kilimanjaro stars yaibanjua somalia 3-0 CECAFA Tusker Challenge Cup 2010.

Tuesday, November 30, 2010
Mie nikiwa na Injia wa Blog zote zenye nembo ya MK,Kamanda Christofa ambaye kwa sasa yupo Bongo pamoja na kamanda wa Mtaa kwa Mtaa, sote tulikuwepo uwanjani kuonyesha uzalendo kwa timu yetu ya Kilimanjaro Stars ambayo imeinyuka timu ya Somalia goli 3 kwa 0 katika michuano ya CECAFA Tusker Challenji Cup 2010.

Ilikuwa patashika uwanja wa taifa leo.
nyomi la watu ambapo leo na mpaka jumamosi wameruhusiwa kuingia bure.
Majeruhi wa Somalia akitolewa uwanjani.
Mchezaji wa Kilimanjaro Stars akiwa amelala chini baada ya kugongana vibaya na mchezaji wa timu ya Somalia.
Refa akiwaelekeza jambo wachezaji wa Somalia.
Mchezaji wa Kilimanjaro Stars akijaribu kumchomoka mchezaji wa timu ya Somalia
Umati wa watu kutoka kila pande ya jiji la Dar lilijitokeza leo jioni kuishangilia vilivyo timu ya Taifa ya Tanzania Kilimanjaro Stars,ambapo timu hiyo imefanya kweli leo na kuwaletea raha upya Watanzania kwa kuibanjua timu ya Taita ya Somalia magoli 3 kwa 0,kwenye mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge Cup 2010.

Goli la kwanza limefungwa na mshabuliaji kiungo wa timu ya Taifa anayecheza mpira wa kulipwa nchini Sweden Hery Joseph alpofunga goli kwa njia ya penati, goli la pili limefungwa na mchezaji John Boko na goli la tatu lilitingwa kimiani na mshambuliaji Mrisho Ngasa.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 30, 2010 | | Permalink | Maoni 2

Bohemia presents Freshly Ground

(South Africa) & Deodato Siquir (Mozambique).

Freshlyground

Shakira ft. Freshlyground - Waka Waka (This Time for Africa) (The Official 2010 FIFA World Cup Song) - http://www.youtube.com/watch?v=pRpeEdMmmQ0

10% of profits will be allocated to Emusoi Community Centre - Thanks to everyone that bought tickets already...

Tickets available at:
* Novel Idea (Seacliff Village, Slipway, Shoppers Plaza, City Center)
* Moevenpick Royal Palm Hotel
* Alliance Francaise
or call 0655 052010.

Tshs 50,000 in advance, 60,000 at the gate, 100,000 VIP (please enquire for VIP perks)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Urban Pulse Yaandaa party ya shukurani kwa wadau


Utawala wa URBAN PULSE CREATIVE MEDIA Unapenda kuwashukuru wale wote ambao walijitolea kufika, kushiriki na kutoa support ya namna moja au nyingine wakati wa URBAN TOUR ili kusaidia kuchangia fedha za kupambana na vita dhidi ya Malaria Tanzania.

Tour hii ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kuweza kupata publicity duniani kote na kuhamasisha watu mbalimbali ili kutambua umuhimu na namna ya kufanya ili kutokomeza ugonjwa huu kama ambapo kila mtu ataamua kuchukua majukumu na kufanya sehemu yake.

Itakuwa ni vigumu kutoa shukrani kwa kila mtu ila URBAN PULSE ingependa kutoa shukrani za dhati kwanza kabisa kwa Mwenyezi MUNGU ambaye alisaidia kufanikisha tour hii, Ubalozi wa Tanzania hapa UK Pamoja na staff wake,ASET(ASHA BARAKA & BARAKA MSILWA) Bloggers Wote waliosadia kutangaza show yetu ukianzia na MICHUZI,JIACHIE,MISS JESTINA,DJ CHOKA,TZ UK, HAKI NGOWI,GLOBAL PUBLISHERS, ABDALLAH MRISHO,KULIKONI UGHAIBUNI,HUNGA,MASHUGULI,KANUMBA,VINCENT KIGOSI,JENGATZ,MASHUGHULI,TA READING,LADY JAYDEE,MJENGWA,MTAA KWA MTAA,BONGO WIKEND na wengine wote.
TV & RADIO STATION zikiwepo BBC, BEN TV, BET,MTVBASE,AILTV, PRESENTERS: SPORAH, AYOUB MZEE, FRED MTOI, FRED MACHA, SAFINA,IDD SAFE, CHRIS GOLDFINGER NA JJ. MA DJZ; CHAMBI,ASH,ANDREW,10 TONNES,JCOM,MOJA PAMOJA NA CHRIS GOLD FINGER

