nyumba inapangishwa

Monday, February 28, 2011
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, February 28, 2011 | | Permalink | Maoni 2

mashindano ya masumbwi klabu bingwa taifa yafunguliwa.

Bondia wa Mkoa wa Ilala Edward Jackson (kulia) akioneshana kiwango cha kutupa masumbwi na Mohamedi Abdalah wa Arusha wakati wa mashindano ya klabu bingwa Taifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa ndani wa taifa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.(Picha na Mpiga picha Wetu).
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, February 28, 2011 | | Permalink | Maoni 1

wasanii wa muziki na filamu wachangia mil 76 waathirika wa mabomu gongo la mboto.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akicheka kidogo na msanii wa maigizo,ambaye ni maarufu sana kwa jina la Dude katika igizo lake lililojizolea umaarufu sana liitwalioBongo Land,ambapo msanii huyo alikuwa akiigiza kama tapeli na kuwaliza wakazi wengi wa jijini Dar na kwingineko.Mh Pinda alionekana kuvutiwa na kazi yake ya usanii kiasi hata ya kumtania kidogo mbele ya hadhara.
Msanii mahiri wa kizazi kipya Hamis Mwinyijuma a.k.a Mwana FA (kwa niaba ya wasanii wenzake wa muziki na Filamu) akiikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu,Mizengo Pinda leo mchana,ikiwa ni sehemu ya kuchangia waathirika wa Mabomu katika eneo la Gongolamboto jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pomoja na Wasanii wa Muziki na Filamu mara baada ya kuwasilisha michango mbalimbali ya fedha na vitu vyenye thamani ya shilingi milioni 76 waliyoipata kutokana na tamasha walilolifanya mwishoni mwa wikend kuchangia waathirika wa Mabomu katika eneo la Gongolamboto jijini Dar es salaam.Kulia ni Kaimu Mkuu wa mkoa Dar es salaam,Mh Sadik na kushoto ni Kamanda Kova,wa tatu kushoto ni Mratibu Mkuu wa tamasha la Wasanii na Filamu lililofanyika mwishoni mwa wikend,Bwa.Ruge Mutahaba.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, February 28, 2011 | | Permalink | Maoni 0

serengeti breweries yatoa msaada wenye thamani ya sh mil 15 kwa waathirika wa mabomu gongo la mboto jijini dar leo.

Waziri Mkuu,Mh Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mapunda mara baada ya kukabidhi misaada hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mapunda akipeana mkono na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda mara baada ya kumkakabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 15 mapema leo Ukonga jijini Dar,msaada huo ikiwemo Mabati 300,Cementi 300,mashuka 200 pamoja na vyandarua 200 vyote vikiwa ni kwa ajili ya kusaidia waliothirika na milipuko ya Mabomu iliyotokea hivi karibuni,Gongo la Mboto,jijini Dar.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mapunda akikabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 15 kwa Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda (pichani kulia) mapema leo Ukonga jijini Dar,msaada huo ikiwemo Mabati 300,Cementi 300,mashuka 200 pamoja na vyandarua 200 vyote vikiwa ni kwa ajili ya kusaidia waliothirika na milipuko ya Mabomu iliyotokea hivi karibuni,Gongo la Mboto,jijini Dar.
Kamanda kanda maalum ya Kipolisi ya Dar Es Salaam,Afande Suleiman Kova akizungumza na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),mapema leo,Ukonga jijini Dar.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Mh.Sadik Mecki Sadik akisalimiana na Kamanda kanda maalum ya Kipolisi ya Dar Es Salaam,Afande Suleiman Kova mara baada ya kuwasili leo mcha kwa madhumuni ya kuikabidhi taarifa rasmi kwa Waziri Mkuu kuhusiana na mchakato mzima wa milipuko ya Mabomu,Gongo la Mboto,pichani kati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano, kutoka Serengeti Breweries (SBL) Teddy Mapunda na kulia mwisho ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Mh Jordan Lugimbana.
MKurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mapunda akizungumza na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media,Bwa.Reginald Mengi mapema leo nje ya ofisi ya katibu Mtendaji Kata ya Ukonga,kabla ya kuwasili kwa Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda eneo hilo kwa ajili ya kupokea taarifa rasmi ya waathiriwa na milipuko ya Mabomu kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Mh.Sadik Mecki Sadik, iliyotokea kwenye kambi ya jeshi,Gongo la Mboto hivi karibuni na pia kutembelea sehemu mbalimbali zilizoathiriwa na milipuko hiyo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, February 28, 2011 | | Permalink | Maoni 0

ajishindia nisan hardbody kwenye droo ya bahatika na tigo

Wa kwanza kulia anaejiandaa kupiga simu kwa mshindi ni Afisa Uhusino wa Tigo, Jackson Mmbando. droo imechezwa leo na Jacqueline Mambo kutoka Kilimanjaro aliibuka mshindi wa Nisan hardody yenye thamani ya sh 59milioni.
Katikati ni Bw Cannon Luvinga moja kati ya washindi wa wiki iliyopita wa promosheni ya Bahatika na Tigo akibonyeza kitufe cha kompyuta ili kumchagua mshindi wa tatu wa gari wa promosheni hiyo,anaefuata kushoto ni Hemedi Abdala Mkaguzi toka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania akisimamia droo hiyo na anaefuata ni Afisa wa Tigo huduma za ziada Pamela Shelukindo.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, February 28, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Balozi wa Iran Nchini Tanzania amtembelea waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akisalimiana na Balozi wa Iran Nchini Tanzania Bw M Movahhedi Ghomi wakati alipofika Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli kujadili Maandalizi ya Mkutano wa Mkataba wa Kuhifadhi ardhi Oevu utakaofanyika Nchini Iran[Picha na Ali Meja].
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, February 28, 2011 | | Permalink | Maoni 0

Rais wa Zanzibar ,Dr Shein awaapisha, Makatibu na Naibu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akimuapisha Said Hassan Said kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu na Naibu Mwanasheria Mkuu na Naibu katibu wa Rais, baada ya kuwaapisha leo Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman, IKulu Zanzibar.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, February 28, 2011 | | Permalink | Maoni 0

BREAKING NEWS:wanafunzi chuo cha IFm wagoma asubuhi hii.!


