidi kufuatana na majira ya mvua kwenye Mkoa husika.
Kwa mfano, Mkoa wa Pwani umepanga kupanda miti tarehe 15 Aprili, 2011. Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Makao Makuu watajiunga na wananchi wa Mkoa huo wakati watakapokuwa wanapanda miti katika msitu wa Kazimzumbwi Wilayani Kisarawe.
Maadhimisho ya mwaka huu ni ya pekee kwa maana ni mwaka ambao umetangazwa na Umoja wa Mataifa kama Mwaka wa Kimataifa wa Misitu. Ni mwaka wa kutafakari mchango wa watu wa mataifa yote katika kuilinda misitu na kuitumia kiuendelevu. Ni mwaka wa kuhamasishana kuendeleza uhifadhi na kupanda miti ili misitu iwanufaishe watu wa kizazi hiki na vizazi vijavyo. Kwa hiyo, mwaka huu tutaitumia tarehe Mosi Aprili kuadhimisha Siku ya Taifa ya Kupanda Miti, pamoja na Mwaka wa Kimataifa wa Misitu.
Tukumbuke pia kuwa huu ni mwaka wa kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Hivyo, tutaadhimisha siku hii kwa kutathmini tulikotoka, tulipo na tunapokwenda kuhusiana na hali ya misitu. Kila mmoja wetu anatakiwa atathmini athari anazopata kutokana na ufyekaji na uharibifu wa misitu na kuamua kwa dhati kuhifadhi misitu, miti iliyopo nje ya misitu na kuongeza jitihada za kupanda kwa wingi miti ya asili na ya kigeni.
Sera ya Taifa ya Misitu imeweka umuhimu mkubwa katika kuhifadhi na kulinda misitu. Sera hii inahimiza ushiriki wa wananchi na wadau wengine kuihifadhi misitu iliyopo na kupanda miti na kuitunza.Nachuku fursa hii kuwapongeza wananchi ambao wanastawisha miche ya miti bila kutegemea ile inayostawishwa katika bustani za serikali. Kwa sasa asilimia 70 ya miche ya miti yote inayopandwa inatokana na juhudi za wananchi wenyewe wanaoanzisha bustani ndogo zinazomilikiwa na vikundi vya kinamama, vijana, asasi zisizo za serikali, shule, na watu binafsi.
Ili kufanikisha upandaji mti nchini napenda kutumia fursa hii kutoa wito kuwa kila familia ianzishe bustani ndogo yenye miche angalau inayolingana na idadi ya wanafamilia. Kwa kufanya hivyo, ni rahisi kuitunza miche hiyo kwa kutumia maji yanayotumika nyumbani. Na pale inapowezekana, ni vema familia zianzishe bustani kubwa kwa ajili ya biashara hivyo kuwawezesha wananchi wengi kupanda miti.
Wakati mwingine siyo lazima miche yote inayopandwa itoke bustanini. Njia nyingine ya kustawisha miti ni kutumia miche inayojiotea yenyewe ardhini kama maotea. Miche hiyo inapandwa katika sehemu zilizokusudiwa ikiwa bado midogo. Njia hii inatumika hasa kwenye sehemu zenye mvua nyingi na udongo tifutifu.
Njia nyingine ya kuongeza kiwango cha upandaji miti ni kupanda mbegu moja kwa moja ardhini kwa baadhi ya miti. Njia hii inatumika sana katika mikoa iliyoko katika nyanda za juu hapa nchini. Kwa mfano wakulima wa miwati katika mikoa ya Tanga na Iringa wanapanda mbegu moja kwa moja ardhini. Aidha, mikaratusi pia inaweza kupandwa kwa njia hii.
Aina nyingine ya kustawisha misitu ni kutenga na kulinda eneo kutokana na uharibifu wa kimazingira ili mbegu ziote zenyewe (yaani natural regeneration). Njia hii imefanikisha shughuli za kustawisha misitu na malisho ya mifugo mkoani Shinyanga. Wananchi wa Shinyanga wanatumia utaalam wao wa jadi unaojulikana kwa jina la Ngitili wa kutenga maeneo na kuyapumzisha ili mbegu zijiotee zenyewe. Matokeo yake ni eneo husika kubadilika na kuwa msitu.