Hiyo basi Imeandaa party ya kutoa shukrani na kusherekea anniversary ya kwanza ya URBAN PULSE kwa wote jumamosi hii kuanzia 10pm- 4am. DJZ on the deck DJ CHAMBI &ANDREW
4th November 2010
CLUB AMBASSADOR
20 LONDON ROAD
BARKING, 1G11 8AJ


WOTE MNAKARIBISHWA
ASANTENI
URBAN PULSE CREATIVE
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

nmb yachangia mfuko wa TANZANIA 50 PLUS CAMPAIGN PROSTATE CANCER:


Dear Prof. Rebbeck and All,
Greetings from Tanzania!
Today we had a Press Conference at which a local bank National Microfinance Bank (NMB) donated 35,000 pieces worth Tshs. 7.5 ml (USD 5,068) of bochure for Prostate Cancer literacy.

This is a great donation to the campaign.Please drop an email message of appreciation to the National Microfinance Bank (NMB) through Ms. Shyrose Bhanji, Public Relations Officer, NMB shyrose.bhanji@nmbtz.com Attached pictures the lady handing over brochures is Shyrose.
We are very greatful to the bank. We pray that others will follow foot steps. We still need more of such brochures taking into account Tanzania has a population of 43 ml.
I am sharing our joy with you all!
Regards,
Rev. Canon Dr. Emmanuel J. Kandusi
Campaign Coordinator
Tanzania 50 Plus Campaign
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

FFU ! Wa Ngoma Africa band Kuvamia Belgrad,Serbia!




FFU ! Wa Ngoma Africa band Kuvamia Belgrad,Serbia!

FFU wa Ngoma Africa band kupeleka mzimu wa Dansi nchini Serbia ,January 2011

Bendi maarufu ya mziki wa dansi Ngoma Africa band aka FFU,wanatarijiwa kutumbuiza katika mji wa Belgrad,nchini Serbia,ulaya ya mashariki katika maonyesho ya Film and music festival yatakayoanza tarehe 5 hadi 12 January 2011,Pia wakazi wa mji wa Montenegro watavamiwa na mziki huo wa dansi kutoka kwa ffu wa Ngoma Africa band yenye maskani yake nchini Ujerumani.

Ni juzi juzi tu wakali hawa wa mziki wa dansi na "MZIMU WA MZIKI" walikuwa wakipeperusha CD maalum "Jakaya Kikwete 2010" .Toka bendi hiyo ipelekewe mwaliko wa kwenda SERBIA ,wanamziki wa bendi hiyo wamshikwa na matumbo joto! kutokana historia ya nchi ya SERBIA ambayo miaka ya nyuma ilikuwa na vita....Pia ziara ya wakali hao Ngoma Africa band,ndio bendi ya mwanzo ya kiafrika kwenda Serbia
wasikilize hapa www.myspace.com/thengomaafrica pia www.unheardradio.com/The_Ngoma_Africa_band
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 30, 2010 | | Permalink | Maoni 1

tigo yamkabidhi milioni 10 mshindi wa promosheni ya dunia ya washindi leo jijini dar

Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi zawadi ya hundi ya shs milioni 10 kwa mshindi wa jumla wa promosheni ya Dunia ya Washindi, Farijala Athumani Iddi mkazi wa Singida, katika makabidhiano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja Miradi wa Huduma za Ziada (VAS) wa Tigo, Suleiman Bushagama.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