Pichani ni Wanafunzi wa chuo cha IFM,wakiwa wamekusanyika leo asubuhi ndani ya uwanja wa chuo hicho,wakiwa na mgomo wa kwa kile walichodai kupinga wanafunzi wenzao kuzuiwa kufanya mitihani kwa sababu tu hawakumaliza kulipa ada ya semester ya kwanza

Aidha imeelezwa kutoka kwa wanafunzi hao pia kuwa kugoma kwao ni kupinga uonevu na mfumo mbovu unaofanywa na chuo hiko kwao wakati serikali ilishaweka wazi kuwa hakuna na marufuku kwa wanafunzi wa vyuo vya umma kuzuiwa kufanya mitihani
== ==== ===
Haya Wadau habari ndio hiyo asubuhi hii ndani ya chuo cha IFM,tutazidi kupeana taarifa kwa kadiri zitakavyokuwa zikipatikana.

Wanafunzi wa Chuo cha IFM,jijini Dar wakiwa wamekusanyika asubuhi hii kwenye moja ya sehemu ya wazi ya chuo hicho kwa madhumuni ya kuanzisha mgomo wa kupinga wanafunzi wenzao kuzuiwa kufanya mitihani kwa sababu tu hawakumaliza kulipa ada ya semester ya kwanza.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, February 28, 2011 | | Permalink | Maoni 2

chadema watinga ndani ya butiama,wakutana na mama maria nyerere.

Sunday, February 27, 2011


Mama Maria Nyerere akiteta jambo na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, wakati viongozi wa Chama hicho na baadhi ya wabunge, walipomtembelea nyumbani kwake Butiama hii leo.
Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), akiweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, wakati viongozi na baadhi ya wabunge wa chama hicho, walipomtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Butiama leo. (Picha na Joseph Senga)
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akitoa salamu za chama hicho kwa Familia ya Mwalimu Nyerere, wakati vongozi mbali mbali na wabunge wa chama hicho, walipomtembela Mama Maria Nyerere (katikati) nyumbani kwake Butiama leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa.Picha kwa hisani ya Joseph Senga.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 27, 2011 | | Permalink | Maoni 3

wadau msaada kwenye tutazzz.!

Kaka inakuaje?

Hebu nisaidie kunijulisha kwa wadau kuhusu ufahamu wa nitakapopata vifaa vya kutengezea mikate kama Mixer yenye uwezo wa kukanda Kilo 25 kwa wakati na Bread Oven yenye uwezo wa kuhifadhi mikate 60 na zaidi kwa wakati.

Kwa wadau watakaopata maelezo ya jinsi ya kupata vifaa hivyo iwe hapa TZ au nje ya nchi na viwe used ama vipya kwangu bongo tambarare tu,tafadhali wawasiliane nami kupitia

HASSAN MBILILI
+255 715 251148
mail:hmbilili@yahoo.com
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 27, 2011 | | Permalink | Maoni 1

ARTI-TZ YAKABIDHI TAA ZA SOLA KWA WAHANGA WA GONGO LA MBOTO


Mkurugenzi wa Appropriate Rural Institute Technology-Tanzania (ARTI-TZ), Bw. Nachiket Potnis (kulia) akimkabidhi mwakilishi kutoka Clouds Media Group Bw. Cathbert Kajuna msaada wa taa za sola 100 zenye thamani ya shilingi milioni 5 zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya wahanga wa milipuko wa mabomu iliyotokea huko kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto,jijini Dar. Msaada huo wa taa za sola aliukabidhi leo katika ofisi za Clouds Media Group zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo taa hizozinatarajiwa kupelekwa kwa wahanga hao kesho jumatatu.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 27, 2011 | | Permalink | Maoni 2

Precision Air yadhamiria kutoa huduma bora kwa wateja wake .

Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Precision Air, ALFONSE KIOKO (kulia) akimwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Stanbic Bank Bashir Awale sare na mavazi mapya yatakayotumika kuanzia sasa ambayo yana gharama ya shilingi milioni 300 wakati wa hafla ya utambulisho iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Precision Air, ALFONSE KIOKO akizungumza jambo na baadhi ya wateja wa kampuni hiyo walioalikwa wakati wa hafla ya utambulisho wa sare na mavazi mapya yatakayotumika kuanzia sasa ambayo yana gharama ya shilingi milioni 300 iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Precision Air, ALFONSE KIOKO akizungumza jambo na baadhi ya wateja wa kampuni hiyo walioalikwa wakati wa hafla ya utambulisho wa sare na mavazi mapya yatakayotumika kuanzia sasa ambayo yana gharama ya shilingi milioni 300 iliyofanyika jijini Dar es Salaam

Wasanii wa kikundi cha Splendid Art Group wakionesha umahiri wao katika mitindo tofauti ya sarakasi wakati wa hafla ya utambulisho wa sare na mavazi mapya yatakayotumika kuanzia sasa ambayo yana gharama ya shilingi milioni 300 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, February 27, 2011 | | Permalink | Maoni 6
Idadi ya watu