Ustawishaji misitu kwa kutumia njia ya Ngitili umewawezesha wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuongoa zaidi ya hekta 500,000 za ardhi ambayo ilikuwa imeharibika kabisa hapo awali. Kutokana na uzoefu huo, nawaasa wananchi kutumia njia zao za jadi za kustawisha misitu na miti kwenye maeneo yao.
Napenda kuwakumbusha na kuwahimiza kuwa kila mmoja wetu aitunze miti atakayoipanda kwa kuilinda dhidi ya uharibifu wa aina yoyote. Aidha, napenda kuchukua fursa hii kumhimiza kila mwananchi ajenge utamaduni wa kuitumia rasilimali ya misitu kwa njia endelevu kwa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria za kuvuna mazao mbalimbali ya misitu.

Je, unamjua Amanda Annan? Amanda ni British Super Model na katika ulimwengu wa ulimbwende anajulikana kama ‘Rebel Niece’, kwa sababu yeye Amanda (Kofi Atta Annan (baba mdogo wa Amanda) ni mdiplomasia toka Ghana ambaye ni mtu wa 7 kuitumikia cheo cha Secretary-General wa United Nations kuanzia 1 January 1997 mpaka 31 December 2006.) amezaliwa kwenye familia ya wasomi, wanasiasa na madiplomasia, lakini alipotimiza umri mdogo wa miaka 17 akajikita kwenye fani ya mitindo, uigizaji na ulimbwende tofauti na matarajio ya wazee wake.
Amanda aliliona jarida la Shear Magazine akiwa matembezini Marekani kwa rafiki yake ambaye in dada yetu wa Kibongo aitwaye Pendo Nyonyi anayeishi Los Angeles. Agent/manager wake akapenda wazo la Amanda kutupatia nasi historia yake kwa ufupi na kuwapa moyo kina dada wa Kibongo mbinu za kujikita katika ulimbwende na kutokukata tamaa katika kufanya kile kitu ambacho moyo unapenda, na pia anaeleza kwa kina kuwa mafanikio hayaji bila kujituma, uvumilivu na ujuzi pia.
Pata nakala yako ya Toleo jipya la Kumi maana liko mitaani sasa uweze kusoma story ya kusisimua ya Amanda, kazi zake alizofanya za kuisaidia jamii ya wanawake Afrika, siri zake za urembo, utunzaji wa mwili, ngozi na nywele. Pia ndani ya toleo hili, utapata kujua historia fupi ya 'Legend' Issa Michuzi katika page maalum ya brothers, mahojiano na Ankal Michuzi amewapa wasomaji historia yake ambayo watu wengi hawaijui na yeye binafsi hajazitoa katika blog yake. Nunua nakala yako sasa kwa TSh.5,000 tu!
In general, Rakesh’s experience is extensive in the East African development sphere, ranging from progressive and community-driven media and telecommunications campaigns, to the assessment of learning across public schools. It is therefore with deep enthusiasm and interest that we, at Vijana FM, took this opportunity to interview Rakesh.
Famili ya marehemu Alhaji Juma Sindano wa Makumbusho Dar es Salaam. Inatoa shukrani kwa wote walishirikiana nasi kwa namna moja au nyingine kutoka ugonjwa hadi kifo chake shukrani za pekee ziwaendee Prof Mgonda wa Muhimbili Hospitali, Hospitali ya Agha Khan, Dr, Kanabal wa Regency Hospital, kwa kutaka kuokoa maisha ya marehemu baba yetu mpendwa, Mh. Rais Jakaya Kikwete, viongozi wote wa chama na Serikali, wafanyakazi wa Gapco Tanzania Ltd, Wafanyakazi wa MGS Ltd, Wafanyakazi wa Riki Hill Hotel, Wafanyakazi wa Wizara ya Afya Kitengo cha Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma,Majirani zetu wa makumbusho, ndugu jamaa na marafiki si rahisi kumshuru kila mtu mmoja mmoja tunaomba shukurani zetu za dhati wote mlioshirikiana nasi katika kipindi hiki kigumu.