*TANZANIA & KENYA INDEPENDENCE DAY BASH WASHINGTON-DEC 10 & 11*


*TANZANIA & KENYA INDEPENDENCE DAY BASH WASHINGTON-DEC 10 & 11*
=UHURU NA JAMHURI DAY =
**PARTY & LIVE BONGO FLAVA CONCERT***
TANZANIA & KENYAN COMMUNITY IN THE WASHINGTON,DC TUNAWAKARIBISHA
KWENYE INDEPENDENCE DAY CELEBRATIONS-THE EAST AFRICAN INVASION
*****PROGRAM IS AS FOLLOWS******
=DAY ONE= FRIDAY DEC 10=
=MAKAMUZI PARTY=FRIENDS MEET & GREET OUT OF TOWN PEOPLE=
=ARTISTS ARRIVAL/BONGO FLAVA/GENGE
******VENUE=KARMA LOUNGE*@ MAGIC JOHNSON THEATER****
****800 SHOPPERS WAY,LARGO,MD.DOORS OPEN @9PM

==========================================================================
==========================================================================

***DAY TWO PROGRAM***SATURDAY=DEC-11***
***KAMA WEATHER IKIRUHUSU--BBQ @GREENBELT PARK***
***INDOOR BASKETBALL//SOCCER//POOL TABLE COMPETITION****
***NIGHT EVENTS=DOORS OPEN @ 9PM ******
***VENUE***24 NIGHT CLUB,2122-24TH PLACE,WASHINGTON,DC****
***LIVE CONCERT/BONGO FLAVA & KENYAN ARTIST-GENGE FLAVA*** **FEATURING=WAKAZI"SWAGGA BOVU"=CHICAGO***
***AJ UBAO=TANZANIA=DC*****
****VINIE"THE KENYAN BOY"-KENYA***
***DIRTY HERRY=TANZANIA=DC******
***GWAII=TANZANIA=DETROIT
***STANBOI THEAFRICANCHILD=TANZANIA-WICHITA***
***BABU "ALBINO FULANI"=TANZANIA=OH******
***************************************************************************
TWO DAYS==6(SIX)DJS-DJ KAY,DJ KVELLI,DJ TERRY.DJ SMOOTH.DJ ACE,DJ SEIF
INFOS VISIT=WWW.DMKGLOBALPROMOTIONS.COM= CALL 3016616207/8653657766/2406437000
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
==================================================================================
**********DAY THREE=SUNDAY DEC 12=FAREWELL & WASHINGTON DC CITY TOUR********


Dickson M.M

Brand & Marketing Director


301-661-6207 / 865-dmk-prom(365-7766)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 30, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Peacock Hotel yaja na usiku wa mtanzania,kufanyika karimjee desemba 3

Mwanamuziki Mkongwe wa Mlimani Park Ochestra,Hassan Bichuka akitoa vionjo kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo asubuhi katika ukumbi wa Flamingo wa Peacock Hotel.

Pichani kulia ni Meneja Masoko wa Precission Air Emilian Rwejuna, akisisitiza ushiriki wa0 katika tukio la kusheherekea usiku wa Mtanzania pale Karimjee Ground.

Pichani kushoto ni Mkurugenzi Uendeshaji wa ya Hoteli ya Peacock Damas Mfugale akiwakaribisha waandishi wa habari leo asubuhi kwenye moja ya ukumbi wa hoteli hiyo kuhusiana na tukio la usiku wa Mtanzania utakaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar, anaefuatia ni Mwenyekiti wa Peacock Hotel Joseph Mlangila Mfugale, Meneja Masoko wa Precission Air Emilian Lwejuna, Meneja Mahusiano wa Bank ya Posta Noves Moses pamoja na Meneja wa kinywaji cha Konyagi Martha Mwangu. Shoo hii imeratibiwa na kampuni ya 1Plus Communication


Peacock Hotel

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Peacock Hotel ni hoteli inayojali wateja wake kwa kiwango cha juu. Ili kudumisha na kuendeleza mila, desturi, na utamaduni wa mtanzania, hoteli ilianzisha Usiku wa Mtanzania ambapo vyakula vya asili ya Tanzania vinaandaliwa kwa ladha ya asilia. Ni hoteli pekee nchini Tanzania ambayo inadumisha menu halisi ya kitanzania.

Usiku huu unatimiza miaka kumi(10) mwaka huu tangu uanzishwe. Kila Jumatano usiku panakuwepo vyakula vya kitanzania vya aina mbalimbali na makabila mbalimbali. Mandhari ya hotel hugeuka kuwa ya asili ili kuleta maana halisi ya lengo la usiku huu.

Tarehe 3.12.2010 ni siku ya kusherehekea kutimiza miaka kumi ya Usiku wa Mtanzania katika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku.Shamrashamra hizo zitapambwa na ngoma za asili pamoja na muziki kutoka kwa Kidum-Kenya, Lady Jay Dee, Sikinde-Ngoma ya Ukae, na Waane Star. Kiiiingilio kimepangwa kuwa ni sh 40,000/=kwa kila mtu

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu wote ambao wanaendelea kuburudika kwa milo ya kitanzania pamoja na burudani za asili. Kwa kutambua uwepo wao na kuthamini usiku huu tunawaahidi huduma bora zaidi na siku ya sherehe tutawatambua rasmi baadhi yao kwa niaba yaw engine kwa kuwapa zawadi.

Washiriki wenzetu katika kuunga mkono U

siku wa Mtanzania kutimiza miaka kumi ni Benki ya Posta, Shear Illussion, Vayle Springs, na Precision Air. Hawa wanadhihirisha dhamira yao ya kuunga mkono mila na desturi za kitanzania.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mr.Damas Mfugale kwa namba 0789-280112

Asanteni

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Tuesday, November 30, 2010 | | Permalink | Maoni 1

Maalimu Gurumo atoka icu

Monday, November 29, 2010
Mwanamuziki wa siku nyingi Mzee Makasy akimjulia hali mwanamuziki mwenzie Maalimu Muhindini Gurumo (KAMANDA) aliyelazwa hospital ya Taifa Muhimbili,Uncle Gurumo yupo wodi ya Mwaisera namba 1 kwa sasa baada ya kutoka katika chumba cha wagojwa wenye uangalizi maalumu (ICU).Kumradhi kwa picha hazionekani vizuri.Picha kwa hisani ya Rajab Mhamila.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 29, 2010 | | Permalink | Maoni 1

WASANII JITOKEZENI TUPIGE VITA UKIMWI-backyards record.

Napenda kumshukuru Mungu kwa kuendelea kuwa hai mpaka sasa.

Pia nawashukuru watanzania wenzangu kwa kushiriki na kufanikisha uchaguzi wetu mkuu. Masikio yalikuwa hoi sana kusikia habari za uchaguzi uchaguzi mpaka tumehitimisha kwa huru na haki ya kidemocrasia.

Shukrani zangu za dhati kwa media zote kwa kupoteza muda, mali hata kuatarisha afya zao ili hali kuhakikisha ujumbe na kampeni za uchaguzi zinatufikia.

Shukrani za pekee kwa wasanii wote walio shiriki kwa njia moja au ningine kuhakikisha kila mtu anajua maana ya democrasia ya uchaguzi. Naamini kwa kupitia wasanii ujumbe umefika sana kwa kiwango walicho fanya na mchango umeonekana na naamini heshima lazima iwepo kwao.

Kwa kuzingatia hilo Backyard Studio tulitoa nafasi kwa wasanii kurecords bure nyimbo zinazo husu uchaguzi mkuu kuanzia tarehe 01/07/2010, mpaka week ya uchaguzi mkuu, nashukuru wito ulitimia kwani tulirecord nyimbo zaidi ya hamsini.

Wasanii tunaweza, kwa niaba ya Backyard Studio naomba nitoe tena fulsa ya pekee kwa Wasanii wote nchini iwe vikundi au mmoja mmoja kurecord nyimbo BURE kuanzia tarehe 30/11/2010 hadi tarehe 09/12/2010. Nyimbo hizo ziwe mahususi kwa ajili ya kusaidia, kuhamasisha jamii na kuelimisha kuhusu janga la Ukimwi linalo tukabili. Dhumuni la Backyard kwa sasa ni kusaidia Jamii katika Majanga yote ya kitaifa kwa kupitia Sanaa.