Hatuna cha kuwalipa mwenyezi mungu ndie atakae walipa
Wainnalilah Rajuhuni
Arobaini ya marehemu itafanyika tarehe 2/04/2011 saa 7 mchana nyumbani kwake Makumbusho Dar es Salaam.
Wote mnakaribishwa.
Mwandishi na mtafiti wa masuala ya kijamii Bwa.Chambi Chachage akizungumza na Dr Emmanuel Kandusi mapema leo mara baada ya kumaliza kuzungumza mjadala wa kusaka jibu kuhusiana na mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiibuka hivi karibuni ikiwemo masuala ya “KIKOMBE”.
Kipindi cha Power Breakfast leo asubuhi kimeendesha live, mjadala wa kusaka jibu kuhusiana na mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiibuka hivi karibuni ikiwemo masuala ya “KIKOMBE”.Mjadala huo umefanyika ndani ya hoteli ya Kilimanjaro Kempinsk,jijini Dar.

Mukubwa ni mlemavu wa mkono mmoja wa kushoto anaodai umekuwa katika hali hiyo kutokana na kudhuriwa kwa uchawi na mama yake wa kambo alipokuwa na umri mdogo.Speaking at a Business Networking meeting in Dar es Salaam yesterday, Ambassador Clarke said that given its geographic location Tanzania has potential to serve as a gateway to the East African region.
He therefore urged European businesses to see to it that they fully utilize the opportunity for their benefit and that of the country and the EA region as a whole."Implementation of the EAC Common Market, as it evolves, will bring increasing trade and investment opportunities for EU businesses," he said.
The EU, with its Member States, is not only the largest development partner of Tanzania, but EU companies also bring significant investment to Tanzania, Ambassador Clarke said.The Business Networking meeting, which aimed to provide a platform for European business representatives to meet and exchange views on challenges and opportunities of doing business in Tanzania, was organised by the EU Delegation and EU Member States present in Tanzania.
Enlisting achievements made so far, Ambassador Clarke said that institutionally the EU was engaged in several processes aimed at facilitating EAC integration including Economic Partnership Agreement (EPA) negotiations and support programmes to EAC integration.
"In future," he said, "we are seeking to be in more active communication with the business community in East Africa-through the East African Business Council, and at a country level."The EU Head of Delegation also said that EU had initiated a dialogue with the Tanzania Revenue Authority where they had agreed on 13 points of action relating to clarity and transparency of tax regulations such as audit process and the open-ended nature of the TRA interventions.
As a result of the dialogue, Ambassador Clarke revealed, TRA has agreed to invite EU business representative to become a member of their stakeholder consultative meeting which until now has been including only sectoral and national representation. The EU business community is keen to contribute to the policy and regulatory debate and to provide feedback on the ongoing reform process.
Serengeti Breweries Limited (SBL), through its iconic premium Scotch whisky Johnnie Walker conducted the second Johnnie Walker Mentorship Program today. The Johnnie Walker Mentorship mentoring and tasting session is an opportunity to immerse the guests into the unique and sophisticated world of the Johnnie Walker and give them an appreciation of what each of the different variants of the brand is made from, how it is made, how to drink it and in what occasions. This unique journey was seen in the last two sessions, and will be seen through by two trained Johnnie Walker mentors Gerald Hando and Dennis Ssebo. They took the invited guests through the journey of taste in the cool and classic environment of the Kibo ball room Kilimanjaro Kempinski-Dar Es Salaam.
According to the Spirits manager at SBL, Benjamin Mariki, “Johnnie Walker has become more than just a drink. It is something we can all relate to in terms of how far we each have come in our lives; in business, socially and at our jobs, today we come together to celebrate personal achievement and progression.’