Tunaamini Ukuimwi ni moja ya Janga kubwa sana linalo pelekea Serekali na Jamii kutumia pesa nyingi, muda na maarifa katika kutaka kuogoa maisha ya ndugu na jamaa zetu sambamba na kutokomeza gonjwa hili. Wasanii ni watu muhimu sana na naamini wakiamua kupiga kampeni hii ujumbe utafika na yote haya yana wezekana.

Naomba nyimbo ziwe za kweli zenye uwezo wa kukaa kwa muda mrefu zaidi na ambazo zitavutia jamii kusikiliza na ujumbe kuwafikia pale walipo ndani ya kipindi chote si wakati wa maadhimisho haya tu.

Tuwasiliane hii ili tupeane utaratibu wa kufuata japo hakuna masharti. Ahsante

Braton (Backyard Records)
S.L .P 14663 D'Salaam
Tanzania
+255 713 888 779.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

ANKAL MICHUZI Amwaga somo la nguvu kwa wasanii


Ankal Michuzi (Issa Michuzi) ambaye ni mmoja wa waasisi wa mitandao ya habari ya jamii (blogs) hapa nchini amewashauri wadau wa sanaa hasa wasanii kuanza kuingia kwa kasi kwenye matumizi ya teknolojia hiyo kwani ni njia kubwa ya kujitangaza na kuuza kazi za sanaa kote duniani.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa leo Jumatatu,Michuzi ambaye blog yake ya www.issamichuzi.blogspot.com imepata umaarufu mkubwa kutokana na kutembelewa na watu wengi aliweka wazi kwamba,blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani hivyo wasanii hawana budi kuzitumia ili kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.

Alisema kwamba, blogs tofauti na aina nyingine za vyombo vya habari inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.

Akizungumzia historia ya blogs,Michuzi alisema kwamba ni teknolojia mpya hapa nchini na kwamba,ilianza kwa kuandika habari za kawaida lakini leo hii ni tegemeo katika kupasha habari kwa uharaka zaidi, kuwafikia watu wengi kuliko vyombo kadhaa vya habari na kimbilio la jamii kwani imekuwa kama sehemu ya jamii katika masuala mbalimbali.

Kwa ujumla Michuzi aliwataka wasanii na wadau wa Sanaa kuamka na kuanza kutumia teknolojia hiyo kwani wasanii mbalimbali duniani si tu wamekuwa wakitumia blog katika kujitangaza na kutambulisha kazi zao bali pia wamekuwa wakimilki mitandao na technolojia mbalimbali za mawasiliano.

Katika kuonesha kwamba, teknolojia hiyo ni muhimu Michuzi ameahidi kuwapa mafunzo ya bure wadau wa Jukwaa la Sanaa juu ya kufungua na kumiliki blog ambayo yataendeshwa Ijumaa ya Desemba 10,2010 kwenye Ukumbi wa BASATA.Wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa.

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 29, 2010 | | Permalink | Maoni 4

rais kikwete afanya kikao cha kwanza na baraza lake jipya la mawaziri ikulu leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana kwa mara ya kwanza na baraza lake jipya la mawaziri ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

chadema walia na polisi kupiga marufuku mikutano yao

Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu (MB), akizungumza na wanahabari Jumapili Nov 28, 2010 katika ofisi za Makao Makuu za chama chake Kinondoni jijini Dar es salaam. Alikuwa akizungumzia hatua ya polisi kupiga marufuku mikutano yao nchi nzima.Na GPL.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 29, 2010 | | Permalink | Maoni 3

WAFANYAKAZI UTUMISHI WA UMMA WAMPOKEA WAZIRI HAWA GHASIA LEO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa Ghasia akilakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw.George Yambesi (kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu Bw. Aloyce Msigwa(kushoto) mara baada kuwasili kuanza majukumu yake leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa Ghasia akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisini leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa Ghasia (kulia) akikaribishwa kwa furaha na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa Ghasia akizungumza na viongozi na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo mara baada yakuwasili leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amewataka wafanye kazi kwa bidii ili kuimarisha utendaji katika sekta ya umma nchini.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

hali ya gurumo bado si shwari,ahamishiwa icu.

Galacha Mkongwe wa miondoko ya muziki wa dansi hapa nchini,Maalim Muhidin Gurumo ambaye wiki iliyopita alilazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar hali yake bado si nzuri.

Maalimu Gurumo ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi ya muziki wa Dansi,Msondo Music .alifikishwa hospitalini hapo Alhmisi na kulazwa wodi ya Mwaisela namba 5 akisumbuliwa na mapafu kujaa maji.

Akizungumza jana jijini Dar,mmoja wa ndugu wa Mwanamuziki huyo alisema kuwa Gurumo baada ya hali yake kuwa mbaya ijumaa mchana alihamishiwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa matibabu zaidi.

Alisema Mwanamuziki huyo kwa sasa hawezi kuzungumza kutokana na hali kuwa si nzuri,ndugu huyo alisema anawaomba Wadau wa Muziki nchini,kujitokeza kumsaidia kwa hali na mali na kumuombea ili aweze kupona maradhi yanayomsumbua.Habari kwa hisani ya gazeti la Majira.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Futa kumbukumbu kabla ya kuiuza kompyuta

Unataka kuuza kompyuta yako na kununua mpya,lakini kwenye kompyuta yako kuna kumbukumbu nyingi za muhimu ambazo usingependa mtu mwingine yeyote azipate wala kuziona.Je utafanya nini?

Utafuta kila kitu kwa kubonyeza "Delete" halafu kwenda jalalani(Recycle bin) kufuta kila kitu? Au utaamua kuformat na kuifanya kompyuta yako kufuta kila kitu? Majibu ni mengi na inategemea na ufahamu wa muhusika,ila ukweli ni kuwa kwa njia zote mbili za hapo juu hakuna hata njia moja iliyo salama,kwani kama utatumia njia kama hizo na ukamuuzia mtu mwenye utaalam wa kompyuta,basi ataweza kuzirudisha(recover) kumbukumbu zote ambazo mwenyewe ilizani zimefutika.

Jinsi gani kompyuta inahifadhi kumbukumbu?

Wengi wetu wanaweza wakawa wameshaanza kujiuliza,inakuwaje sio salama wakati nimeshafuta kila kitu toka kwenye kompyuta? Je mtu ataweza vipi kuona mafaili ambayo tayari nimeshayafuta? Ukweli ni kuwa,kwa mujibu wa uhifadhi wa kumbukumbu kwenye kompyuta.Pindi unapofuta au kufanya format(kuweka mtambo endeshi(OS) mpya),sio kweli unayafuta moja kwa moja mafaili na kumbukumbu toka kwenye kompyuta yako.Kitu kinachofanyika ni kuwa unaondoa taswira yake kwenye uso wa mbele wa hard disk hivyo kukufanya wewe uone kama umeyafuta ila bado yanaendelea kuwepo kwenye disk yako.Na hii ndio maana kama kunatokea kesi,wataalam wa uchunguzi wa makosa ya kompyuta(Computer Forensic) huchukua kompyuta yako kwa ajili ya kuifanyia uchunguzi.

Siku hizi kuna program nyingi sana ambazo zina uwezo wa kurudisha mafaili hata yale yaliyokuwepo kipindi ulipoinunua kompyuta kwa siku ya kwanza, mara nyingi jinsi gani unaweza kuyarudisha hayo mafaili hutegemea elimu ya mtu anayefanya hizo kazi ya kuyarudisha,kwani kazi ya kuyarudisha haya mafaili huwa ngumu kutegemeana na jinsi mafaili hayo yalivyofutwa.Mfano faili lililofutwa kwa kubonyeza "Delete" ni rahisi zaidi kulirudisha kuliko lile lililofutwa kwa kuformat kopyuta, vilevile huwa ngumu zaidi kama mtumiajai alifanya mgawanyo wa hard disk (partition) baada ya kuformat. Hivyo leo hii nitakuonehsha njia thabiti za kufuta kumbukumbu toka kwenye kompyuta unayotaka kuiuza ili kuhakikisha unakuwa salama zaidi.

Nitafutaje kumbukumbu moja kwa moja toka kwenye kompyuta ?