The mentorship took guests through Johnnie Walker’s journey right from the brewery to one’s glass, a process that has been appreciated for more than 150 years. The Marketing Director of SBL, Ms. Caroline Ndungu said “As part of Diageo Inc, Serengeti Breweries (SBL) is now the official distributor of the whole range of the House of Walker brands,”
The Johnnie Walker Mentorship Program commenced on the 10th of March at Mlimani City Conference centre and will continue all through till the end of June. In the coming months, the striding man will be paying visits to different cities around Tanzania including; Arusha, Mwanza and Tanga to share the Johnnie Walker experience with a few of the lucky invites in their respective cities.
Bendi ya Mashujaa inatarajia kufanya onyesho lake katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam ifikapo Aprili mosi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika jijini Dar es Salaam kiongozi wa bendi hiyo Edward Antony almaafu kwa jina la Jadoh FFU kuwa wanatarajia kufanya onyesho lao katika kijiji cha Makumbusho kwa kushirikiana na Kundi la Mapacha Watatu.
"Nawakaribisha sana ndugu zetu wote waje watuunge mkono maana tutafanya onyesho zuri sana ambalo wao wenyewe wanadhihirisha sisi ni wakali, Alisema kiongozi wa kundi hilo.
Onyesho hilo ambalo litaendana na utambulisho wa wasanii wao wapya ambao wanatarajia kutambulisha wapatao saba na kiingilio kitakuwa ni tshs.7,000/=

……W’re polite and progressive by day, more tibalist than even the Kenyans by night…..
Ukweli kama huu anaoweza kuusema Jenerali Ulimwengu ndio umewafanya watawala wengi kumwogopa mwanaharakati huyu kushinda hata UKIMWI, nani nchi hii asiyemfahamu Jenerali Ulimwengu? Licha ya mwandishi huyu kukumbwa na misukosuko hata ya kutaka kunyang’anywa uraia aah wapi Bwana! Jenerali Ulimwengu hana mpinzani kwa jinsi anavyosimamia ukweli.
Pengine kwa waandishi wachanga wenye lengo la kufika alipofika Jenerali waanze mapema kukataa rushwa ambazo huwafanya kutumia kalamu zao kusifia uharamia kuliko kukosoa utawala mbovu, Alleluya Mungu Mwenyezi kwa kutupatia Jenerali Ulimwengu mwenye uwezo wa kuwasemea masikini wan chi hii, mwenye uwezo wa kukemea udini na ukabila , mwenye uwezo wa kumhoji hata rais bila uwoga nani kama Jenerali?
Naam Jenerali Ulimwengu ni bakora ya watawala acha iwachape tu!
Nani kama jenerali, Ulimwengu tumwone
Nani anayetujali, yu wapi tusemezane
Nani tumpe kibali, ukweli akawachane
Jenerali Ulimwengu, kiboko ya watawala.
Wamesuka njama nyingi, zote zimegonga mwamba
Jenerali ndio kingi, wanyonge tunampamba
Wanaoweka vigingi, hao wote ni mafamba
Jenerali Ulimwengu, bakora ya watawala
Nani asiyefahamu, Jenerali ni shujaa
Yu wapi tumuhukumu, kwa kuzidi kuzubaa
Jenerali ni muhimu, Arusha hata kondoa
Jenerali Ulimwengu, sindano ya mabwenyenye
Wakiwa maofisini, watawala wanalia
Wakisoma gazetini , hofu inawaingia
Kwa Jenerali makini, Mwema Raia sikia
Jenerali Ulimwengu, msome Raia Mwema
Beti tano nakomea, mengi nimeongelea
Ulimwengu endelea, uovu kuufunua
Ukweli tunaujua, wewe unatutetea
Jenerali Ulimwengu, mtetezi wa wanyonge.
Nova Kambota Mwanaharakati,
0717-709618 au 0766-730256
Tanzania, East Africa
Jumatano 29 March 2011.