Takwimu z inaonesha kuwa mtu mmoja kati ya wanne wamekuwa wakiibiwa siri zao kutokana na kuuza kompyuta bila kufuta kumbukumbu,hivyo kama wewe hutaki kuingia kwenye hilo kundi basi unaweza kufuata hatua zifuatazo. 1.Chukua ile CD uliyopewa pindi uliponunua kompyuta yako,ambapo nyingi huitwa recovery CD.Kama umepoteza hii CD au haukupewa pindi uliponunua kompyuta,basi nenda online na tafuta programu z inazotumika kufuta kumbukumbu(disk-wiping program). Programu hizi zipo nyingi ila binafsi nimewahi kutumia Darik's Boot and Nuke (DBAN) hivyo nakushauri uijaribu hii. 2.Tumia programu kama Nero au yoyote uliyoizoea kuchoma hayo mafaili ya hii programu kwenye CD,kumbuka kuchagua mtindo wa Bootable CD.

3.Weka CD kwenye kompyuta yako halafu irestart. Kompyuta inatakiwa kuitambua hiyo CD pindi tu inapowaka,kutatokea ujumbe kwenye kioo unaosomeka "press any key to boot from CD." Hapo bonyeza kitu chochote kwenye keyboard yako.

Kumbuka: Kama hautouona huu ujumbe unaosomeka"boot from CD" inawezekanika kabisa umekosea katika kuchoma hiyo CD yako,unatakiwa kuichoka kama "Bootable CD". Jaribu tena au wasiliana na mtaalamu wa IT aliye karibu nawe. Kama una uhakika kabisa uliichoma kama Bootable CD,basi inawezekana kuna mabadiliko unatakiwa kuyafanya ili kuiwezesha kompyuta kuitambua CD,haya kwa wasio na utaalam inabidi wawatafute wenye utaalam kidogo ili wakusaidie kubadilisha utaratibu wa BIOS.

Kama unataka kujaribu mwenyewe,basi kompyuta inapowaka tu bonyeza "Delete",baada ya hapo fuata maelekezo na kuingia kwenye "Boot Sequence",iweke CD or DVD kuwa ya juu kabisa kabla ya Hard drive,hapo mambo yatakuwa sawia. 4.Fuata maelekezo utakayopewa na hiyo programu,mara nyingi huchukua masaa kadhaa hadi siku mpaka kufuta kila kitu kilichopo kwenye kompyuta yako.

Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto. Baada ya hapo basi kompyuta yako itakuwa mbichi kabisa na unaweza kuiuza bila utata wala hofu juu ya kumbukumbuku wala usalama wako.

Zaidi Bofya Hapa
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 29, 2010 | | Permalink | Maoni 0

leo liko mitaani kwa sh 400 tu.




 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Monday, November 29, 2010 | | Permalink | Maoni 1

zanzibar heroes yaichachafya sudan 2-0 michuano ya cecafa tusker challange cup

Sunday, November 28, 2010
Ali Ahmed Salum Shibiri akishangilia baada ya kuipachikia bao la pili na la ushindi, timu yake ya Zanzibar Heroes, timu hiyo ilipomenyana na Timu ya Taifa ya Sudan,leo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
MCHEZAJI Elrayan Abdallah wa timu ya Taifa ya Sudan (kushoto) akipambana na Sabri Ramadhani Mzee wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, wakati wa mechi hiyo.Picha kwa hisani ya Chachandu Daily
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, November 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

OFF SIDE KUZINDULIWA CONGO DRC

OFF SIDE


Filamu ambayo inasubiriwa kwa hamu kuingia katika soko la filamu Tanzania, ikiwa inaigizwa na wasanii mashuhuri wa hapa nchini Steven Kanumba, Vicent Kigosi na Irene Uwoya itazinduliwa kwa mara ya kwanza Congo.

Ikiwa inasambazwa na Steps Entertainment, hii inaonekana kwamba wasamabzaji hawa wanajribu kupanua soko kwa kuweza kushirikisha wadau wengi katika filamu. Kuvuka mipaka ni hatua kubwa katika Tasnia ya filamu Tanzania.

Steven, Vicent na Irene wataelekea huko wakiambatana na wasamabzaji wao na utafinyika uzinduzi mkubwa na wa mara ya kwanza kutokea katika Tasnia ya filamu Tanzania. Steven na Vicent wanaandika historia Tena.Congo kaeni mkao wa kula, Filamu hilo linakuja
OFF SIDE

OFF SIDE

Zaidi Bofya Hapa upate mambo mbalimbali yahusuyo Filamu

 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, November 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

Kaumia yatangulia redioni, Njiwa kwenye luninga


BENDI ya K-Mondo Sound sasa imeamua kufanya mashambulizi ya kujitangaza baada ya kuamua kuachia nyimbo mbili kwa mpigo mmoja ukienda kwenye redio na mwingine kwenye televisheni.Kiongozi wa bendi hiyo, Richard Mangustino alisema mjini Dar es Salaam

mwishoni mwa wiki kuwa baada ya kutengeneza video za Njiwa na Your Still Mine waliona watangulize wimbo mmoja kwenye redio huku mwingine ukipelekwa kwenye redio.“Tangu Mhina (Panduka) ajiunge na bendi yetu, wimbo wake wa kwanza kutunga akiwa na K-Mondo sasa tukaona tuupeleke redioni ili watu wamsikie mkongwe huyu akiwa anatambaa na mduara,” alisema.

Kuhusu video, alisema wamepeleka kwanza Njiwa kutokana na kuiangalia Your Still Mine na kuona inatakiwa kuongezewa vitu vingine. “Njiwa kwa mara ya kwanza tuliitambulisha kwenye mtandao wa FaceBook, tulipata maoni mbalimbali ambayo yakatupa moyo na tukaamua
kuipeleka moja kwa moja kwa Televisheni,” alisema.

Mangustino alisema wamejipanga vizuri kwa ajili ya uzinduzi wao ambao utafanyika mapema mwakani. Alisema kwa sasa bendi yao inafanya maonyesho yake kila Ijumaa katika ukumbi wa Triz Motel uliopo Mbezi wakati Jumamosi wanahamia City Hotel pia Mbezi Beach, Dar es Salaam.
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, November 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

NA & NA INTERNET CAFE 24 - HRS OPEn.

Baadhi ya awadau wakiperuzi

"NA & NA INTERNET CAFE 24 - HRS OPEN"

KIOTA SAFI KWA MATUMIZI YA INTERNET, NA MAHITAJI YA STATIONARIES, PIA TUNATOA HUDUMA ZA INTERNET WIRELESS SERVICE KWA WALE WENYE LAPTOP,KWA HUDUMA YA HARAKA NA SAFI KABISI KATIKA TEKNOLOGIA YA MTANDAO WA INTERNET NA & NA INTERNET NDIO SEHEMU PEKEE YA KUPATA HUDUMA HIZO. NI INTERNET PEKEE INAYOFANYA KAZI KWA SAA 24 KWA KUJALI WATEJA MUDA WOWOTE.

HUDUMA ZINGINE NI KAMA :

- Photocopy, -Lamination, -Scanning, -Printing, -Fax nk.

TUPO SINZA -AFRIKA SANA - PEMBENI YA DUKA LA NGUO LA ZIZZOU FASHION au opposite na Corner Bar

KARIBUNI WOTE
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, November 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0

DIAMOND AFANYA MAKAMUZI YA MWISHO COVENTRY

Diamond akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake.
Diamond akiwarusha vilivyo washabiki wake

DIAMOND afanya makamuzi yake ya mwisho UK kwenye jiji la Coventry Katika nyanda za Midlands. Shoo hiyo ambayo ni part ya Urban Tour iloyofanyika katika miji tofauti ya UK , Urban Tour imeandaliwa kusaidia vita dhidi ya Malaria. Urban Tour iliandaliwa na kampuni inayo milikiwa na Baraka Baraka, Frank Eyenbe na Nocha Sebe ambao ni vijana Wakitanzania waishio UK inajulikana kama URBAN PULSE CREATIVE MEDIA..
 
Muandishi: MICHUZI JR Tarehe: Sunday, November 28, 2010 | | Permalink | Maoni 0
Idadi ya watu